Mama aliyefunga ndoa na mwanae wa kumzaa wa kiume baada ya mumewe ambaye ndiye baba wa mtoto huyo kufariki amesema anawashangaa wanadamu kuingilia mapenzi yao huku mwanae akiwauliza watu mnatutakia nini kwenye mapenzi yetu? akiongeza kuwa mapenzi anayopata kwa mama yake hajawahi kuyapata.
Bi Condorada Ngonyani mwenye umri wa miaka 70 ambaye alifunga ndoa na mwanae wa kiume ameibuka na kusema anawashangaa watu wanaowasimanga kwa mapenzi yao moto moto kati yake na mwanae huyo wa kiume Bw. Joseph Mapunda.
Mama huyo na mwanae waliwekwa kitimoto na wanakijiji waliohoji mapenzi hayo haramu kati ya mama na mwanae. Tukio hilo la kuwaanika hadharani mama na mwanae liliandaliwa uongozi wa serikali ya mitaa.
Mama Condorada Ngonyani (70) mkazi wa mkoani Ruvuma, aliamua kufunga ndoa na mtoto wake wa tatu wa kiume wa kumzaa na kisha kuishi naye kinyumba kama mke na mume.
Wawili hao hawajutii kitendo chao na wameonekana kuona walichofanya ni sahihi na kuwashangaa wanadamu, majirani zao na jamii kwa ujumla kuingilia mapenzi yao.
Wananchi wapatao 400, wa mkoa wa Ruvuma walijitokeza kushuhudia kimbwanga hicho wakati uongozi wa Serikali ya mtaa walipoamua kuwafuatilia na kuwahoji na kuitisha mkutano wa wanakijiji na kuwaweka hadharani.
Wananchi wa mkoa wa Ruvuma wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Maendelo ya Jamii, Jinsia na watoto, kufuatilia kwa karibu suala hilo na kuwaondoa hofu wananchi kama kuna sheria inayomruhusu mtoto na mama Mzazi kuweza kuishi kindoa.
Alipohojiwa mama huyo, Condorada Ngonyani, alisema kuwa mara tu baada ya kufariki mume wake, Mzee Mapunda, yeye aliamua kumchagua mtoto wake huyo Joseph Mapunda, ili amrithi baba yake katika kuumiliki mwili wake kama ambavyo alikuwa akifanya Baba yake mzazi, ili kuondokana na tamaa na vishawishi wa kiulimwengu.
Alisema kuwa baada ya uteuzi huo walifunga ndoa ya kimila japo kuna baadhi ya wanafamilia hawakufurahishwa na tukio ama jambo hilo, lakini yeye aliamua kufunga masikio na kuamua kuvunja amri ya sita na mtoto wake huyo wa kumzaa.
Tukio hili ni mara ya kwanza kutokea kwa mkoa wa Ruvuma na hata kwa Tanzania nzima, ambapo wakazi wa Ruvuma wamekuwa wakibaki na maswali mengi juu ya tukio hilo na kuhoji jamii sasa inaelekea wapi kwa baadhi ya Watanzania kuibomoa wenyewe mila na desturi zetu.
Kwa upande wake, Joseph Mapunda, yeye anasema kuwa upendo na mahaba anayoyapata kutoka kwa mkewe huyo ambaye ni mama yake mzazi, hajawahi kuupata kokote na kusema kuwa wanapendana sana na wanaheshimiana kama mke na mume.
Josepha amehoji kulikoni wanadam kuwafuatilia katika mapenzi yao na kusema kuwa "hawa watu wanaotufuatilia hadi leo hii kutuweka hadharani namna hii, wanataka nini kwetu?".
Wananchi hao waliofurika kwa Mganga wa Jadi Flora Ndembo, wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma, wameiomba Serikali kuingilia kati suala hilo na kuchukua hatua kisheria ili iwe fundisho kwa Watanzania wengine wenye akili kama hizo za kuharibu mila na desturi za kitanzania kirahisi kama hivyo