Pages

HIKI NDICHO KILICHOTEKEA JANA KWENYE VURUGU ZA MACHINGA NA ASKARI WA JIJI LA MWANZA

Nov 16, 2012

Polisi wakiwa kwenye doria eneo la tukio.
 Mtu mmoja ameuawa na wengine wawili kujeruhiwa kufuatiaa vurugu zilizotokea leo majira ya saa tano asubuhi  katika eneo la barabara ya Pamba karibu na soko kuu la jijini Mwanza katika vurugu baina ya wafanyabiashara wadogo maarufu kama wamachinga na askari wa Halmashauri ya jiji la Mwanza.

Mtu huyo ambaye jina lake kamili halikupatikana badala yake ametambuliwa kwa jina moja tu la Greda.

Taarifa zaidi zinasema kuwa leo mnamo majira ya saa nne na nusu asubuhi askari wa halmashauri ya jiji la Mwanza wakiwa katika maeneo yao ya kazi eneo la barabara ya Pamba kwenye stendi ya zamani ya mabasi ya Tanganyika karibu na soko kuu la jiji hilo, wakiwa katika operesheni zao za kawaida za kusafisha jiji walikamata bidhaa zilizokuwa zimepangwa katika maeneo ambayo hayaruhusiwi kisheria wakiwa kwenye eneo hilo mtu mmoja ambaye anadaiwa kuwa ni mmachinga alimrukia mgambo wa jiji shingoni na kumtolea silaha ya jadi aina ya sime kwa nia ya kumdhuru.

Maganda  ya risasi zilizo tumika.
 Baada ya tukio hilo wamachinga waliokuwa eneo la tukio walianza kuwarushia mgambo hao wa jiji mawe ndipo wale mgambo wa jiji katika kujihami wakaanza kurusha risasi hewani kuwatawanya wamachinga hao  waliokuwa wakiongezeka kadri kuanza kwa seleka hilo, kwa bahati mbaya moja kati ya risasi hizo zikampiga mpiga debe mmoja upande wa kushoto na kufariki papo hapo.

 Machinga mwingine amejeruhiwa kwenye mkono wa kushoto katika kiwiko, naye dereva wa magari ya  biashara za kusafirisha mizigo wa gari aina ya Kenta, magari ambayo hupaki katika eneo hilo amejeruhiwa upande wa kushoto kichwani na kukimbizwa hospitali ya rufaa Bugando kwa matibabu. 



Mmoja wa viongozi wa akiwatuliza wamachinga wenzake kupata kumsikiliza mkuu wa polisi (OCD) wa wilaya ya Nyamagana Ally Kitumbu. .

Msikilize kwa kubofya play..
Mkuu wa polisi (OCD) wa wilaya ya Nyamagana Ally Kitumbu. akizungumza na wafanyabiashara hao wadogo (wamachinga) kuendelea na kazi kwa kufuata sheria wakati jeshi hilo likifanya uchunguzi wa tukio hilo.

Msikilize kwa kubofya play...
Maduka mengi hususani yaliyo karibu na eneo la tukio yamefungwa kufuatia seleka hilo.

Makutano ya barabara za Liberty na Nyerere ambalo muda wote huwa na pilikapilika za kibiashara likionekana tupu kutokana na vurugu hizo zilizo sababisha wafanyabiashara kukimbia na kufunga biashara zao kuhofia vurugu hizo.

Mmoja kati ya viongozi wa wamachinga akizungumza na wenzake kuwasihi kulinda utulivu ili haki yao isipotee.
Read more ...

MAJANGA HAYA; ANGALIA PICHA NAMNA : KIJANA WA ROMBO AFYEKA NYETI ZAKE, KISA NI MADEMU

Nov 16, 2012
Kijana Priva Elian wa Rombo mkoani Kilimanjaro, amefyeka sehemu zake za siri na kuziondoa, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kugombaniwa na wanawake wawili.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo, walidai kijana huyo alifikia uamuzi huo baada ya wanawake wawili kumgombea.
Walidai kuwa alifikia uamuzi , mwaka huu saa 1:30 asubuhi baada ya kupandwa na ghadhabu kutokana na usumbufu mwingi aliokuwa akiupata kutoka kwa wanawake hao.
 

