Habari ni kuwa juzi kati Wema Sepetu alishitakiwa na majirani zake kwa tabia ya wafanyakazi wake kutiririsha maji machafu mtaani. globalpublishers imeripoti kuwa majirani wa actress huyo anayekaa Kijitonyama Dar es salaam wamekuwa wakimlalamikia muigizaji huyo kwa kitendo hicho na uvumilivu ulipowashinda ndiyo wakaamua kumchoma kwa serikali ya mtaa. "mara kwa mara wafanyakazi wake wamekuwa wakitiririsha maji hapa mtaani sasa leo tumeona tukamshitaki serikali za mitaa ili sheria ichukue mkondo wake" alisema mmoja wa majirani wa Wema aliyeomba jina lake lihifadhiwe.
Afisa mtendaji wa kata ya Makumbusho pia alifika nyumbani kwa muigizaji huyo kuhusiana na tatizo hilo, msichana mmoja wa kazi aitwae Bite alitoka na kujitetea lakini walionekana wana makosa hivyo kutakiwa kwenda ofisi za kata kwa maelezo zaidi. Hata hivyo amri hiyo ilionekana kuwaweka katika wakati mgumu hivyo busara zilitumiwa na kiongozi huyo na kuwataka watoe faini na mfanyakazi huyo kuingia ndani na baadaye kutoka na kiasi cha pesa ikisadikika Wema ndiye aliyetoa pesa hizo ingawa haikujulikana mara moja ni kiasi gani na walisainishana. Pia kiongozi huyo aliwaonya waache tabia hiyo ya kutiririsha maji machafu mtaani. Hata hivyo Wema alipotafutwa kwa simu alikuwa hapokei na mwandishi alipofika nyumbani kwake aliambiwa hayupo.