Mwenyekiti, kuna mjumbe ameomba msaidizi wako Meshack apige picha ya gari aina ya Peugeot 203 (ingawa yeye amekosea na kuandika Peugeot 403) na aitundike humu. Nilijua alimaanisha Peugeot 203 kwa jinsi alivyoelezea gari hilo lilivyo. Hata hivyo, sidhani kama Meshack atafanikiwa kupata picha ya gari hili Bongo hata kama anajua likoje. Magari haya yalikuwa mengi Tanzania miaka ya 1960, 70 mpaka 80, lakini sasa yametoweka. Niliona Peugeot 203 mara ya mwisho mwaka 1986 Moshi ambako zilikuwa zinafanya kazi kama teksi pale stendi kuu. Hii ni picha ya mtandaoni.
Mdau :