Pages

ABG Supports Training Of Medical Students At Bugando

Nov 20, 2012

                                              
The doctor-in-charge of the Sengerema designated district hospital, Sister Dr. Marie Jose, speaks at the launch of the "Treat & Train" programme in Sengerema district, Mwanza region, recently. African Barrick Gold (ABG) has donated $130,000 to expand access to healthcare in the Lake Zone regions of Tanzania.
A section of students from the Bugando Medical Centre who are studying to become Assistant Medical Officers (in white coats) listen to proceedings at the launch of the "Treat & Train" programme. African Barrick Gold (ABG) has donated $130,000 to expand access to healthcare in the Lake Zone regions of Tanzania.
African Barrick Gold (ABG) has partnered with the Bugando Medical Centre (BMC), the Catholic University College of Health Sciences (CUHAS) and the Touch Foundation to increase access to healthcare for thousands of patients in Tanzania’s Lake Zone through the training of medical students.

Healthcare delivery and patient access to medical care in the densely-populated Lake Zone area is amongst the worst in Tanzania, which has an average of only one doctor for every 20,000 people.

ABG has thus donated US$130,000 (approximately 200 million Tanzanian shillings), through the ABG Maendeleo Fund, to the training programme developed by BMC, CUHAS and the Touch Foundation, a not-for-profit organization dedicated to improving access to quality, basic healthcare and training healthcare workers in sub-Saharan Africa.

“ABG is pleased to work with CUHAS, BMC and the Touch Foundation to support the training of medical students and to improve access to medical care in the Lake Zone,” said Deo Mwanyika, Vice President Corporate Affairs

The Treat & Train programme, an innovative and cost-effective care and treatment programme, brings paediatric, surgery, internal medicine and obstetrics/gynecology specialists to help train students and to treat patients in the Lake Zone, thereby increasing access to medical care in rural areas.  Senior Vice President to Touch Dr. Steve Justus notes, “the Treat & Train program will also have the added benefit of helping doctors and specialists feel part of an integrated system and improve referrals throughout the Lake Zone, thereby increasing retention of healthcare workers in the Lake Zone.”

In collaboration with public and private partners, the Touch Foundation has been working with BMC and CUHAS since 2004 to train hundreds of new healthcare workers, including urgently-needed doctors, nurses and laboratory technicians.

ABG’s donation benefits medical students and thousands of patients in the Lake Zone regions, who usually have to travel for long distances to access medical services.

The programme works by pooling and rotating cross-disciplinary, highly trained clinical teams to rural facilities throughout western Tanzania.

The innovative system, which also supports rotations of assistant medical officer students and medical students from BMC and CUHAS, respectively, and overseen by posted specialists and rotating CUHAS faculty, gives rural patients increased access to skilled health workers.

Reactions::

CRC Members For Capacity Building


Constitutional Review Commission (CRC) Secretary Mr. Assaa Rashid (centre) chats with Board Member of the Open Society Initiative for East Africa (OSIEA) Prof. Chirss Maina Peter (right) when the OSIEA delegation visited the CRC offices in Dar es Salaam today . Left is the OSIEA Director Ms. Binaifer Nowrojee.
Constitutional Review Commission (CRC) Chair Joseph Warioba (left) chats with Ms. Binaifer Nowrojee (2nd right), the Director of Open Society Initiative for East Africa (OSIEA) and its Board Member Prof. Chirss Maina Peter (right) when the two paid him a courtesy call at his Dar es Salaam office today (Tuesday, November 20, 2011). Looking on is the CRC Deputy Secretary Mr. Casmir Kyuki.

