Pages

WANAFUNZI WA BUGANDO WATEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA NYASAKA MWANZA

Jun 30, 2012
 Hii ni sehem ya watoto wakati ambapo walikuwa wakiskiliza maneno kutoka kwa mwenyekiti wa msafara
                                       Kushoto ni Nuri akitake pics za ukumbusho

                                           Zaoro naye kama mwandamizi katika jopo hilo

                                   Godfrey kahamba akitake responsibility za kugawa kilichopo kwa watoto

                             Tino akimsaidia godfrey kugawa kile walichokuwa nacho kwa yatima hao




Bugando blog kwa niaba ya wanachuo wa bugando tunatoa shukraniu za dhati kwa wale wote waliofanikisha tukio hili muhimu na pia kuwapongeza wale wote waliochangia katika ile kidogo walichonacho
Mungu awaongezee kutoka pale mlipo toa .
                               AHSATENI SANA
Read more ...

Leo Katika Historia Peugeot 203

Jun 30, 2012



  Mwenyekiti, kuna mjumbe ameomba  msaidizi wako  Meshack apige picha ya gari aina ya Peugeot 203 (ingawa yeye amekosea na kuandika Peugeot 403) na aitundike humu.  Nilijua alimaanisha Peugeot 203 kwa jinsi alivyoelezea gari hilo lilivyo.  Hata hivyo, sidhani kama Meshack atafanikiwa kupata picha ya gari hili Bongo hata kama anajua likoje.  Magari haya yalikuwa mengi Tanzania miaka ya 1960, 70 mpaka 80, lakini sasa yametoweka.  Niliona Peugeot 203 mara ya mwisho mwaka 1986 Moshi ambako zilikuwa zinafanya kazi kama teksi pale stendi kuu.  Hii ni picha ya mtandaoni. 
Mdau :
Read more ...

Jacob Zuma To Buy Presidential Jet Despite South Africa's Poverty'

Jun 30, 2012


Jacob Zuma is in talks to buy a £165m presidential jet, it was reported, just days after the South African president warned of growing frustration among the country's poorest over the government's failure to improve their lives.


The customised Boeing 777 plane seats 300 people and would cost $150m to buy and an additional $80m to be adapted to Mr Zuma's specifications.




The Department of Defence, which oversees VIP transport, is reportedly considering spending an additional $28m on a second private plane for Kgalema Motlanthe, the deputy president.

Defence Secretary Sam Makhudu Guluybe was on Friday visiting the United States to finalise the sale with Boeing, according to the Johannesburg Star newspaper.

The newspaper said it had documents which showed the defence department had negotiated a significant reduction on the jet's original price of $305m after a deal between Boeing and another buyer fell through.

The current presidential jet, known as Inkwazi which means "fish eagle" in Mr Zuma's mother tongue Zulu, was out of service for much of last year for upgrades and maintenance. 

Read more ...

Dawa Mpya Ya Ukimwi

Jun 30, 2012
                          Baadhi ya dawa za kukabiliana na makali ya Ukimwi


Huenda wagonjwa wa Ukimwi wakanufaika na dawa mpya ambayo itawawezesha kutumia tembe moja kwa siku. Hii ni kwa mujibu wa utafiti mpya nchini Marekani.

Jarida la Afya Lancet limesema tembe hiyo inajumlisha dawa zote nne zinazokabiliana na makali ya ukimwi na kwamba ni salama.Utafiti unasema hii itawarahisishia wagonjwa katika kuhakikisha wanafuata maagizo ya madaktari wao.

Ukimwi hauna tiba lakini watafiti wameweza kutoa dawa za kukabiliana na maradhi nyemela.

Watafiti pamoja na kampuni za dawa wamechanganya dawa nne na kutengeneza tembe moja ili kurahisisha utumizi wa dawa hiyo miongoni mwa wagonjwa.

Tembe inayofanyiwa majaribio na ambayo imechanganywa dawa nne inauwezo wa kudhibiti virusi vya HIV kuongezeka mwilini.

Paul Sax mtafiti mkuum katika Hospitali ya Wanawake ya Brigham huko Boston,Massachussetts ambaye pia ni mwanazuo wa ziada wa taasisi ya afya ya Harvard ameelezea umuhimu wa tembe hii kwa kuimarisha afya ya wagonjwa.

