Pages

DOWNLOAD TRACK MPYA YA BOB JUNIOR INAITWA KIMBIJI

Jun 29, 2013
Read more ...

WEMA SEPETU ASHITAKIWA NA MAJIRANI.

Jun 28, 2013
Habari ni kuwa juzi kati Wema Sepetu alishitakiwa na majirani zake kwa tabia ya wafanyakazi wake kutiririsha maji machafu mtaani. globalpublishers imeripoti kuwa majirani wa actress huyo anayekaa Kijitonyama Dar es salaam wamekuwa wakimlalamikia muigizaji huyo kwa kitendo hicho na uvumilivu ulipowashinda ndiyo wakaamua kumchoma kwa serikali ya mtaa. "mara kwa mara wafanyakazi wake wamekuwa wakitiririsha maji hapa mtaani sasa leo tumeona tukamshitaki serikali za mitaa ili sheria ichukue mkondo wake" alisema mmoja wa majirani wa Wema aliyeomba jina lake lihifadhiwe.

Afisa mtendaji wa kata ya Makumbusho pia alifika nyumbani kwa muigizaji huyo kuhusiana na tatizo hilo, msichana mmoja wa kazi aitwae Bite alitoka na kujitetea lakini walionekana wana makosa hivyo kutakiwa kwenda ofisi za kata kwa maelezo zaidi. Hata hivyo amri hiyo ilionekana kuwaweka katika wakati mgumu hivyo busara zilitumiwa na kiongozi huyo na kuwataka watoe faini na mfanyakazi huyo kuingia ndani na baadaye kutoka na kiasi cha pesa ikisadikika Wema ndiye aliyetoa pesa hizo ingawa haikujulikana mara moja ni kiasi gani na walisainishana. Pia kiongozi huyo aliwaonya waache tabia hiyo ya kutiririsha maji machafu mtaani. Hata hivyo Wema alipotafutwa kwa simu alikuwa hapokei na mwandishi alipofika nyumbani kwake aliambiwa hayupo.


Read more ...

Usafi wa Jiji hadi aje Rais Obama?

Jun 28, 2013

Kuelekea ujio wa Rais Barack Obama nchini wiki ijayo, Jiji la Dar es Salaam ambalo ndilo litakuwa mwenyeji wa mgeni huyo na ujumbe wake hivi sasa limo katika hekaheka kubwa za kuandaa mazingira stahiki kwa ugeni huo. Dar es Salaam ni moja ya majiji machafu sana duniani, hivyo kila juhudi zinafanywa na mamlaka husika kuliweka jiji hilo katika hali ya usafi kabla ya ugeni huo haujawasili.
Sasa sehemu nyingi za barabara zinatengenezwa usiku na mchana kwa kujengwa upya au kuzibwa mashimo, ambayo baadhi yake yalikuwa makubwa mithili ya mahandaki. Katika baadhi ya barabara, mchanga na udongo uliokuwa umezimeza kutokana na kutotunzwa kwa muda mrefu sasa vimeondolewa.
Taka zilizokuwa zimezagaa kila kona sasa zinazolewa kwa kutumia magari ya Jiji na ya wamiliki binafsi. Katika sehemu muhimu za Jiji, madawa ya kuua mbu na wadudu yamenyunyizwa, huku baadhi ya wamiliki wa majengo katika sehemu atakazopita Rais Obama wakilazimika kupaka rangi majengo hayo. Harufu mbaya iliyokuwa imeligubika Jiji kutokana na uchafu sasa imepungua kwa kiasi kikubwa.
Ghafla vijana kutoka vijiweni wamepewa ajira ya muda kufyeka nyasi, kuzibua na kusafisha barabara na mitaro iliyojaa majitaka. Kumbe wanakaa vijiweni sio kwa kutaka, bali kwa kukosa ajira. Polisi nao wameendesha kamatakamata ya vijana wengi inaodai ni vibaka, wavuta bangi na vitendo vingine vya kihalifu, huku lengo kubwa likiwa ni kusafisha mitaa kabla ya ujio wa Rais Obama. Wakati huohuo, Machinga wameondolewa katika sehemu atakazopita mgeni huyo na ujumbe wake na vibanda vyao vimefyekwa na tingatinga za Jiji, huku wananchi waishio mikoani wakitahadharishwa kutokuja Dar es Salaam wakati Rais Obama atakapokuwa jijini.
Jiji la Dar es Salaam zinazoendelea hivi sasa jijini kuelekea ujio wa ugeni wa Rais huyo wa Marekani. Tumefanya hivyo kwa sababu mbili kubwa. Kwanza ni kuonyesha kwamba Jiji la Dar es Salaam na Serikali Kuu vinao uwezo mkubwa wa kulifanya jiji hilo kuwa safi wakati wote. Pili ni kuonyesha jinsi tunavyojidhalilisha kama taifa kwa kuishi katika mazingira machafu, lakini tunachukua hatua za zimamoto na kukimbizana kufanya usafi tunapoona wageni wanatembelea nchi yetu.
Ni aibu iliyoje kwa Watanzania kuishi katika mazingira machafu tukisubiri wageni waje ndio tufanye usafi. Ni dharau na matusi ya viongozi wetu kwa wananchi, kwamba watu muhimu na ambao wanastahili kuwekwa katika mazingira mazuri ni wageni. Wananchi wanasakamwa walipe kodi na wanafanya hivyo. Pamoja na kulipa kodi hizo, mamlaka husika hazioni umuhimu wa kuwatengenezea wananchi mazingira mazuri kwa kuzoa taka, kutengeneza barabara, kufyeka nyasi, kunyunyizia dawa katika mazalio ya mbu na kadhalika.
Usafi wa mazingira na wa kila mwananchi ni muhimu mno katika ustawi na maendeleo ya binadamu. Wakati kila mwananchi analo jukumu la kutunza usafi kwa nafsi yake na mazingira yaliyomzunguka, mamlaka husika zinapaswa kuwawezesha wananchi kufanya hivyo. Inawezekanaje halmashauri za miji na wilaya, kwa mfano, zishindwe kuweka magari ya kuzoa taka kutoka barabarani na mitaani? Zipo wapi dampo za kumwaga maelfu ya tani za taka zinazozalishwa katika makazi ya watu mijini kila siku?
Read more ...