By:  Special Correspondent
The Constitutional Review Commission (CRC) has highlighted three areas which it plans to undertake capacity building measures for its members so that they make informed decisions
Speaking to the delegation of the Nairobi-based Open Society Initiative for Eastern Africa (OSIEA) in Dar es Salaam today (Tuesday, November 20, 2012) the CRC Chairman, former Prime Minister Joseph Warioba said that the measures were aimed at enabling CRC members to make informed decisions as they prepare draft constitution.
The OSIEA delegation, led by its Director Ms. Binaifer Nowrojee and accompanied by its Tanzania Programme Officer Ms. Shamshad Rehmatullah and its Board Member Prof. Chriss Maina Peter paid a courtesy call to Mr. Warioba at his Dar es Salaam office and discussed various ways of collaboration. The meeting was also attended by the CRC Secretary Mr. Assaa Rashid and his Deputy Mr. Casmir Kyuki.
According to Mr. Warioba, the capacity building measures will cover three areas namely types of electoral systems, state ownership in the management of natural resources especially land and social security.
Apart from the three, Mr. Warioba also said his Commission was ready to work with other stakeholders in area of public education especially during constitutional fora stage, currently scheduled for June 2013, when common representatives of wananchi will discuss the draft constitution.
On the electoral system, Mr. Warioba, hinted that the CRC was receiving conflicting views from members of the public on the best type electoral system that was democratic but also affirmative.
“You know that currently we have over 350 Members of Parliament (MPs), some under special seats … as we collect views from members of the public, we receive conflicting views on these,” said Mr. Warioba explaining that some people want the special seats retained in the new Constitution while others proposes for their abolishment.
“We are looking at what type of electoral system is democratic and also affirmative,” he said adding that it was crucial for members of the Commission to be well informed before drafting anything on the issue.
On management of natural resources, the CRC Chairman said according to the opinions the CRC is receiving so far, ownership and allocation of land and other natural resources was critical and the CRC members needed to be well informed especially on areas of public participation and decision making processes on natural resources.
Commenting on the areas, Ms. Nowrojee said her firm was ready to support the CRC in realising its plans and requested for detailed proposal.
“We are ready to support all these plans as we have done in other countries. We basically assist what you ask for. We have no position and you will have to vet for the experts we propose,” she said adding that her firm was in favour of using local and regional experts in capacity building initiatives they support.
Responding to the offer, the CRC Chairman said he was pleased to receive the offer and directed the CRC Secretariat to prepare detailed proposal for the OSIEA.
Read more ...

RAYUU KUCHEZA PICHA ZA NGONO SOUTH AFRICA

Nov 18, 2012
















































































MSANII  wa filamu na tamthilia bongo Rayuu, inadaiwa kuwa amepewa mchongo mkubwa wa pesa ndefu endapo atakubali kushiriki kwenye picha ya ngono huko Afrika Kusini ambayo inashirikisha nyota kibao wa ndani ya Afrika.

Inadaiwa kuwa msanii huyo ameonekana na watu hao baada picha zake kadhaa kuzagaa kwenye mtandao ndipo wapoliamua kumtumia ujumbe kwa njia ya mtandao, na kama atakubali basi atakula mshiko ambao hajawahi kuukamata tangu alipodhaliwa.
 

Chanzo kikubwa cha kuaminika kilichofanya upekuzi huo, kilibaini ukweli kwamba msanii huyo anachati na watu hao lakini hajawaweka wazi kama ataweza kufanya ishu hiyo ambayo itambidi asafiri.
 

Mpekuzi wetu alitumia muda wa saa kadhaa kukaa na msanii huyo na kumdadisi lakini hakupewa chochote na inadaiwa kuwa ishu hiyo ipo na watu wanamtaka kutokana na uzuri wake, pia wameona ni mtu ambaye hana aibu baada ya kuziona baadhi ya tattoo kwenye makalio yake.
 

“Inadaiwa kuwa jamaa walichokipenda kwanza ni msanii pia hana aibu kwani aliweza kuchora tatoo, lakini sijui kama msanii huyo amewajibu kwani habari nilizonazo tena nimeona kupitia macho yangu ni hizo, asa sijui ni watu wanamzingua au vipi,”
 alisema mpekuzi wetu.

Hata hivyo alipotafuwa 
Rayuu kuulizwa juu ya ishu hiyo alibaki kuchecheka na hakuna chochote alichozungumza zaidi ya kudai kuwa kuna watu wamemtumia mail ya kumtaka akacheze picha hizo kwa dau kubwa lakini hajawajibu kwani anahisi wanataka kumuharibia mipango yake ya maisha kwa madai hiyo kitu ambayo hawezi kufanya katika maisha yake.
Read more ...

AY AIBUKA KIDEDEA TUZO ZA CHANEL O

Nov 18, 2012


AY ndio msanii pekee kutoka TANZANIA (East Africa) aliyenyakuwa tuzo ya Channel O Music Video Award kwa mwaka huu 2012 katika kipengele cha MOST GIFTED AFRICAN EAST VIDEO OF THE YEAR. Video iliyochukuwa tuzo hiyo ni I DON'T WANT TO BE ALONE akiwa amewashirikisha wasanii kutoka Nairobi Kenya wanakwenda kwa jina la Sauti Sol.

