Pages

ORODHA YA MADAKTARI 394 WANAOTAKIWA KURUDISHA HATI ZA USAJILI WA MUDA KABLA YA TAREHE 17

Jul 11, 2012




Nilianzia Image, Nikakutana Na Kizazi Cha Nne Cha Daktari wa Mkwawa






Maliga: Kizazi cha nne cha Daktari wa Chifu Mkwawa

Na Daniel Mbega

KWA Jangwa Maliga (38), mkazi wa Kijiji cha Image katika Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, kutibu majeraha na mifupa iliyovunjika kwa ajali umekuwa utamaduni wake wa kila siku.
Kwake kuchelewa kulala ama kuamshwa usiku wa manane ili awahudumie majeruhi hao siyo karaha, kwani amekuwa akiifanya kwa miaka 13 sasa mfululizo.
Maliga, ambaye hakuwahi kuliona darasa la tiba za kisasa, amekuwa mkombozi na kimbilio la wahanga wengi wa ajali, ambao ama wamepata majeraha makubwa yaliyoshindikana kupona au kuvunjika mifupa ambayo imeshindwa kuungwa katika hospitali kubwa.
Hana x-ray, hana utaalamu wa kisasa, lakini anasema anaweza kumtazama mgonjwa na kujua tatizo gani linalomsumbua na tiba ipi ambayo itamsaidia mpaka apone.
“Sijasomea tiba hii, lakini hata nikikaa na madaktari bingwa nitawaeleza kwa Kiswahili tatizo linalomsumbua mgonjwa, maelezo ambayo hayawezi kuwa tofauti na watakayoyatoa wao kwa lugha ya kitaalam.
“Naangalia aina ya majeraha yenyewe, kama ni mfupa wa fibula, tibia, femur, radius, ulna au humerus umevunjikaje. Wachache, ambao matatizo yao yanakuwa makubwa, huwa nawaeleza moja kwa moja tu kwamba hakuna jinsi inabidi wakakatwe viungo vyao,” anasema.


Reactions::

Mjumbe, "Nilikuwa Kwenye Kaburi La Mtwa Munyigumba"

Eneo hili lina makaburi tisa ya ukoo wa Muyinga na linaloonekana hapo ndilo la Chifu Munyigumba Kilonge Mudegella Mwamuyinga, baba yake Mtwa Mkwawa. Kabla ya kuingia ni lazima usali.


Halafu hili ni kaburi la Mtwa Msengele Kilekamagana Munyigumba Mwamuyinga, mdogo wake Mtwa Mkwawa kwa Mama Sengimba mdogo.






Kutoka Mwindaji Wa Ethiopia Hadi Chifu Wa Wahehe

Na Daniel Mbega
MAANDIKO kadhaa yamekuwepo kuhusiana na historia ya Wahehe na hasa ukoo wa Mtwa Mkwavinyika Munyigumba Mwamuyinga, maarufu kama Mkwawa, lakini yote hayo hayakunizuia kuisaka historia hiyo.
‘Jicho halishibi kuona na Sikio halikinai kusikia!’ hivyo nikaamua kufunga safari hadi Lungemba, yaliko makaburi ya Mtwa Munyigumba na ndugu wengine wa ukoo huo, yapata kilometa 62 kutoka Iringa Mjini.
Wapo walioandika kwamba chimbuko la Mtwa Mkwawa ni Ungazija, lakini simulizi ninazokutana nazo hapa ni tofauti, maana zinatoka katika vinywa vya wanaukoo wa Muyinga, ambao nao wameipata ama kurithishwa kutoka kizazi na kizazi kutokana na simulizi za mababu zao.
Wale waliopata kuandika kwamba asili ya akina Mkwawa ni Ungazija wanaeleza kuwa mtawala wa Ngazija aliyeitwa Yusuf Hassan ambaye alikuwa Mwarabu, alizaa watoto wawili wa kiume, Hassan ‘Mbunsungulu’ na Ahmad. Wanasema kwamba Mufwimi alikuwa mmoja wa watoto watatu wa Mbunsungulu aliozaa na mwanamke wa Kikaguru. Ndugu zake wengine walikuwa Ngulusavangi na Ngwila, kwa maelezo yaliyo kwenye baadhi ya maandishi ambayo inatoweka kutokana na Watanzania kukosa utamaduni wa kutembea, kujifunza na kudadisi.


Reactions::

Aliyefunga Milango Ya kanisa Afikishwa Mahakamani

Lawrance Mtatifiko (30)
Pichani ni Lawarance Mtatifikolo (30) Mkazi wa Image wilayani Kilolo, mkoani Iringa.