Dk. Sax ameongoza utafiti huu ambapo pia wamefanyia majaribio tembe hii kwa wagonjwa 700 na kusema inafanya kazi, japo kulitokea matatizo ya figo miongoni mwa waliotumia.

Licha ya mafanikio ya sasa watafiti wanasema raia wengi hawafahamu hali zao ambapo wameendelea kuishi na maambukizi bila kujua.
Chanzo: bbc swahili.   http://www.bbc.co.uk/swahili/habari
Read more ...

JK Na Form Six Wa Marian Girls

Jun 30, 2012







Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipozi na baadhi ya wanafunzi wa kidato cha sita wa Marian Girls Secondary school kwenye kwenye sherehe za "Holy Ghost Congregation 20th General Chapter katika hosteli ya Misheni ya Kikatoliki ya Stella Maris aliyoizindua jana  Juni 29. 2012 huko Bagamoyo, Mkoa wa Pwani. Picha: IKULU
Read more ...

MSAFARA WA RAIS WAZUIWA KWA KUWEKWA MAWE BARABARANI TEGETA, WALINZI 42, WANANCHI 56 WASHIKILIWA POLISI

Jun 30, 2012
Read more ...

MNAOFATILIA FASHION, RIHANNA NA RITA ORA HAWA HAPA.

Jun 29, 2012
Add caption




Read more ...
Jun 29, 2012
Read more ...

MADAKTARI 72 WAFUKUZWA KAZI HOSPITALI YA RUFAA YA MBEYA

Jun 29, 2012


Read more ...

BABA WA ULIMBOKA AMWAGA MACHOZI

Jun 29, 2012

 BABA wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, mzee Steven Mwaitenda
 Baba wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, mzee Steven Mwaitenda akilia na kufarijiwa
 Usu Mallya akilia baada ya kushuhudia mzee Steven Mwaitenda akibubujikwa na machozi mbele yao
 Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Usu Mallya (kushoto) akiwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Lilian Liundi walipomtembelea Dk. Ulimboka kumfariji jana
 Mzazi akimlilia mwanaye Dk. Ulimboka kwa uchungu MOI
 Baadhi ya wanaharakati anuai wakiwa na maua walipomtembelea Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Ulimboka kumfariji jana
 Baadhi ya wanaharakati wakiwa na nyoso za hudhuni baada ya kilio cha baba wa Dk. Ulimboka jana
Na Joachim Mushi, Thehabari.com
BABA wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, mzee Steven Mwaitenda amejikuta akiangua kilio kwa uchungu mbele ya wanaharakati ambao walimtembelea mwanae, Dk. Steven Ulimboka kumpa pole kufuatia tukio la kutekwa na kujeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana.

Hali hiyo ilitokea jana jioni katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), ambapo wanaharakati kutoka taasisi na asasi mbalimbali za utetezi wa haki za binadamu walifika kwa lengo la kumpa pole Dk. Ulimboka kufuatia kitendo kilichomfika.

Mzee Mwaitenda alijikuta akibubujikwa na machozi na kushindwa kuendelea kuzungumza alipokuwa akitoa shukrani kwa wanaharakati hao, kwa niaba ya mwanaye ambaye wanaharakati hao walishindwa kumuona wote kutokana na hali yake ilivyo sasa.

“Niseme wazi nimefarijika sana kwa ujio wenu kumwona mwanangu dhidi ya mambo ya kikatili aliyofanyiwa akitetea haki za wengine…,” alisema mzee Mwaitenda kabla ya kushindwa kuendelea na kuangua kilio mbele ya wanaharakati.

Baada ya tukio hilo baadhi ya wanaharakati walimshika wakishirikiana na wanafamilia ya mzee Mwaitenda na kumbebeleza kisha kumtoa mbele ya mkusanyiko huo wa wanaharakati na kumrudisha wodini huku wakimfariji.

Wakizungumza mara baada ya tukio hilo wanaharakati wameelezea kusikitishwa na vitendo vinavyoendelea MOI eneo ambalo amelazwa kiongozi huyo wa madaktari ambavyo vimeendelea kutishia usalama wa Dk. Ulimboka.

