Mfanyakazi wa Barrick mwaathirika wa kemikali afariki
Oct 29, 2012
Samuel alifariki Oktoba 25 saa 2:00 usiku.
MFANYAKAZI wa Kampuni ya Africa Barrick Gold aliyekuwa akifanya kazi mgodi ya Bulyanhulu, wilayani Kahama, Mkoa wa Shinyanga, Samuel Kamudulu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu akisumbuliwa na mapafu na uti wa mgongo.
Akizungumza kwa simu kutoka Arusha, kaka wa marehemu, Lekiu Kamdulu alisema Samuel alifariki ghafla walipokuwa Arusha baada ya kutoka matibabu Dar es Salaam.
“Samuel alifariki Oktoba 25 saa 2:00 usiku. Unajua baada ya kumwandikia ile habari kwenye gazeti la Mwananchi, kampuni ilimchukua na kuanza kumtibu. Kwa hiyo tuliitwa Kahama tukafanyiwa utaratibu na kurudishwa tena Dar es Salaam kwenye matibabu,” alisema Kamudulu na kuongeza:
“Baada ya kutoka kwenye matibabu tulikuja Arusha nyumbani tangu wiki iliyopita hadi alipofariki juzi.”
Wakati wa uhai wake, Samuel alisema mapafu yake yameathiriwa na kemikali zinazotumika kwenye uchimbaji madini ya dhahabu.
“Mapema mwaka huu nikiwa kazini ndani ya mgodi niliishiwa nguvu ghafla na kuanguka. Nilibebwa bila kujitambua na kupelekwa hospitali ya kazini na kuambiwa kuwa nina ugonjwa wa mapafu (pneumonia),” alisema Samuel wakati wa uhai wake na kuongeza:
“Baada ya hali kuzidi kuwa mbaya nililetwa Hospitali ya Aga Khan ambako nimeambiwa mapafu yangu yameoza kutokana na kemikali zinazotumika mgodini.”
Alipoulizwa kuhusu kifo hicho, Ofisa Habari wa Barrick, Nector Foya alisema hana taarifa za kifo cha mfanyakazi huyo.
Alipoulizwa kuhusu kifo hicho, Ofisa Habari wa Barrick, Nector Foya alisema hana taarifa za kifo cha mfanyakazi huyo.
HII NDO HALI HALISI KILIMAHEWA MWANZA
Oct 26, 2012
Mifereji ipitishayo maji yatiririkayo ni midogo na mingi imeziba hivyo maji yanakatiza katikati ya barabara na kuharibu miundo mbinu. |
Katika maeneo mengine maji yamatengeneza madimbwi makubwa katikati ya barabara. |
Ni kama hakuna barabara vile.... |
Barabara zinapogeuka kuwa.... |
Wenye nyumba zao maeneo haya na kuta za nyumba zao.... |
Mbele ya shule ya chekechea... |
Yahitaji mahesabu wakati wa kuvuta hatua... |
Mbele ya mjengo |
Mbele ya maduka.... kwenye barabara hizi zenye kilio cha miaka nenda rudi.. |
Tuliwakumbusha, CCM Wajihadhari Na ‘Fedha Za Bhangi
Oct 26, 2012
SIKU zote Waswahili wanasema: “Msemea sikioni siyo majinuni!” Hata hivyo, ni wachache wanaoweza kuzingatia yale wanayoambiwa na daima wanapoyafanyia kazi huwa wanapata matokeo mazuri.
Suala la rushwa ndani ya Chama cha Mapinduzi limekuwa sugu, wenye fedha wamekuwa wakilangua kura ili kupata uongozi, hata kama hawana sifa stahiki. Lakini pamoja na ‘Wenye hekima wa Babeli’ kutahadharisha madhara ya mchezo huo mchafu, bado wahusika wameziba masikio kwa nta, hawataki kusikia la Muadhini wala Mnadi Swala!
Matokeo yake CCM limekuwa kokoro kama alivyopata kusema Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere. Kokoro linalovua samaki na konokono kwa pamoja, na inahitajika busara na hekima kuweza kuchambua samaki na konokono hao ambao ni hatari mno.
Uongozi ndani ya CCM ni sawa na kutangaza zabuni, ambayo mwenye fedha nyingi ndiye anayeshinda na kupewa uongozi huo. Rushwa imekuwa kansa mbaya ndani ya CCM, fedha zinamwagwa nje nje na viongozi wao wanaangalia na kuchekelea, wanakemea rushwa na tabasamu pana kana kwamba ni kitu cha kawaida tu. Hii ni aibu kwa chama kikongwe na chenye dhamana ya kuongoza Taifa!
Soma zaidi... www.kwanzajamii.com/?p=4111
Subscribe to:
Posts (Atom)