Hii leo Mtatifikolo amefikishwa katika Mahakama ya Hakim Mkazi wa Wilaya ya Mjini Iringa akituhumiwa kufanya fujo kinyume cha sheria ya makosa ya jinai kifungu namba 170 cha Kanuni ya Adhabu.


Katika mahakama hiyo ilielezwa kwamba mnamo Julai 8, mwaka huu , Mtatifiko akiwa na wenzake wanne (hawajakamatwa) walifanya kitendo kisichoruhusishwa kisheria kwa kufunga mlango wa kanisa na kusababisha usumbufu kwa waumini.


Walifunga lango kuu la kuingilia Kanisa Kuu la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Iringa wakilenga kufikisha ujumbe kwa Askofu wa Dayosisi hiyo kwamba hawataki aendelee kuwa kiongozi wao kwasababu anatuhuma nyingi za kimaadili na uongozi.


Kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Festo Lwila itatajwa tena mahakamani hapo Julai 24 wakati uchunguzi wake ukiendelea.

Chanzo:http://www.frankleonard.blogspot.com/ 
Reactions::

Nyanya Za Nyanda Za Juu Kusini

                                                          Ni Mbigili leo asubuhi
Reactions::

Taarifa Kwa Umma

Baraza la Madaktari Tanganyika limepokea malalamiko kutoka kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwamba, baadhi ya Madaktari waliopata usajili wa muda ili kuwawezesha kufanya mafunzo kwa vitendo (Internship), waligoma kutoa huduma kwa wagonjwa kati ya tarehe 23 na 29 mwezi Juni 2012. Madaktari hao walipangiwa kutoa huduma kwa wagonjwa katika hospitali za Muhimbili, K.C.M.C, Rufaa Mbeya, Bugando, Amana, Temeke,St. Francis- Ifakara, Mwananyamala, Sekou Toure, Haydom na Dodoma. Kufuatia mgomo huo, uongozi wa hospitali husika uliwaandikia barua iliyomtaka kila daktari aliyeshiriki kwenye mgomo kuripoti kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii aliwasilisha malalamiko kwenye Baraza la Madaktari Tanganyika kwamba, Madaktari waliogoma walikataa kutoa huduma za kitaalamu, ikiwa ni wajibu wao, na kwamba kitendo hicho kilihatarisha maisha ya wagonjwa katika hospitali husika na pia ni kinyume na maadili ya taaluma ya udaktari.
Kufuatia malalamiko hayo, Msajili wa Baraza la Madaktari Tanganyika, alimwandikia kila daktari aliyelalamikiwa Taarifa ya Kusudio la Kufanya Uchunguzi (Preliminary Examination) dhidi yake, juu ya malalamiko yaliyowasilishwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Baraza la Madaktari Tanganyika limebaini kuwa, kwa mujibu wa kifungu cha 15(2) cha Sheria ya Madaktari, Sura ya 152, Madaktari waliokuwa kwenye mgomo na ambao kwa sasa wameondolewa katika hospitali walizokuwa wakifanya mafunzo kwa vitendo, wamepoteza sifa za kupata usajili wa muda (Provisional Registration).