Walieleza kuwa mara baada ya kuchukua uamuzi huo, alimwita mdogo wake ambaye hakutambulika jina na kumweleza kuwa achukue viungo hivyo na kuwapelekea wanawake hao ili wavigombee.
 

“Hatujui alitumia kifaa gani kujifyeka kwani kinaonesha ni kikali sana, kwani baada ya kukata sehemu hizo nyeti, alimpa mdogo wake ili awapelekee wanawake hao kwani ndicho kitu muhimu kwao na siyo yeye,” alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo la kusikitisha.
Read more ...

OMMY DIMPOZ AACHIA KICHUPA KINGINE

Nov 15, 2012

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Ommy Dimpoz aachia nyimbo yake mpya anayokwenda kwa jina la You and Me.
Read more ...

BANZA NAE AANZA MBWEMBWE

Nov 15, 2012

"Siku hizi dunia imebadilika sana yani nimeshasahau hata jinsi ya kutongoza"Hii ni kauli ya Mwanamziki Nguri wa Bendi ya Extra Bongo,Ramadhani Masanja a.k.a Banza Stone ambaye alijinadi kuwa amekuwa akipata kero kutokana na kutongozwa na idadi kubwa ya wanawake.
Read more ...

MMACHINGA MMOJA AUAWA

Nov 15, 2012
Mmachinga mmoja ameuawa kwa kupigwa risasi kufuatia vurugu kati ya Askali wa jiji na Wamachinga wa Jiji la Mwanza.
Read more ...

HALI YAZIDI KUWA MBAYA KUFUATIA VURUGU ZA MACHINGA NA ASKALI WA JIJI LA MWANZA

Nov 15, 2012
Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema vurugu hizo zilianza baada ya Machinga mmoja kuzuiwa kupanga bidhaa katika eneo la Makoroboi mwanza na mtu ambaye anasemikana na mmiliki wa eneo hilo. 
Read more ...

MISHAHARA YA WACHEZAJI ZA MANCHESTER CITY

Nov 15, 2012

Read more ...

DIAMOND AFUNGUKA KUHUSIANA NA KILICHOSABABISHA AJALI YAKE

Nov 14, 2012
Add caption
Read more ...

MREMBO AANIKA NYETI ZAKE BAADA YA KUNOGEWA NA EBSS 2012

Nov 14, 2012
Si jambo la kushangaza sana  kusikia flani ameanika nyeti zake nje kwani hapa Bongo imekua kama fasheni au ni njia nyingine rahisi ya kukuzia jina.Binti huyu aliyekua anatumia aina flani ya kilevi alinaswa katika usiku wa EBSS 2012 akiwa ameanika nyeti zake nje.
Read more ...

yg

Nov 14, 2012

Read more ...

NA HII NI TRAILER YA MAGIC MONEY AMBAYO INATARAJIWA KUFANYA VIZURI

Nov 12, 2012

 ''PESA SHETANI ASIYE EPUKIKA KATIKA DUNIA YA SASA NA USIOMBE ABISHE HODI NDANI YA FAMILIA KABISA'' 
...KUMKANYWA NA KUPEWA TAHADHALI KWA MTU NDIYO KUMTIA HAMASA NA MUWASHAWASHA KUITIKIA KIU YA NAFSI YA TAMAA YA PESA . 
MAISHA YA KUKIMBIA NDIYO MATOKEO YAKE KAMA SIO KUKOSANA NA NDUGU AU MPENZI/MUME/MKE WAKO... BASI MTIZAME BINTI HUYU NAMNA NDOA YAKE INAVYO TIBULIWA NA SHETANI  HUYU (PESA).