Akifafanua zaidi mwakilishi wa wanaharakati hao, Markos Albania alisema taarifa walizozipata usiku wa juzi kuna wagonjwa ‘feki’ ambao walijitokeza MOI huku wakitaka kulazwa wodi ya Wagonjwa Mahututi (ICU) alipolazwa Dk. Ulimboka lakini baadaye waligoma kuingizwa wodini.

“Wapo wagonjwa ambao waliletwa na kutaka kupelekwa ICU moja kwa moja…kuna watu wanakuja usiku wa manane wakitaka kumtembelea Dk. Ulimboka…matendo yanayoendelea kutokea ukilinganisha na kauli za Serikali zilizotolewa bungeni yanatishia usalama na uhai wa mgonjwa,” alisema Albania.

Aidha amesema kitendo cha vyombo vya usalama kuendelea kumuhoji Dk. Ulimboka akiwa hoi hospitalini si vya kiungwana kwani tayari muhusika amewataja hadi kwa majina watu ambao anawashuku lakini hadi sasa hakuna aliyechukuliwa hatua yoyote.

Pamoja na hayo wanaharakati hao wameitaka Serikali kuunda tume huru mchanganyiko na raia ambayo itachunguza kiundani suala hilo, kwani hawana imani na Jeshi la Polisi ambalo limedai kuunda timu ambayo inachunguza kwa kina suala hilo.

Dk. Ulimboka ambaye ni kiongozi wa madaktari ambao wanaendelea na mgomo wan chi nzima kuishinikiza Serikali kutekeleza madai yao alitekwa juzi na watu wasiojulikana na kupigwa na kuteswa kikatili kabla ya kutelekezwa katika msitu wa Mabwepande.
*Habari hii imeandaliwa na Mtandao wa Thehabari.com (www.thehabari.com)
Read more ...

TAMSA BUGANDO WAFANYA SEMINA YAO IKIWAHUSISHA NA WAGENI KUTOKA NJE

Jun 28, 2012

Hapo chini kuna video ikionesha jinsi kikao hicho kilivyokuwa na wadau walio kuwepo

Read more ...

Kamamnda Kova Azungumzia Tukio La Kutekwa Dr. Ulimboka...!

Jun 27, 2012



Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la utekaji nyara na kujeruhi lililompata kiongozi mgomo wa Madaktari Steven Ulimboka anayedaiwa kutekwa na watu watano wakati akipata kinwaji katika klabu ya Leaders Kiondoni jijini Dar es salaam.

Kamanda Kova amesema Ulimboka aliokotwa na msamaria mwema ambaye hakutaka kumtaja jina lake kiusalama na kutoharibu upelelezo kuwa msamaria mwema huyo alimuokota Ulimboka katika msitu wa Mabwepande na kutoa taarifa kituo cha polisi cha Bunju, ambapo polisi aliyekuwa zamu alichukua maelezo yake na baadae Steven Ulimboka kuletwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Kamanda Kova amesema jeshi la Polisi Kanda Maalum limeunda jopo maalum kwa ajili ya uchunguzi na upelelezi wa tukio hilo la utekaji nyara, kwani ni tukio la kwanza kutoke nchini, ameongeza kwamba wahusika wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo wachukuliwa hatua za kisheria na sheria itafuata mkondo wake ili kukomesha matukio mengine kama hayo

 

Waandishi wa habari waimsikilza kamanda Suleiman Kova katika kituo kikuu cha polisi Kati jijini Dar es salaam leo mchana.
Read more ...