Kwa kuzingatia masharti ya Sheria kuhusu kupata usajili wa muda, Baraza la Madaktari Tanganyika limeridhika kwamba madaktari wote ambao majina yao yameorodheshwa katika Taarifa hii, wamepoteza sifa na kwa sababu hiyo, usajili wao umesitishwa kuanzia tarehe 11 Julai, 2012. Madaktari wote wanaohusika wanatakiwa kurejesha hati za usajili wa muda kwenye Ofisi ya Msajili wa Madaktari kabla ya tarehe 17 Julai, 2012.
S/NO JINA REG. NO.
MUHIMBILI
1 Dr. Dickson N. Sahini 363
2 Dr. Elphas G. Mrita 4902
3 Dr. Anastazia E. Komba 4973
4 Dr. Anna Lwemunge 5086
5 Dr. Mariam Amour 4974
6 Dr. Jackline Matowo 5372
7 Dr. Baya Kisiwa 4970
8 Dr. Lilian B. Komba 4871
9 Dr. Pavina Kazaura 5089
10 Dr. Herifrid Kimambo 5377
11 Dr. Kokuhabwa Mukurasi 5095
12 Dr. Evance Godfrey 5059
13 Dr. Emmanuel K. Luchagula 4874
14 Dr. Florence Mtei 5094
15 Dr. Alfonse Moyo 5097
16 Dr. Alkwinus Kabwogi 4889
17 Dr. Rebeca A. Kalikawe 4962
18 Dr. Aida O. Salum 5368
19 Dr. Aron Aron 5345
20 Dr. Sabza Masoud 4956
21 Dr. Ramadhani Kabota 4861
22 Dr. Norbert Benjamin
23 Dr. Victroia Paul 5084
24 Dr. Godfery Chuwa 5097
25 Dr. Goodluck Mrosso 356
26 Dr. Luciana Albert 375
27 Dr. Gendagenda Mkombozi 372
28 Dr. Lucas Mselle 4919
29 Dr. Edna Mwakyembe 365
30 Dr. Haruna Rashid 552
31 Dr. Sara Lumumanji 5006
32 Dr. Paul Zacharia 4858
33 Dr. Abza Saka 4981
34 Dr. Baraka Maige 5361
35 Dr. Wilhelmuss I. Mauka 4979
36 Dr. Deogratius Mally 4960
37 Dr. Ahmad Fadhil Kombo 4868
38 Dr. Iman Bawazir 4799
39 Dr. Frank Kagoro 5046
40 Dr. Baraka Yessaya 5058
41 Dr. Naki Kiroga 5347
42 Dr. Bakari A. Gillal 4959
43 Dr. Linda August 5343
44 Dr. Shah Alkash 342
45 Dr. Chihoma Mhaki 358
46 Dr. Gloria Leo 337
47 Dr. Mohamed M. Ally
48 Dr. Ahmed Kombo 5389
49 Dr. Steven Nandi 5030
50 Dr. Moses J. Karashani 5040
51 Dr. Innocent Mpuya 5371
52 Dr. Octar Javett 5048
53 Dr. Juma Mbugi 5018
54 Dr. Neema Nalitolela 4966
55 Dr. John Nkenda 4963
56 Dr. Ngutuni Jackson 5005
57 Dr. Malava F. Raphael 4982
58 Dr. Masawa Nyamunjeku 5000
59 Dr. Shubi Matovelo 4976
60 Dr. Winnie Temu 4965
61 Dr. Sarah Shiraz 5024
62 Dr. Hafsa Hawesi 5369
63 Dr. Anthony Kingilo 5330
64 Dr. Elikanaar Urio 5336
65 Dr. Zainabu Mkinde 5367
66 Dr. Shau Hamdan 5071
67 Dr. Cristogone Justine 4968
68 Dr. Conrade Ngonyani 4865
69 Dr. Deo B. Mwanakulya 4873
70 Dr. Lucy Laurent 4872
71 Dr. Khadija Juma 4969
72 Dr. Valentino Koja 5338
73 Dr. Aloyce F. Lengasia 4977
74 Dr. Zyleen Kasamali 4888
75 Dr. Mwajuma Mustapha 4971
76 Dr. Mariam Hamad 4859
77 Dr. Francis Mwimazi 4967
78 Dr. Hassan Barnabas 5364
79 Dr. Grace Mmasi 5045
80 Dr. Mohamed Mzige 4860
81 Dr. Elias Paschal 4961
82 Dr. Farida Mtonga 5002
83 Dr. Gabriel Mbwete 5337
84 Dr. Magdalena Dennis 4910
85 Dr. Ahmed Ahmed 4798
86 Dr. Joseph Shaban 5408
87 Dr. Prudence Premier 5409
88 Dr. Malaja Ng’wigulu 5019
89 Dr. Biswaro Malima 4975
90 Dr. Isaac Mlay 5007
91 Dr. Raymond Samwel 5017
92 Dr. Michael Kiremeji 5376
93 Dr. Viviene Mlawi 5000