HILI NDILO KASHA JIPYA LA FILAMU YA MAGIC MONEY ITAKAYOINGIA SOKONI MWEZI HUU
HILI  NDILO LILIKUWA  KASHA LA FILAMU HII YA MAGIC MONEY KABLA YA KUINGIA SOKONI

Read more ...

ALICHOKISEMA WALTER BAADA YA KUWA MILLIONARE.....

Nov 11, 2012
Akiongea na media moja maarufu hapa nchini walter amesema hakuwahi kufikiri kuwa na mafanikio kama haya .ila tu nguvu za mungu zimemmulika,na kuongeza kusema kuwa yupo tayari kukabiriana na miki ya game la bongo.

Read more ...

Taswira Kwenye Kikao Cha NEC CCM

Nov 11, 2012

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akisalimiana na MNEC Wilaya ya Monduli, Mh. Edward Lowassa jioni ya leo katika ukumbi wa NEC-Dodoma.

 
 
 

Waziri Mkuu mstaafu Mh. David Cleopa Msuya akibadilishana mawazo na Mh. Abrahaman Kinana leo kabla ya kuanza kwa kikao cha NEC.

 

Mjumbe wa NEC akipitia gazeti la Mzalendo toleo maalum linalozungumzia mkutano mkuu wa CCM .

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha wajumbe wa NEC Dodoma leo, kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama.

 

Read more ...

MASHARTI YALIYOTOLEWA NA SIR CHANDE KUHUSU JINSI YA KUJIUNGA NA FREEMASON

Nov 11, 2012


Sir Andy Chande akifanya interview na Gerald Hando wa Clouds Fm.
Kuna idadi kubwa ya watu waliohitaji kufahamu Freemason ni nini baada ya taarifa kuenea kwamba Freemason ni dini ya kishetani na watu wengi maarufu wamo humo wakiwemo viongozi wa nchi na mastaa wengine kama Jay Z, Rihanna, Beyonce, Kanye West, Celine Dion na hata hapa Tanzania june 2012 magazeti ya udaku yaliwataja wasanii kama Diamond Platnums na Jackline Wolper kwamba wamo humo lakini wasanii wenyewe walikanusha.
Clouds TV/Radio kupitia kwa mtangazaji Gerald Hando ilipata nafasi ya kufanya mahojiano na Sir Andy Chande ambae aliwahi kuwa kiongozi mkuu wa Freemason Afrika Mashariki kwenye nchi za Tanzania, Uganda, Kenya na Seychelles.
Yafuatayo hapo chini ni maelezo aliyoyatoa.
ALIKOANZIA SIR CHANDE:
Sir Chande: Alifika Tanzania mwaka 1950, alihamia Dar es salaam 1953 na kukutana na watu wengi wa bandarini, shirika la reli na mashirika mbalimbali aliyofanyia kazi na alikutana na watu wengi ambao walikua wanahudhuria vikao vya freemasons, akaanza kuuliziaulizia na akajifunza mambo kadhaa kuhusu hao watu.
Kwa wakati huo, hao watu hawakua huru kuzungumzia Freemasons kama anavyofanya chande sasa hivi, haswa kabla ya vita ya pili ya dunia.
Sir Chande anasema wakati huo Freemasons ilikua imegawanywa kwenye makundi tofauti, katika mahospitali, shule, na mashirika mbalimbali na kulikua na kundi maalum la freemasons kwa ajili ya matajiri na wafanyakazi wakubwa wa serikali, ukiangalia vizuri wengi wao walikua wazungu na baadhi ya wahindi.
Kundi la kwanza lilikua linaongozwa na watu wa Scotland, makundi mawili yaliyofata yalikua yanaongozwa na waingereza na kundi la nne lilikua linaongozwa na wahindi ambalo kundi la nne ndilo Chande alilojiunga nalo nalo, ilimchukua miaka miwili kukubaliwa kujiunga na freemason, aliapishwa rasmi rasmi mwaka 1954 akiwa na umri wa miaka 28, kumbuka kwamba masharti ya kujiunga na freemasons ni lazima uwe na umri kuanzia miaka 21.
Baada ya hapo ndipo alipoanza kupenda Freemasons ambapo pia alipanda cheo na kupewa nafasi ya kuongoza kundi au tawi la freemasons katika nchi nne ambazo ni Kenya, Tanzania, Uganda na sychels na akajiunga na miradi tofauti ya freemasons nchini uingereza yakiwemo mahoteli ya kifahari pamoja na kupewa jukumu la kujenga hoteli mpya ya freemasons nchini Ghana kwenye mji wa Khumasi ambayo ni ya kifahari sana.
Hoteli nyingine ya kifahari alisimamia ujenzi wake iko Zambia.
Sir Andy Chande kwa sasa ni mstaafu wa freemasons, 2005 alistaafu kuwa kiongozi wa Freemasons Afrika Mashariki baada ya kuifanyia kazi kwa miaka 19, kwa sasa haudhurii mikutano ya hizi nchi za Afrika Mashariki lakini anahudhuria mikutano ya Uingireza kwa sababu bado anafanya kazi na baadhi ya mashirika Uingereza.

