Pages

Fid Q afunika Wajanja Tour Mtwara

Jul 10, 2012

Fid Q afunika Wajanja Tour Mtwara

Msanii Mkongwe wa Muziki wa kizazi kipya Fid Q akiwapagawisha wakazi wa Mkoa wa Mtwara hapo jana wakati wa tamasha la"WAJANJA" linaendeshwa na Vodacom Tanzania,Jumapili ijayo litafanyika  katika mkoa wa Tanga likiwa na lengo la kuwaelimisha wananchi kutumia mtandao wa kampuni hiyo kwa kuongea kwa robo shilingi na kutuma ujumbe kwa shilingi ishirini na tano kwenda mtandao wowote  na kutumia facebook na twitter

Katika hali isiyotarajiwa na wengi Msanii na Mkali wa Bongo Fleva Farid Kubanda maarufu kama Fid Q juzi alifunika katika shoo wa Wajanja tour  ya Vodacom iliyofanyika Mtwara jumapili hii na kusababisha mashabiki waliojitokeza katika tamasha hilo kukataa asishuke jukwaani.
Fid Q aliepanda jukwaani majira ya saa kumi na moja na nusu baada ya Diamond kumaliza Shoo yake,  na alipopanda jukwaani umati wa wana Mtwara ulilipuka kwa shangwe na kuwapa wakati mgumu mabaunsa waliokuwa wakisimamia shoo hiyo. Hata alipomaliza nyimbo zake mashabiki walipiga kelele kutaka aendelee kuimba na kumwita Ngosha! Ngosha!Ngosha!nakuanza kulisukuma basi alilo[panda msanii huyo mpaka nje ya uwanja.

Wasanii wengine waliofunika katika Show hiyo ni Pamoja na Diamond, Shetaa, Ney wa mitego na Mabeste,


Akizungumza na waandishi wa Habari Meneja Mahusiano wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu amesema kuwa Tour ya Wajanja wa Vodacom itafanyika siku ya jumapili ya wiki hii Mkoani Tanga katika uwanja wa Mkwakwani.


"Wajanja tour sasa inaelekea kwa "waja leo waondoka leo" mkoani Tanga baada ya kufunika vilivyo Mkoani Mtwara hivyo wakazi wa Tanga wajiandae kupata burudani kutoka kwa wasanii kibao watakao kuwa katika Tamasha hilo." Alisema Nkurlu.