Pages

Kim Poulsen ataja kikosi cha Kili Taifa Stars kinachovaana na Ivory Coast leo

Jun 2, 2012



Kocha Kim Poulsen ametaja kikosi cha Kilimanjaro Taifa Stars ambacho leo (Juni 2 mwaka huu) kitakuwa uwanjani kwenye Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abidjan kuivaa Ivory Coast katika mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia.
Amefanya mabadiliko katika nafasi mbili kwenye kikosi ambacho Mei 26 mwaka huu kilicheza mechi ya kujipima nguvu na Malawi (The Flames) iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa suluhu.
Amir Maftah atacheza beki wa kushoto badala ya Waziri Salum wakati Mrisho Ngasa atakuwa mmoja kati ya washambuliaji wa mwisho. Ngasa atacheza nafasi ya Haruna Moshi ambaye hayuko na Stars hapa baada ya kuumia mazoezini siku moja kabla ya safari
Kikosi kamili cha Taifa Stars ambayo itatumia mfumo wa 4-4-2 ni kima ifuatavyo
Kipa; Juma Kaseja
Mabeki; Shomari Kapombe, Amir Maftah, Aggrey Morris na Kevin Yondani
Viungo; Shabani Nditi, Salum Abubakari, Frank Domayo na Mwinyi Kazimoto
Washambuliaji; Mbwana Samata na Mrisho Ngasa


Wachezaji wa akiba; Mwadini Ali, Waziri Salum, Juma Nyoso, Erasto Nyoni, John Bocco, Simon Msuva, Jonas Mkude, Christopher Edward na Ramadhan Singano
Kim amesema kikosi chake kimejiandaa vizuri kwa ajili ya mechi hiyo, na kilichobaki ni kwa wachezaji kudhibitisha maandalizi hayo kwenye dakika 90 za mchezo huo utakaoanza saa 11 kamili jioni (nyumbani itakuwa saa 2 kamili usiku).
Mechi hiyo itaoneshwa moja kwa moja (live) kupitia televisheni ya RTI ambapo itaonekana katika nchi 58 duniani