Kanye west, Jay Z na Rihanna.
FREEMASONS NI NINI?
Ni taasisi ambayo ilianzishwa miaka 350 iliyopita katika njia ambayo haikua rasmi ikaja kuhalalishwa miaka 300 iliyopita, hatujui vizuri ilianzishwa vipi ila inaaminika walikua wajenzi wanaojenga mashule, makanisa, wakati ule kulikua hakuna miji mikubwa kama sasa wala mahoteli, na wao walikua wakiishi pamoja na familia zao na wakihama wanahama pamoja, wakaanzisha miradi ya kujenga hoteli ndogo ndogo ili kusaidiana kama wajenzi na kujikwamua kiuchumi, wakawa wanafundishana.. yani kama una ujuzi unamsaidia na mwenzako kujua.
Anasema “Freemasons sio dini na tukikuta wewe ni mkristo tunakushinikiza ukristo wako, kama wewe ni mhindu unabaki kuwa mhindu, lakini freemasons orijino ilianzishwa na wakristo nchini Uingereza na baadae ikahamia Ulaya, Marekani, Australia na India Freemasons ikaja kuwa kubwa sana”
NCHI ZA AFRIKA AMBAZO FREEMASON NI KUBWA:
Kwa nchi za Afrika Freemasons imekuja kuwa kubwa kwenye nchi kama za Nigeria na Ghana pia Sierra Leone, kwanza aliyewahi kuwa rais wa nchi hiyo Daudi Jawala alikua mmoja wetu.
Freemasons ilianza mwaka 1646 alafu ikaja kuwa rasmi mwaka 1717 lakini kabla ya hapo katikati ilikua inafanywa kimya kimya.
KAZI ZINAZOFANYWA NA FREEMASON
Kazi zinazofanywa sasa hivi na Freemasons ni kufundisha wanachama wake kuhusu majukumu yao kwa mwenyemwezi Mungu, kwa nchi yako, familia, na nchi unayofanyia kazi hata kama ni ugenini, na kutoa misaada.

