Lyndell Locke, huyu jamaa ndiyo alikuwa mpenzi wa kwanza wa Beyonce. Unaambiwa jamaa alikuwa akimsindikiza Beyonce kwenye mazoezi ya kuimba na kucheza akiwa ndiyo yupo kwenye harakati za kuwa star. Beyonce anasisitiza kwamba pia hajawahi kuwa na uhusiano wa chumbani na huyu jamaa.
Cam’Ron, msanii maarufu aliyewahi kutamba na ngoma Oh Boy, alisema kwamba kwasababu walifanya ngoma pamoja na Beyonce na katika mambo yao mengine huko nyuma ya pazia. Beyonce alimpa nafasi ya ku-share chumba kimoja na yeye lakini watu wengi hawaya amini maneno ya Cam’Ron.
Justin Timberlake, moja ya marafiki wakubwa wa mume wa Beyonce. Kulikuwa na uvumi kwamba wawili hawa Justin na Beyonce wali-spend usiku mmoja kwenye club na baadaye kufanya vitu vingi. Japokuwa hii habari haikuwa na uthibitisho wowote lakini ilivuma kwa wakati wake.
Sean Paul ; Huyu jamaa ndiyo anasadikiwa sana kuwa na mahusiano ya siri na Beyonce. Kuna muda walikuwa karibu sana na kufanya mambo mengi pamoja hadi baadaye ketengeneza ngoma ya Baby Boy ya Beyonce pamoja. Ukaribu upo hadi leo na unaweza kuona kwamba hadi marafiki wa Beyonce ni marafiki wa Sean Paul, mtu kama Kerry Rowland ambaye ameipendezesha ngoma ya how deep ya Sean Paul. Sean Paul mwenyewe aliwahi kuulizwa kuhusu hii ishu na alikataa katakata.
Marquise Huston, huyu jamaa aliwahi kuja Tanzania kipindi flani akiwa na mdogo wake Omarion. Jamaa aliwahi kushikilia bango kwamba aliwahi kuwa na uhusiano na Beyonce akiwa na miaka 17. Baada ya muda kidogo Marquise alipiga kimya mwenyewe.
Wyclef Jean, jamaa huyu ambaye pia ni producer aliwasaidia sana wakina Beyonce enzi za Destiny Child kwenye ngoma yao ya kwanza. Katika hizo harakati unaambiwa mtu mzima hakuweka juhudi kwenye kuandaa ngoma peke yake bali pia juhudi ziliwekwa kwenye mtego wa kumnasa Beyonce.