Pages

BIBI CHEKA NA KITU KIPYA

Apr 21, 2012

BIBI CHEKA AJA NA RUDI BABA FELLA


BAADA ya kutamba na singo yake ‘Ni Wewe’ aliomshirikisha Mh.Temba
msanii kutoka kundi la Mkubwa na Wanawe anayekwenda kwa jina la Bibi
Cheka anatarajiwa kuachia singo yake ya pili inayokwenda kwa jina la
‘Rudi Baba Fella’.
Akizungumza na mwandishi wa habari hivi karibuni, Bibi Cheka alisema
kuwa singo hiyo aliyoitayarisha katika studio za Poteza inatarajiwa
kuwashika mashabiki kwani ndani yake amechana ‘kurap’ipasavyo.
Alisema pamoja na singo hiyo kwa sasa anaendelea na kazi ya
kutayarisha albamu yake mpya ambayo inatarajiwa kukamilika wakati
wowote na ndipo ataanza harakazi za kuingiza sokoni.
“ni matarajio yangu mashabiki wataupokea tena wimbo wangu huo mpya
ntakaoutoa kama ilivyokuwa kwa ule wa kwanza ambao kwa kiasi kikubwa
umeweza kuniweka juu katika medani ya muziki wa bongo fleva,”alisema
Bibi Cheka.