Maandamano ya watoto kuelekea uwanja wa michezo wa Nyamagana yaliyofanyika asubuhi hii jijini Mwanza.
Historia Siku ya Mtoto wa Afrika huadhimishwa tarehe 16, Juni ya kila mwaka. Siku hii inaadhimishwa kwa Azimio la nchi 51 wanachama wa uliokuwa Umoja wa Nchi huru za Afrika (OAU) kwa ajili ya kukumbuka mauaji ya kinyama waliofanyiwa watoto wa kitongoji cha Soweto nchini Afrika ya Kusini mnamo mwaka 1976. |
Lengo la Maadhimisho |
Siku hii huadhimishwa kwa lengo la kukumbuka mauaji ya kinyama
waliofanyiwa watoto nchini Afrika ya Kusini wakati wakidai haki zao za
msingi, pia kuwakumbusha wazazi/walezi na jamii kwa ujumla juu ya haki
na wajibu wa jamii katika kuwalea watoto. Aidha, hutoa nafasi ya
kuwakumbusha watoto haki na wajibu wao kama watoto katika Taifa
|
Maandamano yakikatiza barabara ya Kenyata kuelekea uwanja wa michezo Nyamagana jijini Mwanza.
Kusanyiko la watoto ambao ni wanafunzi ndani ya uwanja wa Nyamagana.
Diwani ambaye pia ni makamu meya wa Halmashauri ya jiji la
Mwanza Mh. Chinchibela akimzawadia kiongozi wa uimbaji wa kikundi cha
watoto toka shule ya watoto wenye mtindio wa ubongo.
Banda la maonyesho kiwanjani hapo.
Maskauti watoto waliojitokeza kusanyikoni.
Meza za mbele kusanyikoni.
Banda la maonyesho na picha za viongozi wa Baraza la Watoto.
Engo ya maonyesho hayo na kazi za mikono ya watoto.
Tafadhali kama unajali soma ujumbe huu.
Watoto waliojipanga vizuri kusanyikoni katika siku ya mtoto wa Afrika mkoani Mwanza.