HONGERA  "AY"
Read more ...

UCHAFU WA NAY WA MITEGO NA NISHA HUU HAPA

Nov 16, 2012





Picha hizi zimesambaa kwa kasi ikiwa ni siku moja tu baada ya NEY KUKANUSHA KUWA HANA UHUSIANO NA NISHA ...

Sasa Sijui Zimevujaje ? Ney wa Mitego ni mwanamuzi Ambae Siku za Karibuni Amepata umearufu kwa Kuwapa"MADONGO" Wasichana wa Bongo Movies Kuwa ni Malaya Wenye Viwango ...

Kumbe na  yeye alikuwa  anaponea huko  huko  
Read more ...

WAREMBO WAZICHAPA MPAKA WAVUANA NGUO

Nov 16, 2012
Read more ...

KOCHA WA LIVERPOOL ATOA TAMKO KUHUSIANA NA SUAREZ

Nov 16, 2012


Luis Suarez
Luis Suarez

Kocha wa livepool Brendan Rodgers amesema nyota wake Luis Suarez atasalia na klabu hiyo na kukariri kuwa hakuna klbau yoyote ambayo imeonyesha nia ya kumsajili mchezaji huyo.
Klabu ya manchester City imeripotiwa kuonyesha nia ya kumsajili Suarez, 25,. Mapema msimu huu mchezaji huyo kutoka Uruguay alisaini mkataba mpya na klabu hiyo na amekuwa katika hali nzuri ambapo amefunga jumla ya magoli 11 baada ya kucheza mechi kumi na sita.
'' Ikiwa tutampoteza Luis, basi hatutakuwa na washambulizi, na kwa sasa sina uwezo wa kumpoteza yeyote'' alisema Roggers.
Suarez alilipwa kitita cha puani milioni 22.7 wakati alipokihama klabu ya Ajax na kujiunga na klabvu ya Liverpool Januari mwaka wa 2011.
Katika msimu wake wa kwanza na Liverpool, Suarez alifunga magoli 17 baada ya kucheza mechi 39.
Hata hivyo mchezaji huyo amekumba na mizozo kadhaa akiwa England.
Suarez alipatikana na hatia ya kutumia lugha ya ubaguzi wa rangi dhidi ya mlinda lango wa Manchester United Patric Evra, na kupigwa marufuku ya kutoshiriki katika mechi nane.
Vile vile alishutumiwa kwa kutomsalimia Evra wakati wa mechi yao katika uwanja wa Old Trafford. 
Read more ...

OBAMA KUSHAURIANA NA WABUNGE WA CONGRESS

Nov 16, 2012


Rais Barack Obama, anatarajiwa kushauriana na viongozi wa bunge la Congress, kwa mara ya kwanza hii leo, tangu alipochaguliwa kwa awamu nyingine, kujaribu kuzuia kutokea kwa mzozo wa bajeti.
Ikiwa rais Obama na viongozi hao hawataafikiana lolote kabla ya mwisho wa mwaka huu, viwango vya ushuru vitaongezeka na serikali italazimika kupunguza matumizi yake, kwa mujibu wa sheria mpya itakayoanza kutekelezwa mwezi januari mwakani.
Rais Obama, tayari amesisitiza kuwa raia wa nchi hiyo wenye mapato ya juu, washurutishwe kulipa ushuru zaidi lakini chama cha republican, ambacho kina idadi kubwa ya wabunge katika bunge hilo,kimepinga vikali pendekezo hilo la raisObama.
Read more ...

RAGE ATIMUA WANACHAMA NA TAWI LA SIMBA MPIRA PESA

Nov 16, 2012


Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage akizungumza leo (Habari na picha vimehamishwa kutoka dinaismail.blogspot.com)