Rihanna.
WANACHAMA WA FREEMASONS DUNIANI:
Duniani kote sasa hivi kuna wanachama milioni tatu laki tano wa freemasons na wanachangia dola za kimarekani zaidi ya milioni 400 kwa ajili ya misaada kila mwaka, yani kwa siku ni zaidi ya dola milioni moja kusaidia afya, elimu vilevile wajane wa wanachama wa freemasons wanasaidiwa ambapo pia ukiumwa na ukiwa na shida yeyote kuna msaada wa bure unapatiwa nakumbuka hata dr Charles Matwali alipoumwa sana, tulimpeleka uingereza kwa matibabu.
JINSI YA KUJIUNGA NA FREEMASONS:
Ili kujiunga ni lazima uwe na umri wa miaka 21, ni hiari kujiunga na pia uwe unamwamini Mungu haijalishi ni Mungu gani, watu ambao hawamuamini Mungu hawaruhusiwi kuwa Freemasons, na lazima uwe mtu mkweli.
Ni lazima familia yako ikubali pia wewe kujiunga na freemasons kwa sababu freemasons hawatokubali kujiunga kwako kukufanye uwe masikini kutokana na kutoa misaada.
Unapotaka kujiunga ni lazima upeleke maombi yako kwa mtu unaemfahamu ambae yuko Freemasons, au kama hujui mtu unaandika barua baada ya hapo utapewa nakala za kusoma na kuelewa na kamati ya kukuruhusu kuingia kwenye freemasons itakupeleleza wewe na familia yako, na pia watakutembelea nyumbani kuongeana mkeo au mumeo au familia.
Inaweza kuchukua mwaka mmoja na nusu au mwaka kuruhusiwa kujiunga na freemasons baada ya kupeleka maombi, ambapo hapo ni kukubaliwa tu, baada ya hapo ili uwe freemason kamili kuna vyeo vitatu ambavyo tunaviita degrees ambavyo ni lazima uvikamilishe jambo ambalo linaweza kuchukua zaidi ya miaka miwili.

.
BAADA YA KUJIUNGA:
Pia unatakiwa kujifunza vitu vingi na kuvihifadhi kichwani kama vile maneno ya kusema wakati unafanya ibada za freemasons kwa sababu tukiwa pamoja tunavyozungumzia sifa za kuwa binadamu kamili unaweza ukafananisha na ibada ya kanisani.
KUHUSU FREEMASON YA UINGEREZA:
Acha nizungumzie Freemason ya Uingereza ambayo mimi ni mmoja wao, Makao makuu yako London kwenye barabara inaitwa great queen street, Mkuu wa Freemasons Uingereza ni binamu yake malkia Elizabeth ambae tunamuita Grandmaster.
Kazi zote zinazofanyika na Freemasons zinaendeshwa kutoka kule, kwa mfano mv bukoba ilivyozama nilipiga simu kule kuomba msaada wakatuma pound elfu 10 ingawa na sisi hapa tuna kitengo chetu cha misaada ambayo kilichangia, maamuzi ya misaada mikubwa yanatoka Uingereza.
Kuna mahoteli ya freemasons Uingereza, Scotland na Ireland na katika nchi zilizokua za kisovieti zamani, tuna mahoteli duniani nzima ambapo kama upo kwenye freemasons ya Dar es salaam unaweza kuhudhuria vikao kwenye yeyote kati ya hizo hoteli duniani tunazomiliki ambazo zinatumika pia kama kumbi za mikutano yetu ili mradi wawe na uthibitisho kwamba wewe ni mmoja wetu.
Watu wengi huwa wanasema ni taasisi inayofanya mambo yake kwa siri lakini ukweli ni kwamba siri pekee iliyopo ni jinsi nitakavyokutambua kama wewe ni mmoja wetu, vingine vyote viko wazi na vinapatikana hata kwenye internet na unaweza kwenda kwenye maduka ya vitabu kote afrika mashariki hata uingereza ukapata nakala zote za freemasons ikiwemo hata maneno tunayosema tukifanya ibada zetu.
Kwa afrika Mashariki makao makuu ya freemasons yako Nairobi Kenya kwa sababu aliechukua nafasi yangu yuko Nairobi na pia makamu wake yuko Nairobi, Kuna majumba 50 ya freemasons Afrika Mashariki
Ingawa makao makuu yako Nairobi, jumba la Dar es salaam linajitegemea lenyewe na tunafanya miradi yetu na kusajili watu wetu hapahapa, hatuingiliwi na ofisi ya Nairobi, maamuzi yetu yanafanyika hapa hapa.