GRAND MALT KUDHAMINI TAMASHA LA FILAMU TANZANIA 2012

Jun 27, 2012

 Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt,Consolata Adam (katikati) akizungumza mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es salaam leo kuhusiana na tamasha hilo la Filamu za Kitanzania lifahamikalo kwa jina la Grand Malt Film Festval Tanzania litakalofanyika siku ya Jumamosi Juni 30 katika Viwanja vya Wazi vya Tangamano,Jijini Tanga.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Sofia Productions,Mussa Kisoky akisisitiza jambo wakati akitoa taarifa ya maandalizi ya Tamasha hilo la Grand Malt Film Festval Tanzania linalotarajiwa kufanyika jijini Tanga jumamosi hii.Kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya bia Tanzania (TBL), Fimbo Butallah na kulia ni Mmoja wa Wacheza Filamu hizo watakaoonyesha kazi zao katika Tamasha hilo,Vicent Kigosi a.k.a Ray.
Meneja Masoko wa Kampuni ya bia Tanzania (TBL), Fimbo Butallah (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es salaam leo kuhusiana na tamasha la Filamu za Kitanzania lifahamikalo kwa jina la Grand Malt Film Festval Tanzania ambalo hufanyika Mkoani Tanga kila mwaka.Tamasha litafanyika Jumamosi Juni 30 katika Viwanja vya Wazi vya Tangamano,Jijini humo.Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Sofia Productions,Mussa Kisoky na kulia ni Mmoja wa Wacheza Filamu hizo watakaoonyesha kazi zao katika Tamasha hilo,Vicent Kigosi a.k.a Ray

Kinywaji cha Grand Malt leo kimetangaza kuendelea kudhamini tamasha maarufu la Filamu hapa Tanzania lijulikanalo kama “Tanzania Open Film Festival” (TOFF) ambalo hufanyika jijini Tanga kila mwaka.

Akizungumza katika uzinduzi wa tamasha la mwaka huu, meneja wa kinywaji cha Grand Malt Bi. Consolata Adam alisema; Kinywaji cha Grand Malt ndiye mdhamini mkuu wa Tamasha la Filamu Tanzania.

Tamasha hili limekuwa likifanyika katika Jiji la Tanga na limeonesha kupendwa sana na wakazi wa Jiji la Tanga. Kwa mwaka huu wa 2012, tamasha hili linaanza tarehe 30 June hadi tarehe 6 Julai.

Kwa kipindi chote hiki, Grand Malt imejipanga kuhakikisha kuwa tunafanya uhamasishaji wa kutosha katika jiji la Tanga, ili kuwawezesha wakazi wa Tanga na maeneo ya jirani kuweza kuhudhuria tamasha hili.

Tunawakaribisha watu wote wenye mapenzi na filamu zetu za kitanzania kufika na kushuhudia Tamasha hili ambalo mwaka huu limeboreshwa zaidi.

Nae Meneja Masoko wa TBL, Bw. Fimbo Butallah alisema; Kama mtakumbuka, Mwaka jana Grand Malt iliamua kushirikiana na Kampuni ya Sophia Records, ambao ndio waandaaji na waasisi wa Tamasha hili.

Ushirikiano wetu ulikuwa mzuri, kwani tulijifunza mambo mengi juu ya Tamasha hili, lakini kikubwa zaidi tulijionea jinsi wananchi wanavyozipenda sana filamu za Kitanzania almaarufu kama “Bongo Movies” na jinsi walivyo na kiu ya kuwaona wasanii wa Bongo Movies ana kwa ana.

Kufuatia umuhimu huo hatua ya kwanza tuliyochukua ni kusaini mkataba wa udhamini wa miaka mitatu na kampuni ya Sophia Records, na hatua nyingine itakuwa kuweka utaratibu wa kulipeleka Tamasha hili katika mikoa mingine ya Tanzania na hatimaye kuliweka katika hadhi ya kimataifa.

 Grand Malt inawaahidi wakazi wa Tanga na Watanzania wote kwa ujumla, kuwa Tamasha hili litakuwa na mvuto wa aina yake na hatimae kutumika kulitangaza Taifa letu kupitia tasnia hii ya filamu ambayo kwa sasa inakua kwa kasi kubwa.

Nae Mkurugenzi wa Sophia Records, waandaaji na waasisi wa Tamasha hili, Bw. Musa Kissoky alisema; kwanza kabisa tunatoa shukurani za dhati kwa Grand Malt kwa kukubali kushirikiana nasi katika kuboresha na kuendeleza Tamasha hili.