KAMATI ya utendaji ya klabu ya Simba imewafuta uanachama viongozi na tawi maarufu la Mpira Pesa, sambamba na kuzivunja kamati zake ndogondogo. 
Mwenyekiti wa Simba Alhaj Ismail Aden Rage, amesema kamati ya utendaji ya Simba iliyokutana juzi ilifikia maamuzi hayo baada ya kutokea kwa chokochoko katika siku za hivi karibuni. 
Alisema mwenyekiti wa tawi hilo, Masoud Awadh na Katibu wake Ali Bane walikiuka katiba ya Simba kwa kuongea hovyo na vyombo vya habari sambamba na kuitisha mkutano wa wanachama bila ya kupata ruhusa ya uongozi. 
Rage aliongeza kuwa Awadhi si mwanachama hai wa klabu hiyo kutokana na kutolipa ada ya uanachama kwa zaidi ya miaka miwili, huku barua yake aliyouandikia uongozi  kwa niaba ya Simba nayo ni kinyume na katiba kwani hana mamlaka ya kufanya hivyo. 
Tawi la Mpira Pesa chini ya Awadhi lilifanya kikao cha kushinikiza Rage na viongozi wenzake kuachia ngazi baada ya timu kufanya vibaya katika mechi za mwisho za mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom na kuishia nafasi ya tatu. 
Kama hiyo haitoshi, wanachama wa tawi hilo waliorodhesha majina zaidi ya 600 ili kutimiza akidi inayoruhusu kufanyika kwa mkutano wa dharula wa Simba. 
Hata hivyo, Rage alisema uongozi umebaini kuwa zaidi ya asilimia 90 ya wanachama waliojiorodhesha ni wafu, huku pia saini zilizowekwa ni za kughushi. 
Kuhusiana na kamati ndogondogo, Rage alisema uongozi umeona hazina msaada wowote kwa timu hivyo hivi karibuni ataunda kamati nyingine zitakazosaidia timu kupata ushindi.
Read more ...

MAPENZI YAMFANYA JANETH JACKOS KUWA MUISLAM

Nov 16, 2012

Janeth Jackson akiwa na Wissam Al ManaJaneth Jackson akiwa na Wissam Al Mana
Dada yake Michael Jackson, Janet Jackson amesilimu kuwa muislamu na atafunga ndoa ya kiislamu na mpenzi wake bilionea wa Qatar, Wissam Al Mana mwanzoni mwa mwaka ujao.
Sherehe ya kukata na shoka ambayo inatarajiwa kufanyika kwenye mji wa Doha, Qatar inatarajiwa kugharimu mamilioni ya dola ambapo bilionea huyo wa Qatar anataka kuifanya harusi yake iingie kwenye historia ya harusi bora kuliko zote duniani.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani zilizopatikana Janet na mchumba wake huyo wamepanga kutumia dola milioni 3 kwaajili ya kuwakodishia ndege za kuwaleta wageni wapatao 500 watakaohudhuria harusi hiyo.
Katika kuhakikisha kuwa wanaifanya harusi yao inakuwa ya kifahari zaidi, bilionea huyo wa Qatar amepanga kuwazawadia wageni wote watakaohudhuria sherehe hiyo saa ya kifahari aina ya Rolex yenye thamani zaidi Tsh, milioni 20. Kila mgeni atapata saa hiyo kama shukurani ya kutumia muda wake kuhudhuria harusi hiyo.
"Itakuwa ni harusi ya karne, Wissam amepanga kumwaga pesa kuifanya harusi yake na Janet iwe ya kipekee", alisema mtu mmoja wa karibu na wapenzi hao.
Janet mwenye umri wa miaka 46 alikutana na Wissam ambaye ni mdogo kwa miaka takribani 10 mnamo mwaka 2009 wakati Janet alipotembelea nchi za Mashariki ya kati na kufanya shoo maalumu kwenye nchi hizo.
Janet na Wissam walianza mapenzi yao mnamo mwaka 2010 na walivalishana pete za uchumba mwaka jana ambapo Wissam alimvalisha Janet pete ya uchumba ya almasi yenye carat 15.
"Mama yangu alitulea na kutufundisha tuamini kuwa umri ni namba tu", alisema Janet wakati alipoulizwa kuhusiana na umri wake mkubwa kulinganisha na Wissam.
Read more ...

GEORGE ENTWISTLE AJIUZULU UKURUGENZI BBC.

