Pages

Mrisho Mpoto atangaza ofa kwa wezi waliomuibia vifaa vya gari, yuko tayari kuvinunua tena kwa milioni 2 kutoka kwao

Oct 18, 2013
mpoto amedai kuwa mbali na vifaa vya gari lake ambavyo vimeibiwa na wezi hao pia kuna vitu vingine muhimu vikiwemo vitabu vyake, hivyo amewasihi wezi hao wamrudishie vitu hivyo
Kupitia ‘You Heard’ ya XXL leo Mjomba ametangaza ofa kwa yeyote aliyehusika kumuibia amrudishie vitu vyake na kuongeza kuwa yuko tayari kuvinunua kutoka kwa wezi hao kiasi kisichozidi shilingi 2,000,000

natumia fursa hii au nafasi hii kuwaomba mnirudishie aidha kwa kunionea huruma kama mjomba, lakini pia niko tayari kulipia na kiasi ambacho naweza nikaahidi kulipia kwa mtu ambaye ataweza kunirudishia vitu vyangu ni thamani ya shilingi milioni mbili niko tayari kurudisha, kwahiyo wezi mlioiba vitu vya mjomba naomba mnirudishie tafadhali Alisema mjomba Mrisho Mpoto
Read more ...