Sophia Records iliona kiu ya watanzania kupata fursa ya kuona filamu za wasanii wetu hasa katika jukwaa kubwa la wazi, lakini pia kukutana na wasanii wenyewe na kubadilisha na nao mawazo juu ya tasnia hii, hivyo tukaanzisha Tamasha hili ambalo sasa linajulikana kama “Grand Malt Tanzania Open Film Festival”.

Tunawashukuru saana wasanii wa Bongo Movies, hususan uongozi wao, kwa ushirikiana mkubwa wanaotupatia katika kuhakikisha mafanikio ya matamasha haya.

Akizungumzia maandalizi ya Tamasha la mwaka huu linaloanza Juni 30, alisema; maandalizi yote yapo tayari, kama ilivyo kawaida, Tamasha litafanyika katika viwanja vya Tangamano na litakuwa likianza asubuhi hadi usiku.

Tumeandaa burudani nyingi zitakazosindikiza maonesho haya ya Filamu kwa siku zote saba, na hakutakuwa na kiingilio, hivyo watu wote wanakaribishwa kuja kujionea Filamu zetu na kukutana na wasanii waliobobea katika tasnia hii ili wabadilishane mawazo.
Read more ...

DK ULIMBOKA WA MGOMO WA MADAKTARI APIGWA NA KUNDI LA WATU, ALAZWA MOI

Jun 27, 2012




Dokta Steven Ulimboka ambaye ni Kiongozi wa Jumuia ya Madaktari  Tanzania akiwa ameumia vibaya kutokana na majeraha ya kipigo alichopia na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo.Tetesi zinasema MUHAS wamefunga chuo kwa muda na Bugando bado hakijaeleweka




                        na huu ni ujumbe aliotumiwa zito kuhusu hali ya ulimboka


‘Kaka Zitto,hali ya Dr.Ulimboka yuko unconscious,multiple ribs fracture na kwenye mikono pia amevunjika pamoja na taya,yuko icu wanamstabilise kwanza kwasababu hapumui vizuri,the situation here is really bad,I agree with you this is outright outrageous’

Nimechukizwa sana na habari za kutekwa, kupigwa na kuumizwa vibaya kwa Dr Ulimboka, Kiongozi wa Madaktari Nchini. Mambo kama haya tumezoea kuyasikia kwenye nchi za kidikteta na kuongozwa kiimla ambapo watawala badala ya kutumia njia ya kidemokrasia na kisheria kushughulikia wanaoamini ni maadui zao katika utawala, hutumia wahuni katika Taasisi za usalama kuteka raia, kuwatesa, kuwafunga na hata kuwaua.

Sitaki kuamini kwamba Tanzania imefikia huko. Nimezungumza na baadhi ya madaktari walio karibu na Dokta Ulimboka na kujulishwa kwamba majeruhi huyu wa vitendo vya hovyo kabisa kutokea hapa nchini alikamatwa jana usiku mnamo saa sita na watu wasiojulikana na kupelekwa katika msitu wa MagwePande na kujeruhiwa vibaya. Habari hizi bado hazijathibitishwa na vyanzo huru lakini ndio zilizopo hadi hivi sasa.

Serikali kama mlinzi wa usalama kwa raia inaWAJIBU kueleza tena kwa haraka ni nini kimetokea kwa kijana huyu msomi na kiongozi wa wataalamu wenzake. Serikali INAWAJIBIKA kueleza katika nyakati kama hizi ambapo kuna mgogoro kati yake na madaktari imekuwa wapi kuhakikisha usalama wa viongozi wa madaktari ili kuepusha watu wanaoitwa ‘agente provocateure‘ kuweza kuhatarisha hali ya amani ya nchi na hata kupelekea kuweka hali ya vitisho kwa madaktari wetu.

Serikali INAWAJIBIKA kueleza kama sasa imeamua kutumia njia za kihuni kumaliza matatizo na wananchi wake.

Nimemuomba Waziri kivuli wa Afya wa CHADEMA kufuatilia suala hili kwa kwa karibu sana ili kuhakikisha kwamba ukweli wote na ukweli mtupu unafahamika. Kamwe hatuwezi kuacha Mtanzania yeyote aonewe, anyanyaswe au akandamizwe eti kwa sababu ya kudai haki yake na za wenzake. ‘An injury to one, injuries to all’

Naomba madaktari wamwangalie kwa karibu daktari mwenzao ili aweze kupata nafuu. Ulinzi uimarishwe ili kuhakikisha usalama wake.
Read more ...

walicho kiandika mwananchi kuhusu mgomo wa madaktari

Jun 26, 2012
Mwananchi
click hilo neno kusoma habari kabili
Read more ...