Nov 16, 2012

Mkurugenzi aliyejiuzulu, George Entwistle.Mkurugenzi aliyejiuzulu, George Entwistle. BBC
Mkurugenzi Mkuu wa British Broadcasting Corporation au BBC, George Entwistle amejiuzulu wadhifa huo baada ya kushutumiwa kushindwa kushughulikia vyema taarifa iliyorushwa katika kipindi cha TV cha NewsNight.
Taarifa hiyo kwa makosa ilimshutumu aliyekuwa Waziri wa Fedha wakati wa serikali ya Conservative , Lord McAlpine, kwamba alihusika katika kashfa ya kudhalilisha watoto
BBC tayari wameshaomba radhi kutokana na kurusha taarifa hiyo na kama kuonyesha kusikitishwa kwake na kitendo hicho, George Entwistle amejiuzulu. Katika speech yake aliyoisoma wakati akitangaza kujiuzulu kwake, George alisema:
“Nilipopewa kazi hii, ambapo nilikuwa na uzoefu wa miaka 23 kama mtayarishaji na kiongozi wa BBC, nilikuwa na imani kwamba uongozi wa BBC ulimchagua mtu sahihi kufanya kazi hii. Hata hivyo,matukio tofauti ambayo yamekuwa yakitokea week hizi chache yamenifanya nifikie kuona kwamba BBC inahitaji kuchagua kiongozi mpya.”
Tim Davie,mkurugenzi wa BBC Audio & Music ambaye ndio aliyekuwa anasemekana kuchaguliwa kuwa CEO wa BBC Worldwide, atashika wadhifa wa Mkurugenzi Mkuu kwa muda wakati yule wa kudumu akitafutwa. Entwistle amefanya kazi hiyo kwa muda wa miezi miwili tu.
Read more ...

HIVI NDIVYO IBRAHIMOVIC ALIVYOWACHEZESHA WAINGERZA

Nov 16, 2012
Pure delight: Zlatan Ibrahimovic celebrates his outrageous fourth goal as Sweden beat England

Opener: Zlatan Ibrahmovic fires Sweden into the lead against England before celebrating (below)

Sweden's Zlatan Ibrahimovic reacts after scoring the opening goal

Debut strike: Steven Caulker puts England in front in Sweden before he is mobbed by team-mates (below)

Bright spark: Raheem Sterling (above) impressed on his debut but Wilfried Zaha was given little time (below)

England Wilfried Zaha (L) is challenged by Sweden's Behrang Safari

Hat-trick hero: Zlatan Ibrahimovic curls home a free kick to put Sweden in front against England

Chezea ZLTAN IBRAHIMOVIC wewe..................Utaumia mwenyewe.

Read more ...

KOCHA MKUU WA SERENGETI BOYS MICHELESEN AWAHOFIA WAKONGO

Nov 16, 2012
Michelsen wa tatu kutoka kulia waliosimama akizungumza na wachezaji wa Serengeti. Kulia kwake ni wasaidizi wake, Jamhuri KIhwelo na Manyika Peter, wakati kushoto kwake ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Serengeti, Kassim Dewji, Katibu wa Kamati, Henry Tandau, Suleiman na Nyambui na Katibu wa TFF, Angetile Osiah.

