Pages

BUGURUNI WAONJA JOTO LA JIWE KWA WIZI WA UMEME

Jul 25, 2012
Mtuhumiwa wa wizi wa umeme Jeilan Mohamed, akiongozwa na jeshi la polisi kupanda gari baada ya kutuhumiwakuliibia umeme shirika hilo kwa njia ya kuunganisha kabla haujafika kwenye mita (kubaipass) maeneo ya Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam. 




WATU watano wakazi wa Buguruni jijini Dar es Salaam wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za wizi wa umeme kufuatia operesheni kaliinayoendeshwa na shirika la umemem Tanzania kupitia kanda zake za Ilala, Kinondoni na Temeke.
Kwenye zoezi hilo ambalo juzi lilifanyika kwenye maeneo ya buguruni watu watu watano walikutwa wakiiba umeme kwa njia ya kuchezea mita kwa kuchukua umeme kabla haujafika kwenye mita ambayo kitaalamu hujulikana kama (bypass).
  
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye eneo la tukio Meneja wa Shirika hilo kanda ya Ilala Athanasius Nangali amesema kuna kila sababu ya zoezi hilo kuwa endelevu kutokana na watu wengi kuiba umeme.
Nangali amesema tatizolililopo kwa sasa sio la wateja wapya wanaounganishiwa sasa bali ni la wateja wazamani wanachezea mita ili waibe jambo ambalo halikubaliki hata kidogo.
“Akitoa mfano wa kwenye nyumba ambayo inamilikiwa na mmoja wa watuhumiwa hao ambaye ni Jeilan Mohamed, huyu ni mteja wetu wa siku nyingi lakini umeme aliokuwa akiiba ni asilimia 75 na kulitia hasara shirika hilo.
Aidha katika hatua nyingine ya kuongeza nguvu kwenye zoezi hilo Meneja huyo ametoa ofa kwa yeyote atakaetoa siri na kusaidia kukamatwa mwizi wa umeme atapata zawadi ya Tsh.50,000 kwa kila nyumba itakayokutwa inaiba umeme.
Akijibu maswali ya waandishi waliotaka kujua ufanisi wa zoezi hilo Nangali alisema linamafanikio makubwa kwani hadi sasa wamefanikiwa kukusanya zaidi ya Tsh 80millioni.
Aidha nangali pia ametoa ofa kwa wezi watakaojisalimisha wenyewe wataepuka kufikishwa mahakamani lakini badalayake watalazimika kufanyiwa hesabu ya umeme walioiba na kuulipia katika kipindi chote cha wizi.
Zoezi hilo linaendelea tena maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
 
CHANZO