Pages

"NAOLEWA KWA AJILI YA STAREHE ZA MAPENZI NA SI KWA AJILI YA KUZAA"...NATASHA WA BONGO MOVIE

Jul 12, 2013


MWIGIZAJI mkongwe wa maigizo na filamu Bongo, Suzan Lewis ‘Natasha’ ambaye pia ni mtangazaji wa Radio Times FM, anayetarajia kufunga ndoa kesho, amefunguka kuwa anaoelewa kwa ajili ya kustarehe na siyo kwenda kuzaa kama wengine wanavyofanya.

Akizungumza na mwandishi wetu, Natasha alisema kuwa katika maisha yake hakuna kitu anachokichukia kama kubeba mimba na umri alionao ndiyo kabisa hawezi kufanya hivyo bali atalea wajukuu tu.