Hapa ni Freemasons Hall Dar es salaam ambapo Sir Chande anasema kuna masonic lodge nne Dar es salaam. (Picha imepigwa na blog ya samsasali)
FREEMASONS WANAPOKUTANA:
Huwa tunakutana saa 12 jioni na kutoa ripoti ya tulivyovifanya tangu mkutano wa mwisho, kuhusu misaada tuliyotoa, wanachama wanaoumwa, na nani wa kwenda kumtembelea au kama kuna mwananchama mpya wa kumuapisha, kama hayupo tunajadiliana kuhusu mambo tofauti yanayotuhusu isipokua siasa na dini, tunakula pamoja na kila mtu anaondoka.
MNAKUTANA MARA NGAPI?
Inategemea kama tawi la Uingereza tulikua tunakutana mara mbili kwa mwaka, la huku ambalo ndiko nilikoapishwa tulikua tunakutana mara 11 kwa mwaka lakini siku hizi ni mara kumi, wengine wanakutana mara 5, inategemea na kazi za kufanya, mfano labda wanachama wa kuapisha ni wengi.
Ibada inafanyikaje?

.
Ibada inaanza wakati vikao vinaanza, inahusisha mara nyingi kitu ambacho kinafanana na ibada kanisani, mara nyingi inahusika kumuweka mwananchama mpya kwenye mstari na mtazamo mmoja na aliowakuta na kwenye ibada huwezi kuvaa unavyotaka, lazima uvar suti na tai isipokua nchi kama India ambao hawavai tai.
Ukiwa mwanachama unapewa maswali ambayo ukiyajibu vizuri kwa muda wako unaweza kupandishwa cheo na inachukua muda kufikia degree ya tatu, tukiwa kwenye vikao mwenyekiti anaitwa Master na anao wasaidizi wawili, kwenye ibada mwenyekiti anakaa mashariki, msaidizi mmoja ana kaa mbele yake akimtizama na wa pili anakua anasaidia kwa shughuli nzima inayoendelea.
Kuna mwingine ambae ndio muongozaji wa sala na wakati tukisali, Mungu tunamuita Fundi mkuu aliyeumba sayari zote hiyo inahakikisha kwamba uwe Musilamu au mkristo tunakwenda sambamba.
ISHARA ZINAZOTUMIKA FREEMASONS

.

.
Kuna alama ya Compass inayotumika kuonyesha mwelekeo kwa mishale yake, kuna ruler na pembe nne ambavyo ni vitu vinavyotumika kwenye ujenzi ila vinaweza kutumika kufundisha kuhusu maisha, na ndio vinatumika hivyo wala sio kuhusu kitu kingine.
Tukifanya ibada zetu au kumkubali mtu kuingia freemasons lazima avae pajama au mavazi yanayotumika kulalia usiku, na haruhusiwi kuwa na pesa mfukoni, kuvaa saa au cheni ishara ya kuwa yeye ni masikini kama alivyozaliwa.
Uchawi, kuabudu shetani na mambo kama hayo watu wanayosema kwamba freemasons ndio inajihusisha na hivyo vitu ikiwemo kutoa uhai ndugu, ni waongo, hawana ujuzi wa kutosha, nakumbuka pia rais Moi aliunda kamati maalum kuchunguza uchawi na waabudu shetani na tuliitwa nikaenda kuwaeleza kwa muda wa karibu saa na nusu kuhusu freemasons, ingawa hawakuja kutupa ripoti kamili waliyopeleka kwa rais moi, walituambia kwamba wamekubali maelezo yetu na ingekua bora kama tungekua tunaeleza zaidi watu wajue na tusiwe wasiri.
FAIDA ZA KUWA FREEMASONS:
Hakuna faida za kupata pesa kama wengi wanavyoambiwa kwamba ukiwa freemasons unapewa mihela, faida za kuwa freemasons ni pamoja na kuongeza idadi ya marafiki na kuongeza knowledge (ufahamu)
Faida nyingine labda ni kama ukitoa tenda kama unaanzisha kiwanda na umetoa tenda ya kazi, ukiona mmoja wa freemasons yuko kwenye list ya walioomba tenda utampa kipaumbele kwa sababu unamfahamu na ni kama ndugu.
Hakuna utoaji wa kafara kama inavyosemekana na pia hakuna uhusiano kati ya freemasons na agano la kale.
MAMA MZAZI WA KANUMBA KUHUSU KANUMBA KUWA FREEMASON:
Mama mzazi wa Marehemu mwigizaji Steven Kanumba alisema siku kadhaa baada ya Kanumba kufariki kuna kijana alikuja nyumbani na kumwambia mama kwamba yeye (kijana) ndio alimsaidia Kanumba kujiunga na Freemasons miaka kadhaa iliyopita hivyo alikwenda nyumbaniili wazungumze na mama, mama Kanumba alimfukuza hapohapo na kumwambia mwanae hajawahi kuwa freemason na akamwambia akirudi tena atamwitia polisi.

