Pages

MISS UTALII KANDA YA ZIWA YAFUTWA

Jul 21, 2012
BODI ya Taifa ya Miss Tourism Tanzania Organization (MTTO), imelifuta shindano la Miss Utalii Kanda ya Ziwa 2012, lililo fanyika New Mwanza Hotel, juzi, huku taifa likiwa kwenye maombolezo ya siku tatu kutokana na msiba mkubwa wa ajali ya meli ya Mv Skagit, mjini Zanzibar na
kupoteza uhai wa watu wengi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa katika vyombo vya habari jana jijini Dar es Salaam na kutiwa sahihi na Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Miss Utalii Tanzania, Abubakari Omary Bakari, ilisema shindano hilo limefanyika kimakosa na matokeo yake hayawezi kutambuliwa kwa namna moja ama nyingine.

Alisema uamuzi wa serikali ni wa mwisho, hivyo hawajaunga mkono kufanyika kwa shindano hilo wakati nchi ina majonzi ya kupoteza ndugu na jamaa wao.