Pages

Hawa ndio waliomwua mwandishi wa Channel Ten huko Iringa

Sep 2, 2012


JamiiForums | The Home of Great Thinkers - JamiiForums.comNaomba mniruhusu niweke picha zenye sura za walioshiriki kitendo hiki cha kihuni ambacho ni uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu kama kamera yangu ilivyokinasa.


Nina picha ambazo zimechukuliwa zinazoonyesha walioshiriki na jinsi walivyoshiriki. Hata RPC alikuwepo eneo la tukio.

Mods, naomba msiunganishe thread yangu plz.

Picha nyingine nimezituma kwa watetezi wa haki za binadamu na video nimeziweka YouTube (sitatoa link kwa sasa).

Wanahabari, ni wakati wa kuonyesha umoja wetu dhidi ya udhalimu huu.

-----


Huyu askari alimwelekezea mtutu tumboni na kumsambaratisha marehemu. Ni wazi watu wa Iringa wanamfahamu askari huyu.



Pembeni ni shangingi la RPC, askari huyu naye kashuhudia kitendo hiki cha kikatili. Wanahabari tushirikiane kupiga kelele. Hapa walikuwa wamemaliza unyama wao wakimwondoa mwenzao aliyeumia eneo la tukio

Maiti ilisambaratishwa kabisa utumbo, si uungwana kuweka picha kama hizo hapa.


Kama ni kesi, askari huyu anaweza kuhojiwa. Nimekata picha kusitiri mwili wa marehemu.

Marehemu kafa akipigania haki za wanahabari, ni wakati wa wanahabari kushirikiana vinginevyo wanasiasa wataendelea kutumia vibaya vyombo vya dola dhidi yetu.