Kibaka aliyetaka kumpora denti wa kidato cha sita shilingi milioni tatu akiwa hoi baada ya kupokea kichapo kutoka kwa wananchi eneo la Area Five jirani na kituo cha Oil Com kilichopo maeneo ya Nane Nane mkoani Morogoro leo.
Askari wa pikipiki maarufu kama 'Voda Fasta' walifika eneo la tukio na kumuokoa kibaka huyo asiendelee kupokea kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali.
Denti aliyefanikiwa kumkabili kibaka huyo, Marry Gasto (22) akiwa na begi lililokuwa na fedha hizo alizotumiwa na baba yake kama ada ya shule.