Ndege 8 kubwa za Obama Zatua Dar

Jun 28, 2013

Mmoja ya Madege ya Marekani yaliotua Tanzania.Dar es Salaam, Tanzania.Makachero wa Marekani wameendelea na matayarisho ya mwisho ya ziara ya Rais Barack Obama, na katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere walikuwa na kazi ya kuunganisha helikopta za doria.


Makachero hao walikuwa wakiunganisha helikopta sita zilizosafirishwa vipande vipande kutoka Marekani, ambapo meli mbili za kivita na ndege moja pia zimewasili.


Rais Obama tayari yuko katika ardhi ya Afrika, na  leo anatarajiwa kwenda Afrika Kusini baada ya kumaliza ziara yake ya kwanza Senegal na anatarajiwa kuwasili nchini Jumatatu.


Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa jana unaonyesha Marekani imeleta helikopta hizo kwa ajili ya ulinzi wa Rais Obama, zikiwamo meli zilizobeba helikopta nyingine mbili na ndege.

Habari zilizopatikana kutoka kwa wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, zinasema kuwa helikopta sita zinaunganishwa katika sehemu ya karakana ya Kikosi cha Anga cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Mtu mmoja amesema helikopta hizo zililetwa kama vipande vipande vilivyosafirishwa kama mzigo kwenye meli za kivita zilizotia nanga jijini Dar es Salaam.


“Nilikaribia kwenye eneo la karakana na nikashangaa kuona jinsi jamaa walivyokuwa ‘bize’ wakiunganisha vyuma mbalimbali na kutengeneza helikopta hizo,” amesema mtu huyo.


Inaaminika kuwa helikopta hizo zitakuwa zinasaidia kusafirisha watu na mizigo kutoka kwenye meli za kivita ambazo zimeegeshwa kwenye Kikosi cha Maji cha JWTZ.

Pia helikopta mbili zinaaminika ziko katika meli ambazo zimeegeshwa huko Kigamboni.


Meli za kivita na ndege ya kijeshi


Katika hatua nyingine, meli mbili za kivita ambazo zimetengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu zimeegeshwa Kigamboni.

“Jamaa wana meli kali kwa kweli, mimi nimekuwa askari wa Kikosi cha Maji kwa muda mrefu na kufanya mazoezi na mataifa kadhaa, lakini sijaona meli kama zile.

“Wamarekani wanatisha sana. Meli zao zina zana muhimu za kivita. Pia wanafuatilia kila kitu kinachoweza kuhatarisha usalama wao. Hawaamini mtu kabisa wala kudharau chochote,” amesema mtoa habari mmoja.

Ndege ya kijeshi

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa kuna ndege ya Jeshi la Marekani, lakini imeegeshwa kwenye karakana ya Kikosi cha Anga cha JWTZ.


Ndege hiyo inadaiwa iko nchini tangu mwanzoni mwa wiki hii, ingawa kuna taarifa kuwa zipo ndege nyingine ambazo zimekuwa zikitua na kuruka.


“Ndege nyingi za Wamarekani zinatua nchini kwa kipindi cha wiki mbili sasa, zaidi zinaleta watu, ambao nahisi ni wale wanaohusika na usalama na mizigo.


“Kimsingi kuna mambo mengi yanaendelea hapa uwanja wa ndege. Ila msisahau pia kuna ujio wa marais kutoka sehemu mbalimbali duniani kwa ajili ya mkutano wa Smart Partnership ndiyo maana kuna mengi yanaendelea hapa,”  chanzo cha habari kimesema. Chanzo: Mwananchi.co.tz
Read more ...