Pages

NA HURU NI MREMBO ALIYEACHANA NA CHRISS BROUWN KISA DRAKE

Jul 19, 2012

Stori mtaani ni kwamba mwimbaji Star Chris Brown ameachana na girlfriend wake aitwae Karrueche na hiyo yote ni kwa sababu ya Drake.
Mtandao wa Hellobeautiful UMESEMA kwamba Kilichotokea ni baada ya Chris Brown kugundua kwamba Karruche amekua akiwasiliana na Drake japo sio kwamba wako kwenye mapenzi, wamekua wakiwasiliana kwa ishu za kibiashara.
Chris ameshindwa kuvumilia baada ya kugundua kwamba mpenzi wake anawasiliana na adui yake (Drake) ambae zaidi ya siku 30 zilizopita walikua kwenye ugomvi mkubwa uliotokea kwenye club moja ya usiku New York Marekani.
Kingine alichokifanya Chris Brown ni kufuta picha zote alizokua ameziweka Twitter na Instagram akiwa na Karrueche.