Pages

KAMA ULIMISS MAHAFALI YA CBE MWANZA MPANGO MZIMA ULIKUWA HIVI

Dec 8, 2012
Chuo cha Elimu ya Biashara Kampasi ya Mwanza leo kitawatunuku wahitimu katika nyanja mbalimbali waliomaliza na wanaoendelea na mafunzo chuoni hapo. Chuo hiki cha CBE kampasi ya Mwanza  kilianzishwa mwaka 2007 na haya ni mahafali ya tano kufanyika katika kampasi hii. CBE kampasi ya Mwanza ni chuo cha tatu kuanzishwa kikitanguliwa na Dodoma na cha Kwanza kabisa ni kampasi kuu ya Dar es Salaam kilichoanzishwa mwaka 1965 chini ya sheria ya Tanzania No. 31. Tayari mahafali mengine ya chuo hiki yalishafanyika katika kampasi ya Dar es Salaam na Dodoma.

Wadau na wafanyakazi wa CBE MWanza wakihakikisha mambo yanakaa sawa kabla ya sherehe hizo za mahafali. pichani ni Angel Mchaki (kushoto), John Mwambigija (katikati) na Stella Nyenza .
Viti na mahema vipo tayari vikisubiri wakaaji
Jukwaa katika maandalizi
Kama kawaida kipindi hiki huwa cha neema kwa wauza mashahada na maua kwa ajili ya kuwapongeza wahitimu (hapa samaki)
Na hapa ni mbele ya mkataba ya mkoa
 Mahafali haya yanatarajiwa kuanza mnamo saa sita mchana. Nyote mnakaribishwa

BUGANDO BLOG  itakuletea habari kamili ya picha na matukio ya tukio hili. stay tuned