94 Dr. John Jananga 5380
95 Dr. Said Ibrahim 5020
96 Dr. Alphonce Simbila 5047
97 Dr. Catherine Mlowe 5044
98 Dr. Barbara Mwaipola 4964
99 Dr. Joel J. James 5129
100 Dr. Bright Sangiwa 5053
101 Dr. Evance Alexander 4887
102 Dr. Martha Nkya 5335
103 Dr. Camilla Kinemo 5406
KCMC
1 Dr. Malkiadi P. Mbota 5208
2 Dr. Wilfred j. Meza 4900
3 Dr. Shomari O. Masenga 4983
4 Dr. Jamila J. Shemweta 5009
5 Dr. Godbless E. Massawe 5026
6 Dr. Rahel T. Mwavika 4879
7 Dr. Eliakimu P. Kapyolo 5032
8 Dr. Godfrey N. Barabona 5051
9 Dr. Aristides K. Raphael 4984
11 Dr. Emmanuel M. Manyonyi 5077
12 Dr. Herielly O. Msuya 5118
14 Dr. Noel J. Makundi 5142
15 Dr. Maxigama Y. Ndosi 5107
16 Dr. Patrick A. Karua 5137
17 Dr. George C. Mgalega 5155
18 Dr. Juma Adinan Juma 5151
19 Dr. Kenneth J. Mlay 5158
20 Dr. Njengo B. Mbanga 5145
21 Dr. Yesige A. Mutajwaa 5171
22 Dr. Mbazi D. Shemwetta 5139
23 Dr. Mwanaidi S. Mkwizu 5141
24 Dr. Peter E. Ng’wamkai 5109
25 Dr. Tumaini D. Ndibwire 5131
26 Dr. Lucas D. Ngamtwa 5161
27 Dr. Goodluck J. Ulomi 5143
28 Dr. Juma M. Nahonyo 5150
29 Dr. Emmanuel S. Masatu 4899
30 Dr. Angela E. Pallangyo 5110
31 Dr. Casto E. Mlay 5182
32 Dr. Birjna A. Hirani 5152
33 Dr. Anette J. Kessy 5178
34 Dr. Ester P. Lazaro 5190
35 Dr. Mugisha N. Nkoronko 5115
36 Dr. Sofia A. Ottaru 5146
37 Dr. Raya Y. Mussa 5132
38 Dr. Regina Y. Msanga 5148
39 Dr. Delfina R. Msanga 5147
40 Dr. Allen G. Kangarawe 5138
41 Dr. Sia C. Kiwia 5198
42 Dr. Peter E. Kipiki 5144
43 Dr. Avelina R. Kimaryo 5177
44 Dr. Peter F. Mwandiga 5075
45 Dr. Daimon B. Mwasamila, 5210
46 Dr. Emmanuel D. Lema 5185
47 Dr. Karungi J. Karoma 5130
48 Dr. Fortunatus m. Ibreck 5199
49 Dr. Sadiq S. Dawood 5121
50 Dr. Witness M. Mchwampaka 5186
51 Dr. Azza A. Naif 5111
52 Dr. Malkiadi P. Mbota 5208
53 Dr. Mariam T. Johari 5013
54 Dr. Daniel M. Chochole 5162
55 Dr. Oliver T. Masoy 5197
56 Dr. Gerald C. Robi 4927
57 Dr. Erasto S. Odindo 5229
58 Dr. Kasirye J. Collins 5243
59 Dr. George D. Dilunga 5239
60 Dr. Emmanuel S. Maro 5240
61 Dr. Irene R. Haule 5242
62 Dr. Godfrey A. Kisuma 5246
63 Dr. Frank M. Sudai 5231
64 Dr. Annette A. Marandu 5196
65 Dr. Joseph E. Soka
66 Dr. Hans Mpimilwa
MBEYA REFFERAL
1 Dr. Msafiri Lewanga 5069
2 Dr. Regan Rajuu 5224
3 Dr. Alex Mwakyandile 5311
4 Dr. Osmundi Dyegula 4954
5 Dr. Ireene Kato 5012
6 Dr. Lutaragula Masili 5067
7 Dr. Nindwa Maduhu 5209
8 Dr. Noel Dominic Swai 4952
9 Dr. Masanja Erasto Kasoga 5100
10 Dr. Mwanahamisi Japhary 4768
11 Dr. Nuru Mwambola 5100
12 Dr. Jane Maganga 5174
13 Dr. Karim Mohamed 4767
14 Dr. Joyce T. Massaro 5195
15 Dr. Kanjanja A. Amas 5213
16 Dr. Joseph Msemwa 5116
17 Dr. Jonas Lulandara 4851
18 Dr. Kulwa Itambula Joseph 5173
19 Dr. Josephat Mapunda 4890
20 Dr. Joseph Antony Legembo 5392
21 Dr. Saili Mbukwa 5381