.
MISTARI YA JAY Z KWENYE WIMBO WA FREEMASON WA RICK ROSS.
Watu wananisingizia mambo ya kishetani, uvumi unaenea sehemu zote,  nipishe huyu ni Mungu anafanya mambo yake, najua mnaniogopa Sijui wa kumwamini sala ya maria inafanya kazi.
Mnanisingizia vitu vingi vya kishetani lakini bado mnapandisha sauti kubwa mkisikiliza muziki wangu, hizo stori zote hazina msingi, mniache Mungu anafanya kazi yake.
Mungu ndio injinia hapa, asiefanya fanya dhambi atupe jiwe la kwanza angalieni sura zenu kwenye vioo mnavyoonekana, Sio kwamba mimi ni Freemason, nilipitia tu mambo mengi sana na Mungu anisamehe manake nisingefika nilipo bila kufanya dhambi, nimeosha sura yangu kwa maji matakatifu hii rozari yenye shanga, tena shanga za diamond ni uthibitisho kwamba Mungu alinisamehe.
Mi ni mkali, acha kutazama kwenye sahani yangu… sema tu unatamani nilichonacho.
RIPOTI YA CNN AUGUST 2010 KUHUSU FREEMASON:
Baadhi ya maseneta wa majimbo kadhaa ya Marekani walikiri kuwa ni wanachama wa Freemason ambapo ilifahamika kwamba Marais 12 waliowahi kuiongoza Marekani walikua wanachama wa Freemason ambapo pia watu 9 kati ya waliosaini hati ya uhuru wa Marekani walikua freemason akiwemo George Washington
story zote kutoka 
                                  www.millardayo.com
Read more ...

MAZISHI YA ASKOFU BALLINA YALIKUWA HIVI..JK ASHIRIKI MAZISHI

Nov 10, 2012

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Mhashamu Baba Askofu Aloysius Balina wa Jimbo Katoliki la Shinyanga baada ya kuwasili kwenye Kanisa la Mama wa Huruma katika Parokia ya Ngokolo mjini Shinyanga kushiriki mazishi ya Askofu huyo leo, Jumamosi, Novemba 10, 2012.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Mhashamu Baba Askofu Aloysious Balina wa Jimbo Katoliki la Shinyanga wakati wa mazishi wa Askofu huyo kwenye Kanisa la Mama wa Huruma, Ngokolo, mjini Shinyanga leo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la Askofu Aloysius Balina wakati wa mazishi ya Askofu huyo leo kwenye Kanisa la Mama wa Huruma, mjini Shinyanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua kwenye kaburi la Askofu Aloysius Balina wa Jimbo Katoliki la Shinyanga wakati wa mazishi ya Askofu huyo kwenye Kanisa la Mama wa Huruma, Ngokolo, Shinyanga leo. Picha na mdau Fred Maro-Ikulu
Read more ...