Na Mahmoud Zubeiry
KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys, Mdenmark Jacob Michelsen amesema kwamba kuelekea mechi ya keshokutwa ana wasiwasi wapinzani wake, Kongo Brazzaville wana wachezaji waliozidi umri.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya mazoezi ya jioni, Michelsen alisema kwamba ameichunguza vizuri Kongo na sasa anaifahahamu vema.
Serengeti itamenyana na Kongo keshokutwa Uwanja wa Taifa, katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Tatu na ya mwisho ya kuwania kucheza Fainali za Vijana Afrika zitakazofanyika nchini Morocco mwakani.
Michelsen alisema kwamba alikwenda kushuhudia mchezo wa kwanza wa raundi iliyopita, baina ya Kongo na Zimbabwe waliotolewa na wapinzani wao hao na kujionea makali ya wapinzani wao.
Pamoja na kukiri kwamba Kongo ni timu bora na ilicheza Fainali zilizopita za Kombe la Dunia nchini Mexico mwaka jana na kutolewa raundi ya pili, Michelsen alisema bado ana wasiwasi timu hiyo ina ‘vijeba’.
“Nilipokwenda kuwaangalia wakicheza na Zimbabwe, nilikuta kikosini mwao kuna wachezaji sita wa kikosi kilichokwenda Mexico kwenye Kombe la Dunia, inanitia shaka kwa sababu hakuna mchezaji anayeweza kucheza michuano mikubwa kama ile akiwa ana umri wa miaka 15.
Mimi ni kocha wa vijana na ninajua, haiwezekani. Ucheze fainali za Kombe la Dunia za U17 una miaka 15, hakuna,”alisema Michelsen, ambaye aliwataja baadhi ya wachezaji anaowatilia shaka wamezidi umri ni Hady Binguila na Charvely Mabiat.
Pamoja na hayo, Michelsen amesema ana matumaini ya kuwatoa Kongo kutokana na maandalizi yao ya muda mrefu na pia sapoti anayoipata kutoka kwa viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Kamati maalum iliyoundwa kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri.
Amesema wamecheza mechi za kujipima nguvu 15 zikiwemo dhidi ya timu za Ligi Kuu na hawajafungwa hata moja, kitu ambacho anaamini ni kipimo cha ubora wa timu yake.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Saidia Serengeti Ishinde, Kassim Dewji alisema kwamba wanapambana kwa uwezo wao wote kuhakikisha timu hiyo inakwenda kwenye fainali za Morocco, mwakani.
Dewji aliwataka wachezaji wa timu hiyo kucheza kwa nidhamu, kujituma na kufuata maelekezo ya makocha wao, ili wapate ushindi katika mchezo wa Jumapili.
Serengeti imefanikiwa kufuzu hadi Raundi ya Tatu bila jasho, baada ya wapinzani wake wa awali katika Raundi ya Kwanza na ya Pili, Kenya na Misri kujitoa. Iwapo timu hii itafuzu, hii itakuwa mara ya pili kwa Serengeti kukata tiketi ya kucheza fainali hizo, baada ya mwaka 2005.
Hata hivyo, pamoja na kuzitoa Rwanda, Zambia na Zimbabwe, Serengeti haikwenda Gambia mwaka huo kutokana na kuondolewa kwenye michuano hiyo na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), baada ya kubainika walitumia kijana aliyezidi umri, Nurdin Bakari.
Read more ...

HAMISI KIZA KUONDOKA YANGA LEO

Nov 16, 2012

Mshambuliaji wa Yanga, Hamisi Friday Kiiza 'Diego' (pchani), anatarajiwa kuondoka leo saa 11:00 jioni mjini Dar es Salaam kwenda Kampala, Uganda kujiunga na timu yake ya taifa, The Cranes kwa ajili ya kambi ya kujiandaa na michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, Tusker Challenge itakayofanyika mwishoni mwa mwezi huu hadi mwanzoni mwa mwezi ujao mjini Kampala. Kiiza aliyewezesha Yanga kuongoza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacoim Tanzania Bara, anaondoka akiwa katika kiwango kizuri kwenda kuisaidia Uganda kutetea taji lake ililotwaa mwaka jana Dar es Salaam wakiifunga Rwanda katika fainali.
Read more ...

LADY JAY D KUTOKELEZEA NDANI YA EATV

Nov 16, 2012

LADY JAYDEE SASA NDANI YA EATV KATIKA DIARY

Mwanamuziki maarufu nchini, Lady Jaydee (kulia), akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Nyumbani Lounge, Oysterbay, Dar es Salaam kuhusu kipindi chake kipya cha Lady Jaydee Diary, kitakachokuwa kikirushwa hewani na kituo cha East African TV, maarufu kama Channel 5 kila Jumapili saa 3:00 usiku. Kushoto ni Mkuu wa vipindi EATV, Lydia Igarabuza.  