22 Dr. Samwel Cherubini Mkumbe 5395
23 Dr. Serephine J. Mrosso 4950
24 Dr. Agapiti Hipoliti Chuwa 4903
25 Dr. Deusdedit Kalaso 4986
26 Dr. Ano A. Maseta 5437
27 Dr. Alinanuswe Kasililika 4953
28 Dr. Anicetus Rwebangira 5123
29 Dr. David Hamisi Mvunta 5172
30 Dr. Ally Mbwana Mhando 5327
31 Dr. Aminiel E. Ngomuo 5068
32 Dr. Emmanuel Obasy Mwakibinga 5010
33 Dr. Erica A. Balama 4687
34 Dr. Fred Frank 5281
35 Dr. Emmanuel Bahemana 5070
36 Dr. Elisonguo E. Kimambo 5282
37 Dr. Furaha Mwakafwila 5108
38 Dr. Emmanuel J. Itambu 4685
39 Dr. Beniedy A. Chitama 5205
40 Dr. Gwakisa John 5023
41 Dr. Charrido Chalo
42 Dr. Winfrida Halinga 5435
43 Dr. Wistone I Ngaiza 5441
44 Dr. Honsia E. Moshi 5288
45 Dr. Lewanga Msafiri 5069
46 Dr. Peter Frank Saria 5202
47 Dr. Ngwilo Mwakyusa 5317
48 Dr. Adison Mpyambala 4955
49 Dr. Ilekizemba G. Khalfanis 4420
50 Dr. Angela T. Mlole 5013
51 Dr. Rajab Mramba 5245
52 Dr. Lusajo Raphael Mwakajoka 5441
53 Dr. Musa Gabriel 377
54 Dr. Bogias Fidelis Mwamgunda 378
55 Dr. Raymond Mwalonde 5230
BUGANDO MEDICAL CENTRE
1 Dr. Lukansola Makubula 4863
2 Dr. Amos Stanley 4876
3 Dr. George B. Rweyemera 4913
4 Dr. Peter J. Kitenyi 4925
5 Dr. Florian Mutasingwa 4918
6 Dr. Mwanaisha Seugendo 4905
7 Dr. Derick David 4884
8 Dr. Baraka R. Mkinze 4883
9 Dr. Emanuel Alphonce 4911
10 Dr. Paulina M. Manyiri 4891
11 Dr. Wilhelmina J. Mbwana 4924
12 Dr. Jacqueline B. Iraba 4941
13 Dr. Dismas Stephen 4934
14 Dr. Deo Donald Kisaka 4989
14 Dr. James J. Gesimba 5008
16 Dr. Athuman M. Mambo 4988
17 Dr. Hadija M. Bushahu 5015
18 Dr. Cosmas H. Mbulwa 4942
19 Dr. Raymond M. Wilson 5041
20 Dr. Elizabeth N. Kwiyolecha 5065
21 Dr. Flavian Simula 5165
22 Dr. George Adriano 5035
23 Dr. Enock J. Simeon 5079
24 Dr. Devotha J. Mbabala 5153
25 Dr. Hellen Munaku 5135
26 Dr. Kilemo J. Mzobora 5192
27 Dr. Shija F. Mahenda 5164
28 Dr. Frank Mayaya 5136
29 Dr. John N. Akwitende 5223
30 Dr. Dorice L. Shangali 5193
31 Dr. Albert J. M. Mnyanzilu 364
32 Dr. Amina J. Yusuph 5102
33 Dr. Immaculate Henry 5188
34 Dr. Deus R. Luhanga 5258
35 Dr. Noreen Jandwa 5279
36 Dr. Flora Willy Rumoka 5299
37 Dr. Gabriel C. Makenga 5303
38 Dr. Joel L. Maduhu 5307
39 Dr. Joan J. Nguma 5298
40 Dr. Museveni N. Justine 5349
41 Dr. Emanuel Nhonoli 4847
42 Dr. Ally Akrabi Munir 4773
43 Dr. Regina Mtayangulwa 4753
AMANA
1 Dr. Fredrick Tembo 5265
2 Dr. Daudi Hassan 5267
3 Dr. Tumaini Bryon 5247
4 Dr. Tenga Yerko 4886
5 Dr. Majala Maulidi 4870
6 Dr. Elice Mweluka 4877
7 Dr. Kibona Samwel 5296
8 Dr. Abdulrahan Amin 5037
9 Dr. Alexander Kailembo 366
10 Dr. Mwanaasha Malewenga 5448
11 Dr. Valeria Ndomba 5390
12 Dr. Anna Sanga 5016
13 Dr. Luoga Prospelia 4850
14 Dr. Georgia Kamese 5052
15 Dr. Ally Mbikilwa 5450
16 Dr. Peter Kyabaroti 5016
17 Dr. Mamelita Basike 5402
