Serikali imetoa tamko juwa tarehe za kufanya mitihani ya kidato cha nne na sita sasa itaongezwa muda ilikuongeza muda wa wasahihishaji kusahihisha kwa ufasaha na umakini zaidi
ZITTO:NARUDIA TENA SIGOMBEI URAISI 2015
Sep 28, 2012
Na hiki ndicho alichokiandika zito kabwe katika fanpage yake kuhusu kugombea ama kutogombea uraisi 2015
Dr.PAUL SWAKALA MWENYEKITI WA MADAKTARI WALIOATHIRIKA NA MGOMO AMWANGUKIA JAKAYA
Sep 17, 2012
MADAKTARI INTERN WAMWANGUKIA JK KUFUATIA KUSHIRIKI KWAO KATIKA MGOMO WA MADAKTARI.
Hawa ndio waliomwua mwandishi wa Channel Ten huko Iringa
Sep 2, 2012
Naomba mniruhusu niweke picha zenye sura za walioshiriki kitendo hiki cha kihuni ambacho ni uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu kama kamera yangu ilivyokinasa.
Nina picha ambazo zimechukuliwa zinazoonyesha walioshiriki na jinsi walivyoshiriki. Hata RPC alikuwepo eneo la tukio.
Mods, naomba msiunganishe thread yangu plz.
Picha nyingine nimezituma kwa watetezi wa haki za binadamu na video nimeziweka YouTube (sitatoa link kwa sasa).
Wanahabari, ni wakati wa kuonyesha umoja wetu dhidi ya udhalimu huu.
-----
Huyu askari alimwelekezea mtutu tumboni na kumsambaratisha marehemu. Ni wazi watu wa Iringa wanamfahamu askari huyu.
Pembeni ni shangingi la RPC, askari huyu naye kashuhudia kitendo hiki cha kikatili. Wanahabari tushirikiane kupiga kelele. Hapa walikuwa wamemaliza unyama wao wakimwondoa mwenzao aliyeumia eneo la tukio
Maiti ilisambaratishwa kabisa utumbo, si uungwana kuweka picha kama hizo hapa.
Kama ni kesi, askari huyu anaweza kuhojiwa. Nimekata picha kusitiri mwili wa marehemu.
Marehemu kafa akipigania haki za wanahabari, ni wakati wa wanahabari kushirikiana vinginevyo wanasiasa wataendelea kutumia vibaya vyombo vya dola dhidi yetu.
Subscribe to:
Posts (Atom)