Na Princess Asia
MWANAMUZIKI mkongwe nchini, Lady Jadee ameanzisha kipindi cha TV kiitwacho Diary Ya Lady Jaydee, kitakachokuwa kikirushwa hewani na kituo cha East African TV, maarufu kama Channel 5 kila Jumapili saa 3:00 usiku.
Kama msanii, Lady Jaydee amefanikiwa na kutambulika katika kiwanda cha muziki ndani na nje ya nchi, huku akitunukiwa tunzo nyingi zaidi akiwa albamu zake tano. Pamoja na kuwa anaendelea na fani yake ya muziki, Lady Jaydee ameamua kuwafikia na kuwaburudisha wapenzi wa kazi zake kwa njia nyingine.
Lady Jaydee sasa anaanza sura mpya ya burudani kwa kuleta kipindi cha TV kiitwacho DIARY YA LADY JAYDEE, ambacho kutaonekana katika kituo cha TV cha EATV
Diary Ya Lady Jaydee itaonesha maisha na hadithi za kweli za Lady Jaydee kwa lengo la kuburudisha kwa kuonyesha mambo yate mazuri anayopitia au kuyaona Lady Jaydee kuelimisha kwa kushiriki mambo ya kijamii, kutia moyo wengine wafuate ndoto zao kwa uadilifu, kuongeza kipato kama msanii kwa kutangaza biashara mbalimbali na hatimae kudumisha ajira binafsi kwa njia ya sanaa.
Lady Jaydee anatoa shukrani kwa mashabiki kwa kuendelea kumpokea, jambo ambalo linampa nguvu zaidi ya kufanya kaza.
Pia anashukuru sana vyombo vya habari na zaidi anawashukuru EATV na washirika wake kwa kumpa nafasi ya kurusha kipndi chake kipya Diary Ya Lady Jaydee. EATV imekuwa mchango wa aina yake katika kuwakuza wasanii Tanzania.
Lady Jaydee anatoa wito kwa vyombo vya habari kuendelea kushirikiana na naye kwa kila namna, ili kukuza na kuendeleza kipaji chake na sanaa ya muziki wa Tanzania kwa ujumla wake.
Zaidi anatoa wito kwa makampuni kishiriki na kuungana nae ili waweze kumpa nguvu msanii, kutangaza biashara zao na kushawishi ajira katika fani ya muziki.
Na mwisho Lady Jaydee anawaribisha wote kusikiliza CDs zake au kuburidika na kundi lake la Machozi Band au kupata chakula ktk mgahawa wake wa kisasa Nyumbani Lounge au ukiwa umepumzika nyumbani utazame kipindi chake Diary Ya Lady Jaydee ktk EATV. 

Read more ...

MAMA MZAZI AFANYA MAPENZI NA MWANAE WA KUZAA

Nov 16, 2012

Bi. Condorada Ngonyani akiwa na mumewe/mwanaeBi. Condorada Ngonyani akiwa na mumewe/mwanae
Mama aliyefunga ndoa na mwanae wa kumzaa wa kiume baada ya mumewe ambaye ndiye baba wa mtoto huyo kufariki amesema anawashangaa wanadamu kuingilia mapenzi yao huku mwanae akiwauliza watu mnatutakia nini kwenye mapenzi yetu? akiongeza kuwa mapenzi anayopata kwa mama yake hajawahi kuyapata.

Bi Condorada Ngonyani mwenye umri wa miaka 70 ambaye alifunga ndoa na mwanae wa kiume ameibuka na kusema anawashangaa watu wanaowasimanga kwa mapenzi yao moto moto kati yake na mwanae huyo wa kiume Bw. Joseph Mapunda.
Mama huyo na mwanae waliwekwa kitimoto na wanakijiji waliohoji mapenzi hayo haramu kati ya mama na mwanae. Tukio hilo la kuwaanika hadharani mama na mwanae liliandaliwa uongozi wa serikali ya mitaa.
Mama Condorada Ngonyani (70) mkazi wa mkoani Ruvuma, aliamua kufunga ndoa na mtoto wake wa tatu wa kiume wa kumzaa na kisha kuishi naye kinyumba kama mke na mume.
Wawili hao hawajutii kitendo chao na wameonekana kuona walichofanya ni sahihi na kuwashangaa wanadamu, majirani zao na jamii kwa ujumla kuingilia mapenzi yao.
Wananchi wapatao 400, wa mkoa wa Ruvuma walijitokeza kushuhudia kimbwanga hicho wakati uongozi wa Serikali ya mtaa walipoamua kuwafuatilia na kuwahoji na kuitisha mkutano wa wanakijiji na kuwaweka hadharani.
Wananchi wa mkoa wa Ruvuma wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Maendelo ya Jamii, Jinsia na watoto, kufuatilia kwa karibu suala hilo na kuwaondoa hofu wananchi kama kuna sheria inayomruhusu mtoto na mama Mzazi kuweza kuishi kindoa.
Alipohojiwa mama huyo, Condorada Ngonyani, alisema kuwa mara tu baada ya kufariki mume wake, Mzee Mapunda, yeye aliamua kumchagua mtoto wake huyo Joseph Mapunda, ili amrithi baba yake katika kuumiliki mwili wake kama ambavyo alikuwa akifanya Baba yake mzazi, ili kuondokana na tamaa na vishawishi wa kiulimwengu.
Alisema kuwa baada ya uteuzi huo walifunga ndoa ya kimila japo kuna baadhi ya wanafamilia hawakufurahishwa na tukio ama jambo hilo, lakini yeye aliamua kufunga masikio na kuamua kuvunja amri ya sita na mtoto wake huyo wa kumzaa.
Tukio hili ni mara ya kwanza kutokea kwa mkoa wa Ruvuma na hata kwa Tanzania nzima, ambapo wakazi wa Ruvuma wamekuwa wakibaki na maswali mengi juu ya tukio hilo na kuhoji jamii sasa inaelekea wapi kwa baadhi ya Watanzania kuibomoa wenyewe mila na desturi zetu.
Kwa upande wake, Joseph Mapunda, yeye anasema kuwa upendo na mahaba anayoyapata kutoka kwa mkewe huyo ambaye ni mama yake mzazi, hajawahi kuupata kokote na kusema kuwa wanapendana sana na wanaheshimiana kama mke na mume.
Josepha amehoji kulikoni wanadam kuwafuatilia katika mapenzi yao na kusema kuwa "hawa watu wanaotufuatilia hadi leo hii kutuweka hadharani namna hii, wanataka nini kwetu?".
Wananchi hao waliofurika kwa Mganga wa Jadi Flora Ndembo, wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma, wameiomba Serikali kuingilia kati suala hilo na kuchukua hatua kisheria ili iwe fundisho kwa Watanzania wengine wenye akili kama hizo za kuharibu mila na desturi za kitanzania kirahisi kama hivyo
Read more ...