18 Dr. Mariam Msimbe 5191
19 Dr. Khadija Msami 5300
20 Dr. mosses Wamoa 5038
21 Dr. Jasinta Lugila 5363
22 Dr. hellen Machagge 5249
23 Dr. Anna Asenga 5265
24 Dr. Salum Mruma 5268
25 Dr. Neema Ntamanwa 5291
26 Dr. Fatuma Kibao 5316
TEMEKE
1 Dr. Godbless Charles 5168
2 Dr. Henry Jason Tarimo 4632
3 Dr. Clephace G. Mtana 4907
4 Dr. Daniel Joseph Mganyizi 4992
5 Dr. Elisha Otieno Osati 5336
6 Dr. Tony Mitala Luwukya 5455
7 Dr. Emmanuel G. Badya 4912
8 Dr. Phillipo S. Muhochi 4993
9 Dr. Alen Oden Kitalu 4994
10 Dr. Frexon Liseki Kiandiko 5180
11 Dr. Rose Sikazwe 5214
12 Dr. Nevelin Hezron 5216
13 Dr. Daniel A. Mashamba 5212
14 Dr. Hadija M. Kimwaki 5260
15 Dr. Lucas James Maiga 5400
16 Dr. Odiwa C. Ombati 5452
17 Dr. Thomas D. Kapela 4906
ST. FRANCIS IFAKARA
1 Dr. Greyson Mpinga 5403
2 Dr. Kasanzu Masanja 5262
3 Dr. Haitham Mohamed 5450
4 Dr. Massanja Dotto 5263
5 Dr. Nicholaus Sayana 4937
6 Dr. Kahibi Bernard 5055
7 Dr. Emmanuel Kimario 5098
8 Dr. Rebeca Majige 5064
9 Dr. Allen Kissanga 5321
10 Dr. James Zakaria 5326
11 Dr. Kurenje Mbura 5264
12 Dr. Nyambura Moremi 4920
13 Dr. Donald Kenedy 5056
14 Dr. Elipokea Sarakikya 5314
15 Dr. Magreth Kagashe 4894
16 Dr. John Mrina 4843
17 Dr. Sebastian Pima 5053
M/ NYAMALA
1 Dr. Veronica Lyandala 4908
2 Dr. Goodluck Mlimbila 4938
3 Dr. Geofrey Seusi 4923
4 Dr. Zena Suleiman 5087
5 Dr. Fadhil Mlimbila 5225
6 Dr. Wilfred Rutahoile 4882
7 Dr. Ikupa Mwasubi 5076
8 Dr. Janeth Mandepu 5025
9 Dr. Paul Swakala, 4928
10 Dr. Mwandu Makani 4929
11 Dr. Vivian Rugarabamu 5033
12 Dr. Mufida Mshimba 5133
13 Dr. Didas Patris 5069
14 Dr. Adelina Rutashobya 5112
15 Dr. Kunge Klint 5235
16 Dr. Pius Ezekiel 5272
17 Dr. Daniel Hubert 5290
18 Dr. Petro Sewa 5271
19 Dr. Diana Damian 5331
20 Dr. Egbert Eslone 5340
21 Dr. Meshack Ole Sabaya 5432
22 Dr. Manyere J. Kapongo 5428
23 Dr. Joseph Mkenda 5429
24 Dr. Wendy Robert 5430
25 Dr. Eshmedi Mathayo
26 Dr. Jualako Nassoro 4775
SEKOU TOURE HOSPITAL
1 Dr. Akili Msei 5412
2 Dr. Patrick Mhagama 5415
3 Dr. Vitalis Ruyimba 5422
4 Dr. Robert Onesmo 5418
5 Dr. Catherine Moshi 5463
6 Dr. Musyangi Tekele 5445
7 Dr. George Ngimba 5420
8 Dr. Elias Ndongo 5275
9 Dr. Belkumas.H. Mbawala 5454
10 Dr. Ezekiel Kambona 4948
11 Dr. Zakayo Ilomo 5444
12 Dr. Yahaya Nasoro 4781
13 Dr. Rehema Mwabaya 5459
14 Dr. Grace Bash 5464
HYDOM HOSPITAL
1 Dr. Edwad Lengai 4990
2 Rommy andrew 5389
3 David Mgaya 4854
4 Innocent mtenga 5049
5 Edward Joseph 5011
6 Israel Alexseko 4901
7 Angelo Joachim 5042
8 Deogratius Baruba 4991
9 Johnson Joachim 5034
10 Evarist Kentgen 5043
11 Gabriel M. Soko 4915
DODOMA REGIONAL HOSPITAL
1 Gustavus Deusdedith 5385
2 Cassian G. Mkuwa 5384
Imetolewa na:
Dkt Donan Mmbando
MWENYEKITI- BARAZA LA MADAKTARI TANGANYIKA
11 Julai, 2012.