ISIKILIZE RIPOTI NYINGINE YA MWANDISHI AKIWA TEMEKE HOSP AMBAKO INAAMINIKA KUNA WATU WAMEGANDANA WAKIFANYA MAPENZI, POLISI WAMEANZA KUTUMIA MABOMU.

Nov 8, 2012

Hii ndio ripoti ya mwandishi Salehe Masoud wa Clouds tv kuhusu taarifa ya miili ya watu kung’ang’ania wakiwa gest house baada ya kufumaniwa, yani ni mwanaume aliekutwa na mke wa mtu ambapo Masoud ambae yuko kwenye hospitali ya Temeke ambako watu hao wanadaiwa kupelekwa ameripoti kwamba baadhi ya mashuhuda wanasema watu hao wamefikishwa hospitali wakiwa wamegandana na waliteremshwa kwenye gari wakiwa hivyohivyo ingawa uongozi wa hospitali umekanusha na tayari umeshatoa tamko kwa mamia ya watu waliokusanyika kwamba sio la kweli, hakuna ukweli wa hizo taarifa.
Baada ya watu kuzidi kuwa wengi na kila mmoja akitaka kuona hao waliogandana, polisi wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya mamia ya watu waliofika kushuhudia ambapo inasemekana wawili hao wamehifadhiwa nyuma ya Mochwari.
Hao watu inasemekana walikutwa wakifanya mapenzi kwenye nyumba moja ya wageni huko Temeke 
CHANZO NI MILLARD AYO.COM
Read more ...

JK: Azindua Ujenzi Wa Bomba La Gesi Asilia Kutoka Mtwara-Dar es salaam

Nov 8, 2012

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na ujumbe wa kampuni inayojenga bomba la gesi asilia kutoka Mtwata hadi Dar es salaam, Benki ya Exim ya China na viongozi waandamizi wa serikali alipowakaribisha Ikulu kwa mazungumzo baada ya uzinduzi rasmi wa ujenzi wa bomba hilo maeneo ya Kinyerezi jijini Dar es salaam.

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali na viongozi wengine wakimsikiliza  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo miundombinu ya  bomba la gesi asilia toka Mtwara hadi Dar es salaam leo Novemba 8, 2012 maeneno ya Kinyerezi njijini Dar es salaam. Nyuma yake ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua rasmi ujenzi wa bomba la gesi asilia toka Mtwara hadi Dar es salaam leo Novemba 8, 2012 maeneno ya Kinyerezi njijini Dar es salaam. Nyuma yake ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali.
Read more ...

MWONEKANO WA IRINGA LEO HII

Nov 8, 2012
Read more ...

Swahili Fashion Week T-shirt Designing Competition 2012

Nov 8, 2012
Read more ...

AJITEKETEZA NA MOTO KWA KUCHOSHWA NA MAISHA...

Nov 8, 2012
Wanaharakati nchini China wanasema kuwa vijana watatu watawa wa Tibet pamoja na mama mmoja walijiteketeza mkesha wa kongamano la chama cha tawala cha kikomunisti nchini China.
Shrika la Free Tibet linasema kuwa mmoja wa watawa hao alifariki katika kile inachosema ni idadi kubwa ya watu kujiteketeza kama njia ya kuonyesha kukerwa na utawala wa china.
Matukio ya hivi karibuni ya watu kujiteketeza moto katika maeneo ya china yaliyo na watu wa Tibet yamefikisha idadi ya watu hao wanaojiteketeza kuwa zaidi ya watu sitini tangu mwaka jana.
Wengi wao wamefariki. Na huenda kuna umuhimu katika wakati ambapo visa hivi vimetokea.
Kuimarishwa kwa usalama kote China kwa kongamano la chama tawala cha kikomyunisti nchini, hakujazuia malalamiko ya raia wa Tibet dhidi ya utawala wa China. Badala yake yameongezeka.
Wanaharakati wanasema idadi ya watu kujiteketeza kwa muda wa siku moja, hii leo, haikutarajiwa.

Read more ...