Pages

SHARO MILLIONARE BAADA YA AJARI ALIFANYIWA KITU MBAYA

Nov 27, 2012
Kwa habari zilizopo ni kwamba baada ya ajali ilyomtokea Msanii wetu kipenzi cha wengi Hussein Mohammed Mkieti maarufu kama Sharo Millionaire watu wenye roho mbaya zisizofanana na za watu walivyofika katika eneo la tukio na kubaini kuwa msanii huyo ameaga dunia walimpekua kila kitu alichokuwa nacho mfukoni na kutokomea navyo na pia waling'oa vitu flani vya gari na kuondoka navyo.
 Haya ni mambo ambayo yanatokea sana pindi zinapotokea ajali imekuwa ni kitu cha kawaida sana kwa Hawa wanadamu wa sasa.
kwa mujibu wa maelezo ya kina kutoka kwa rafiki wa karibu sana na Marehemu ambaye pia ni mwigizaji mchekeshaji maarufu kama KITALE ameelezea kile ambacho kilikuwa kinampeleka Sharo Millionaire Nyumbani kwao TANGA kuwa alikuwa anampelekea mama yake hela za Biashara ambazo zilikuwa shilingi Million Sita (6 000 000Tshs).
Kama utakuwa ni mtu mwenye busara utasikitika sana kuwa ni kiasi gani kijana huyo alikuwa akimjali mama yake tofauti na vijana wengi wa sasa ambao wamekolewa na starehe na kuwasahau wazazi wao ila kwa kazi ya Mungu inawezekana pia Hela zote hizo wameziiba hao Majangili wasiokuwa binadamu na wametokomea nazo.
Ni pigo kubwa sana kwa mama wa Sharo Millionaire, Familia yake, Tasnia ya filamu na Muziki lakini pia kwa Watanzania kwani Sharo alikuwa akipendwa na watu wa marika yote Nchini na Hajawahi kuhusishwa na skendo zinazomshusha thamani mtu yeyote.

Kutokana na Maombi ya watanzania walio wengi wameomba mazishi ya Msanii huyo yafanyike kesho na Familia ya Marehemu imekubali kuwa Mazishi yanafanyika Kesho Tar. 28-11-2012 huko kijijini kwao Wilayani muheza Mkoani Tanga.
Ikumbukwe kuwa wiki iliyopita tumepoteza pia wasanii wawili wa filamu Nchini ambao ni MLOPELO  na JOHN MAGANGA ambaye anzikwa leo tar 27-11-2012 huko jijini Dar-es-Salaam makaburi ya kinondoni. 

SWALI LANGU NI UBINADAMU GANI WALONAO WANADAMU KUMWIBIA MAREHEMU????

HUU NI MWAKA MBAYA SANA KWA TASNIA YA FILAMU TANZANIA-----
R.I.P SHARO MILLIONAIRE