Pages

Shemeji yake Kim Kardashian ambaye ni star wa NBA amfanyia kali paparazi

Jul 11, 2013
Kama umewahi kuangalia show ya Keeping up with Kardashian basi utakuwa umewahi kuomuona Lamar Odom  mume wa Khloe Kardashian ambaye ni mdogo wake Kim Kardashian. Hivi karibuni jamaa huyu ambaye pia ni mkali wa NBA, amepata kashfa za kuwa na mahusiano nje ya ndoa na kuandamwa na mitandao kadhaa ya udaku. Lamar akiwa mtaani na mizunguko yake akafatwa na paparazi akiwa na camera zake na kuanza kumuuliza maswali ya kuhusu yeye ku-cheat kwenye ndoa yake. Kilichotokea hapo ni balaa kubwa ambalo Lamar alimfanyia paparazi huyo. Cheki hizi picha pamoja na video jinsi mambo yalivyokuwa.