MTOTO ALIYECHOMWA MOTO NA KULAZIMISHWA KULA KINYESI SASA AKATWA MKONO

Nov 16, 2012



Huyu ndio mtoto anayefahamika kwa jina la Aneth ambaye alifanyiwa ukatili na Mama yake Mdogo kwa kuchomwa moto.



Bahati Rukangara.

Tukio hili limetokea eneo la Majengo Jijini Mbeya ambapo Bahati Rukangara Mama mdogo  wa Aneth inasemekana alikuwa anampa manyanyaso na mateso mtoto huyu mdogo ambaye kwa hali ya kawaida hana uwezo wa kutetea katika mateso hayo, cha ajabu mtoto huyu baada ya kuchomwa moto amekuwa akifungiwa ndani na kulazimishwa kula kinyesi cha mama yake huyo mdogo.

Read more ...

JOSEPH OWINO AHUSISHWA KURUDI TENA SIMBA

Nov 16, 2012


Mwandishi wa habari za michezo Shaffih Dauda ameripoti kwamba zoezi la klabu bingwa ya Tanzania bara Simba kupata mbadala wa beki wake aliyetimkia Yanga, Kelvin Yondani linaendelea baada ya Lino Musombo kutemwa na kusajiliwa kwa Keita na Ocheing ambao wameonekana kuhangaika kuziba pengo la Yondani, sasa klabu hiyo ya Simba inasemekana ipo katika harakati za kumrudisha mmoja wa mabeki wao bora katika kipindi cha miaka 10 iliyopita mganda Joseph Owino.
Simba ambao walianza ligi vizuri na kuongoza ligi kwa muda mrefu kabla ya kupoteza muelekeo mwishoni mwa raundi ya kwanza ya msimu wa VPL sasa katika kujaribu kuimarisha safu ya ulinzi ya timu hiyo ambayo imeonekana kuyumba sana msimu huu, uongozi wa Simba umeona bora ufanye mpango wa kumrudisha kundini Owino ambaye amesajiliwa Azam lakini amekuwa akikosa namba ya kudumu baada ya kurudi kutoka kwenye majeruhi yaliyomuweka nje kwa muda mrefu.
Taarifa ambazo hazijathibitishwa ni kwamba Simba tayari wapo kwenye mazungumzo na Azam ili kuweza kuona uwezekano wa kumsaini Owino  ambae aliondoka Simba baada ya kupata majeraha ya goti ambayo yalimuweka nje kwa muda mrefu, na Azam wakamsajili akiwa mgonjwa wakamtibu lakini baada ya kupona amekuwa na urafiki mzuri na benchi la Chamazi.
Read more ...

TAMKO JUU YA VURUGU ZA JANA ZILIZOSABABISHA CHINGA KUUAWA

Nov 16, 2012

Sikiliza kilichosemwa na Mstahiki meya wa jiji la Mwanza (Nyamagana) Stanslaus Mabula (wa pili kutoka kulia) kwa kubofya Play..
Read more ...