Reactions::

Profesa Mahalu Kusuka Au Kunyoa Leo


Tausi Ally
MAHAKAMA ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo inatarajia kutoa hukumu ya kesi ya uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya Euro 2 milioni, sawa na Sh3.1bilion  inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania, nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na Ofisa Utawala wa ubalozi huo, Grace Martin.

Hukumu ya kesi hiyo iliyokuwa ikinguruma mahakamani hapo kwa miaka kadhaa sasa, itasomwa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Ilvin Mgeta.

Profesa Mahalu  na Grace wanakabiliwa na mashtaka sita likiwemo la uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara hiyo.

Mei 8 mwaka huu Grace ambaye alikuwa Ofisa wa Utawala aliieleza mahakama hiyo ya  Kisutu kuwa Balozi  Mahalu hakuisababishia serikali hasara  ya kiasi hicho cha fedha, bali alileta faida kwa taifa kwa   kuwa na jengo zuri na kwamba anahitaji kupewa shukrani.

Akiongozwa na Wakili Mabere Marando  kujitetea dhidi ya tuhuma zinazomkabili, Grace alidai kuwa kwa ufahamu wake Balozi Mahalu hakuisababishia serikali hasara kwa kuwa manunuzi yalileta faida na nchi kupata jengo zuri na hakuna fedha zilizopotea.

“Mheshimiwa kwa ufahamu wangu, Balozi Mahalu mashtaka yote sita yanayomkabili hakuyatenda, aliwasilisha  mikataba miwili kama taarifa iliyofanyika kihalali,”alidai Grace.

Aliendelea kuiomba mahakama itupilie mbali tuhuma hizo  na kwamba madai ya kuwa Balozi Mahalu alitumia risiti ya ununuzi wa jengo la ubalozi wa Tanzania nchini Italia kuidanganya serikali kuwa mwenye nyumba amelipwa fedha siyo ya kweli.

Hata hivyo, akiongozwa na Wakili Marando, Grace  alihoji ni kwanini upande wa Jamhuri haukumleta mmiliki wa jengo hilo la ubalozi wa Tanzania nchini Italia  kukana risiti hiyo  au Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( Takukuru), Edward Hossea  na Fungo  kuulizwa juu ya ununuzi wa jengo hilo kwa sababu walikwenda nchini humo kufanya uchunguzi. SOMA ZAIDI http://mwananchi.co.tz/habari/5-habari-za-siasa/24659-profesa-mahalu-kusuka-au-kunyoa-leo

Reactions::

Ukiriguru Hii




Reactions::

Magazeti Leo Jumatano




















Reactions::

CHADEMA Hawana Imani Na Polisi, Wagoma Kuhojiwa


Dkt Slaa.


Dk. Peter Slaa akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na wanahabari leo.

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema hakiwezi kukubali viongozi wake wanaodaiwa kutishiwa maisha kuhojiwa na Jeshi la Polisi kama imevyoelekezwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi kwani hawana imani na Polisi. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Peter Slaa alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari Makao Makuu ya chama hicho Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Akitoa tamko hilo ambalo limepitishwa na Kikao cha Kamati Kuu iliyokutana tangu juzi, Dk. Slaa amesema hawaoni sababu ya kuhojiwa na Jeshi la Polisi kwa kuwa wamewahi kuwapa taarifa nyingi za vitisho dhidi yao na hakuna hata moja imefanyiwa kazi.

“Hatuwezi kwenda Polisi kwa sababu tumekuwa tukipeleka mambo mengi ya vitisho lakini hayafanyiwi kazi…na hili tulisha waambia hatuendi kwao labda watukamate,” alisema Dk. Slaa akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema yeye mwenyewe licha ya kuwasilisha madai mbalimbali aliwahi kutegeshewa vinasa sauti na kutoa taarifa polisi lakini tangu wachukue vifaa hivyo hawajasema chochote hadi leo, jambo ambalo limewafanya waamini hata wakienda huko hakuna chochote kitafanyika.

Dk. Slaa alisema leo asubuhi alipigiwa simu na mmoja wa maofisa upelelezi kutoka Makao Makuu ya Polisi akiomba miadi ya kukutana naye, jambo ambalo amesema hayupo tayari kuhojiwa na wanausalama hao wa raia labda wamkamate.

Alisema tayari baadhi ya viongozi wa Serikali wameanza kuipuuza malalamiko yao dhidi ya vitisho wakidai huenda viongozi wa CHADEMA wanatafuta umaarufu wa kisiasa kwa kutoa taarifa hizo, kitendo ambacho amesema umaarufu wao hautatokana na viongozi wa Serikali au CCM bali ni kwa kazi wanazozifanya kwa wananchi.

