Baadhi ya dawa za kukabiliana na makali ya Ukimwi
Huenda
wagonjwa wa Ukimwi wakanufaika na dawa mpya ambayo itawawezesha kutumia
tembe moja kwa siku. Hii ni kwa mujibu wa utafiti mpya nchini Marekani.
Jarida
la Afya Lancet limesema tembe hiyo inajumlisha dawa zote nne
zinazokabiliana na makali ya ukimwi na kwamba ni salama.Utafiti unasema
hii itawarahisishia wagonjwa katika kuhakikisha wanafuata maagizo ya
madaktari wao.
Ukimwi hauna tiba lakini watafiti wameweza kutoa dawa za kukabiliana na maradhi nyemela.
Watafiti
pamoja na kampuni za dawa wamechanganya dawa nne na kutengeneza tembe
moja ili kurahisisha utumizi wa dawa hiyo miongoni mwa wagonjwa.
Tembe inayofanyiwa majaribio na ambayo imechanganywa dawa nne inauwezo wa kudhibiti virusi vya HIV kuongezeka mwilini.
Paul
Sax mtafiti mkuum katika Hospitali ya Wanawake ya Brigham huko
Boston,Massachussetts ambaye pia ni mwanazuo wa ziada wa taasisi ya afya
ya Harvard ameelezea umuhimu wa tembe hii kwa kuimarisha afya ya
wagonjwa.
Dk.
Sax ameongoza utafiti huu ambapo pia wamefanyia majaribio tembe hii kwa
wagonjwa 700 na kusema inafanya kazi, japo kulitokea matatizo ya figo
miongoni mwa waliotumia.
Licha ya mafanikio ya sasa watafiti wanasema raia wengi hawafahamu hali zao ambapo wameendelea kuishi na maambukizi bila kujua.
Chanzo: bbc swahili. http://www.bbc.co.uk/swahili/habari