Pages

MKE AMWANGUSHIA MUME KICHAPO KIKALI MARA BAADA YA KUMFUMA NA 'KIMADA'

Dec 10, 2012


Tukio hili la kushangaza limetokea huko Nchini Zimbabwe ambapo mwananume mmoja aliponaswa na kimada ndani ya chumba chake chake cha kulala pale mara baada yaa mkewe kuaga kwenda kuzika!!

Jamaa huyo ambaye alitambulika kwa jina la Leonard Gandaraliamua kumungiza ndani kimada wake huyo ambaye inasemekana walikuwa kwenye uhusiano kwa kipindi kirefu sasa na jambo hilo amekuwa akilifanya mara nyingi na hususani mkewe awapo safarini, Ndipo siku za mwizi zilipotimia siku hiyo mara baada ya mke huyo kuwanasa wagoni hao wakiwa ndani huku wakiendelea kujivinjari.

Mgoni wa kike aliytambulika kwa jina la Memory Mupindu aliainishaa kwamba Leonard alimdanganya kuwa yeye yupo Single na kwamba kitendo cha kumpeleka Nyumbani kwake ni ahadi ya muda mrefu ambayo alikuwa akimuahidi.

Mke wa Leornad alionekana kushikwa na Hasira na kuanza kuwaangushia vichapo vya mbwa mwizi wagoni hao na kudai Talaka yake kwani hawezi tena kuvumilia Aibu nzito kama hiyo ambayo amemletea Mumewe huyo...