AJALI MBAYA YATOKEA MBEZI
Ajali hii imetokea maeneo ya Mbezi Afrikana jijini Dar es Salaam leo ambapo
Lori hili lenye nambari za usajili T 545 BPU lililokuwa likimwaga mchanga na
kujikuta likipiga mweleka na kuangukia Gari ndogo aina ya Toyota Rav4 yenye
nambari za Usajili T839 BSL iliyokuwa imepaki katika eneo hilo. Hakuna mtu
aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa katika ajali hiyo.