Pages

SABABU KUU ZA DR KABANGILA KUJIUZURU (MAT)

Dec 2, 2013
Picture: Dk Rodrick Kabangila
 Katibu Mkuu na baadaye President-Elect wa Chama cha Madaktari Tanzania, MAT, Dk Rodrick Kabangila ametangaza rasmi kujivua na kujiudhulu nyadhifa zake zote ndani ya chama hicho cha kitaaluma, na kutangaza kujinga rasmi na chama cha siasa, CHADEMA.

Katika taarifa iliyooneshwa na runinga ya Star-Tv, Dk Kabangila amesema kuwa kwa mujibu wa sheria, imembidi kuamua kufanya lililo sahihi na sasa amejiunga rasmi ili kupata wigo mpana wa kupigania maslahi ya fani, madaktari na wananchi.