MGOMO WA MADAKITARI MUHIMBILI BADO TETE

Jun 26, 2012

Aliekuwa Mpiga picha wa magazeti ya Habari leo Athumani Hamisi akitoka katika Taasisi ya Mifupa MOI Muhimbili ambaye alifika kwa ajili ya kupatiwa huduma ambayo huipata kila jumanne na amekosa huduma hiyo na kurudi baada ya madakitari kuendelea na mgomo

Aliekuwa Mpiga picha wa magazeti ya Habari leo Athumani Hamisi akitoka katika Taasisi ya Mifupa MOI Muhimbili ambaye alifika kwa ajili ya kupatiwa huduma ambayo huipata kila jumanne na amekosa huduma hiyo na kurudi baada ya madakitari kuendelea na mgomo
Read more ...

TAMASHA LA WAZI LA AIRTEL JIUNGE NA SUPA5 LAITIKISA JIJI LA MWANZA

Jun 26, 2012


 Meneja Mahusiano wa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel-Tanzania,Jackson Mmbando akimkabidhi Jamila Juma simu ya mkononi aina ya Sumsung,baada kuibuka mshindi kwa kuichammbua vyema huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa5.
 Pichani shoto wakazi wa Mwanza, Jamila Juma na  Sandra Mwashitete wakipewa maelekezo mafupi namna ya kutumia mtandao wa Airtel pamoja na huduma zake mbalimbali, mara baada ya kujishindia simu aina ya Sumsung,wakati kampuni ya Airtel ilipokuwa ikizindua huduma yake mpya ya Airtel Jiunge na Supa5,uliofanyika jana kwenye viwanja vya Furahisha,jijini Mwanza.
 Ni Mzee wa Makamo hivi lakini alionesha umahiri wake mkubwa wa kuwachangamsha vilivyo sehemu ya wakazi wa jiji la Mwanza.Anaitwa Mzee Salum akikamua jukwaani jana kwenye viwanja vya Furahisha jijini Mwanza,wakati wa uzinduzi  wa huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa5.

 
 Sehemu ya wakazi wa jiji la Mwanza waliojitokeza kwa wingi jana jioni kwenye uzinduzi ramsi wa huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa5,uliofanyika kwenye viwanja vya Furahisha jijini humo.
 Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya na kiongozi wa kundi la Wanaume Halisi kutoka Temeke,jijini Dar,akiwa sambamba na msanii mwenzake (hayupo pichani) aitwaye Kr-Mulla wakilishambulia jukwa huku shangwe kubwa ikilipuka kutoka kwa sehemu kubwa ya wakazi wa jiji la Mwanza waliojitokeza jana wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa5.
 Baadhi ya wasanii wa kikundi cha Kinonko chenye maskani yake pale Kinondoni,kikionesha umahiri wake wa kucheza mbele ya umati mkubwa wa wakazi wa jiji la Mwanza waliojitokeza kwenye viwanja vya Furahisha wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa5.
.Baadhi ya Wakazi wa jiji la Mwanza wakiendelea kuhamia Airtel na kupata huduma mbalimbali za kampuni hiyo,jana jioni kwenye  viwanja vya Furahisha wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa5.
Read more ...

PICHA ZNINAZOONESHA AJALI ALIYOIPATA 50CENTS JANA USIKU

Jun 26, 2012
  1

  
                                                            2
Rapper 50 CENT amepata ajali mbaya ya gari jana usiku huko Queens New York baada ya gari lake kugongwa na lori ambapo yeye na dereva wake walikimbizwa hospitali ya karibu kutibiwa, hakuna taarifa nyingine za ziada lakini millardayo.com iko karibu na inafatilia kikitokea chochote kipya utakifahamu kupitia hapa hapa.
                                        CHANZO
                          www.millardayo.com
Read more ...