Juzi Dk. Nchimbi alisema taarifa za kutishiwa maisha dhidi ya viongozi wa CHADEMA ni nzito hivyo haziwezi kupokelewa kirahisi Jeshi la Polisi linaanza kazi ya kuwahoji wahusika ili kulifanyia kazi jambo hilo. Alisema suala la usalama wa raia si hiyari bali ni la lazima hivyo hata kama wahusika hawataki lazima taratibu zifanywe kuhakikisha usalama kwa wahusika.

Wakati huo huo CHADEMA inaanza ziara ya Oparesheni Sangara ambayo itafanyika katika mikoa mitano ya Tanzania ikiwemo Dodoma, Morogoro, Iringa na Manyara. Akizungumzia ziara hiyo ambayo itashirikisha viongozi wa juu wa CHADEMA, Wabunge, Wajumbe pamoja na viongozi wengine wa ngazi mbalimbali. Dk. Slaa amesema ni ziara ya kukiimarisha chama ikiwa ni pamoja na kuangalia mchakato wa uchaguzi wa chama hicho unaoendelea ngazi za chini.

Alisema katika ziara hiyo ambayo kauli mbiu yake ni “Hakuna Kunywa, Kula wala Kulala” inatarajiwa kuzunguka katika majimbo ya uchaguzi 44 ya mikoa hiyo, Kata 806 na vijiji 4,000. Ziara hiyo inatarajia kutumia siku 104.

Akifafanua zaidi kuhusiana na ziara hiyo amesema CHADEMA ni chama ambacho kinajitofautisha na vyama vingine katika utendaji wake na ndiyo maana wanaendelea kufanya ziara zao vijijini kuangalia maisha ya wananchi mpango ambao ni mpya.

“Kuna taarifa za baadhi ya watu wanabeza ziara zetu kwamba zinalenga posho…no CHADEMA hakuna posho, kwenye ziara zetu tunakula hadi kwa mama ntilie (chakula cha kawaida), tutaendelea kupiga kelele hadi pale haki za Watanzania zitakapokuwa zikipatikana bila vikwazo…tunapigania haki ya kila mmoja awe mwanafunzi, wafanyakazi, wakulima na hata madaktari,” alisema Dk. Slaa.
Chanzo: http://www.hakingowi.com
Reactions::

Tuesday, July 10, 2012


Bado Niko Stockholm Na Leo....

Leo nimeshiriki kikao kirefu cha kazi hapa Stockholm, Sweden.
Kikao kimekwenda vizuri sana.
Usiku huu nitaingia mitaa ya kati ya Stockholm. Stockholm imechangamka sana wakati wa summer kama hii.
Usiku mwema.
Maggid

Reactions::

Furahia Muda Wa Maongezi Bure Kutoka Vodacom

Furahia muda wa maongezi BURE! Tuma hela kupitia M-pesa wewe na unaye mtumia mpate muda wa maongezi kutoka Vodacom!

Reactions::

Kijiweni Cha Miwa...

    Mzee mtu mzima akimuuzia miwa kijana ambaye hakufahamika jina,leo jioni eneo la Kihesa Iringa.
Reactions::

Uchaguzi Wako + Matendo Yako = Tukio


Mara nyingi nimekuwa nikiongelea ile kanuni isemayo ‘uchaguzi wako + matendo yako = tukio’ au fikra zako + uamuzi wako = tukio yaani (Event+ Response=Outcome) Usikose Makala yangu kesho katika gazeti la Kwanza Jamii-Iringa.
MeshackMaganga-Mjengwablog.

Reactions::

Ubunifu...

                                           Bao la mchangani...ni Mwangata Iringa.
Reactions::

Wakamatwa Wakisafirisha Bangi kwenye Madumu Ya Mafuta Ya Kula-Iringa


Hawa ni askari Polisi wa Mjini Iringa, usidhani walikuwa wakinunua mafuta ya kula, Hapana. Ndani ya madumu hayo ya kuhifadhia mafuta walibaini kuwepo kwa bangi iliyokuwa ikisafirishwa kupelekwa Tunduma, Mbeya


Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Peter Kakamba akitoa na kuonesha bangi kutoka katika moja ya madumu ya mafuta aina ya Oki.


Fadhil Juma (kushoto) na Baraka Mwinuka (kulia) wakiwa ndani ya ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa baada ya kukamatwa na kilo 60 za bangi zilizokuwa zimejazwa ndani ya madumu ya mafuta ya kula yaliyotobolewa kwa chini.Chanzo: www.frankleonard.blogspot.com

Reactions::

Pilipili...

                        Ni jioni biashara haijachanganya...Iringa leo.     
Reactions::