Pages

JINSI RPC WA MWANZA ALIVYO UWAWA

Oct 13, 2012

Marehemu Kamanda Liberetus Barlow (kulia) enzi za uhai wake akizungumza na vyombo vya habari jijini Mwanza. 

Ilikuwa ni majira ya saa  8 usiku huu napata taarifa ambazo hatimaye zinathibitishwa kutoka kwa waugwana kuwa  Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow amefariki dunia kwa kupigwa risasi usiku huu maeneo ya hotel Tai 5, Kitangili jijini Mwanza .


Marehemu Kamanda Liberatus Barlow alifariki kabla ya kufikishwa katika hospitali ya Bugando ambapo inadaiwa alivamiwa na watu takribani wanne waliokuwa wamevalia mavazi ya polisi jamii ndipo aliposimamishwa na baada ya kusimama watu hao walimmiminia risasi kufuani na kusababisha  kifo chake

Imeelezwa kwamba Marehemu Kamanda Liberatus Barlow alikuwa akitoka kwenye harusi na alikuwa na mtu mmoja
  kwenye gari aliyekuwa akimsindikiza mtu huyo ambaye ni mwanamke yeye hakudhurika na chochote katika tukio hilo.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.Eng. Evarist Ndikilo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama mkoani Mwanza ameshathibitisha kutokea kwa tukio hilo la kifo cha kamanda Liberatus Barlow.

Aidha taarifa zaidi kuhusu tukio hilo tutaendelea kuwajuza kwa kadri tutakavyozipata hapa
Read more ...

HUYU NDO 0.5 .KUTOKA KWA MICHAEL GAGI,HONGERA SANA BROOO

Oct 13, 2012
KWA WALE WANAOJUA KUWAJIBIKA HUYU NDO MWANA (0.5) WA MICHAEL GAGI AMBAYE KAZALIWA JUZI HUKO NCHI SWIZZ NA HII NDO PICHA YA CHALII HAPO CHINI


                            Photo: lil Robin just after birth..thank you god for this blessing.
Read more ...

TAREHE ZA KUFANYA MITIHANI YA FORM 4 NA 6 ZABADILISHWA

Sep 28, 2012
Serikali imetoa tamko juwa tarehe za kufanya mitihani ya kidato cha nne na sita sasa itaongezwa muda ilikuongeza muda wa wasahihishaji kusahihisha kwa ufasaha na umakini zaidi
Read more ...

ZITTO:NARUDIA TENA SIGOMBEI URAISI 2015

Sep 28, 2012

Na hiki ndicho alichokiandika zito kabwe katika fanpage yake kuhusu kugombea ama kutogombea uraisi 2015
Read more ...

Dr.PAUL SWAKALA MWENYEKITI WA MADAKTARI WALIOATHIRIKA NA MGOMO AMWANGUKIA JAKAYA

Sep 17, 2012

MADAKTARI INTERN WAMWANGUKIA JK KUFUATIA KUSHIRIKI KWAO KATIKA MGOMO WA MADAKTARI.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari walioathirika na mgomo Dr. Paul Swakala (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Na. Datus Boniface
Wanaodaiwa kuwa ni Madaktari wanaofanyakazi chini ya usimamizi wa madakatari bingwa (Intern Doctors), wamemwangukia Rais Jakaya Kikwete huku wakimwomba radhi kwa ushiriki wao katika mgomo wa madaktari uliosababisha maafa kwa baadhi ya wagonjwa.
Kwa upande mwingine wamekijua juu Chama Cha Madaktari Tanzania (MAT) kuwa kimewasaliti katika kutatua matatizo yao kwa sasa.
Hata hivyo, wameomba radhi kwa Wananchi walioathirika na mgomo huo kwa usumbufu uliyosababishwa na mgomo huo.
Hadi sasa Madaktari 364, wako mtaani baada ya kusimamishwa kazi kutokana na kushiriki katika mgomo ambao umeisha hivi karibuni, baada ya kushawishiwa na wenzao wakiwemo viongozi wa MAT.
Akitoa tamko kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari hao, Paul Swakala alisema “Tulikaa na MAT kuzun gumza juu ya kutusaidia kutatua kero zetu lakini wameshindwa kutusikiliza na baadala yake tumeamua kufika hapa na kutoa kilio chetu”
Kutokana na kusalitiwa huko, alitoa onyo kwa Madaktari wengine kuwa wanaweza kupima kama wataendelea kujiunga na MAT au la.
Alienda mbali zaidi na kusema, hawako tayari tena kushiriki kwa namna yoyote katika migomo inayoweka rehani maisha ya Watanzania.
Alisema, kwa hakika wanajutia kosa lao la kushiriki mgomo na wako tayari kurejea kazini ili kuendelea na kazi ya kuwahudumia Wananchi kwa moyo mweupe.
Read more ...

Hawa ndio waliomwua mwandishi wa Channel Ten huko Iringa

Sep 2, 2012


JamiiForums | The Home of Great Thinkers - JamiiForums.comNaomba mniruhusu niweke picha zenye sura za walioshiriki kitendo hiki cha kihuni ambacho ni uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu kama kamera yangu ilivyokinasa.


Nina picha ambazo zimechukuliwa zinazoonyesha walioshiriki na jinsi walivyoshiriki. Hata RPC alikuwepo eneo la tukio.

Mods, naomba msiunganishe thread yangu plz.

Picha nyingine nimezituma kwa watetezi wa haki za binadamu na video nimeziweka YouTube (sitatoa link kwa sasa).

Wanahabari, ni wakati wa kuonyesha umoja wetu dhidi ya udhalimu huu.

-----


Huyu askari alimwelekezea mtutu tumboni na kumsambaratisha marehemu. Ni wazi watu wa Iringa wanamfahamu askari huyu.



Pembeni ni shangingi la RPC, askari huyu naye kashuhudia kitendo hiki cha kikatili. Wanahabari tushirikiane kupiga kelele. Hapa walikuwa wamemaliza unyama wao wakimwondoa mwenzao aliyeumia eneo la tukio

Maiti ilisambaratishwa kabisa utumbo, si uungwana kuweka picha kama hizo hapa.


Kama ni kesi, askari huyu anaweza kuhojiwa. Nimekata picha kusitiri mwili wa marehemu.

Marehemu kafa akipigania haki za wanahabari, ni wakati wa wanahabari kushirikiana vinginevyo wanasiasa wataendelea kutumia vibaya vyombo vya dola dhidi yetu.
Read more ...
Aug 24, 2012
Read more ...

CUHAS RESULT 2011/2012

Aug 21, 2012


















Read more ...

AJALI YATOKEA\MWANZA YAHUSISHA KARANDINGA LA POLISI MAHABUSU WAHAHA

Aug 16, 2012










Read more ...