Pages

MBWA WA WEMA SEPETU APIMIWA MAGAUNI IKIWA NI MAANDALIZI YA NDOA YAKE NA MBWA WA IRENE UWOYA

Jun 2, 2012


Na Imelda Mtema
Staa mwenye jina kubwa Bongo, Wema Isaac Sepetu ambaye aliwahi kuchangia ‘malavidavi’ na mwanamuziki mkali wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’ juzikati aliwaacha watu midomo wazi kufuatia kutinga na mbwa wake kwa fundi cherehani kwa ajili ya kumpima nguo.


Kituko hicho kilishuhudiwa na mwandishi wetu na wapita njia wengine ambapo staa huyo alitinga kwa fundi maeneo ya Kinondoni Kwamanyanya, Dar  kwa ajili ya kumshonea nguo za ‘kisista duu’ mbwa wake ‘aliyembatiza’ jina la Fiona.


Mbele ya fundi, Wema alitoa maelekezo kwamba anataka Fiona ashonewe nguo za rangi mbalimbali ambazo yeye anazo ili wakitoka wote wawe wanamechisha.


Sikia fundi, nataka umshonee nguo za kisista duu za rangi mbalimbali, siku nikitoka naye ‘out’ tunavaa sare, sawa ee?” Alisikika akisema Wema.


Hata hivyo, baadhi ya watu walikichukulia kitendo hicho kama kufuru kwa Mungu wakidai kuwa kuna binadamu wana shida ya mavazi, hivyo ni vyema kama mlimbwende huyo angewasaidia wahitaji hao kuliko mbwa ambaye alivyoumbwa Mungu alimfanya asiwe anavaa nguo.  


Baada ya kumaliza ratiba yake kwa fundi, mnyange huyo alielekea duka la vipodozi kwa lengo la kununua vibanio vya vywele kwa ajili ya Fiona ambaye ana manyoya mengi kwenye paji la uso.


“Unajua mbwa wangu huyu ana manyoya mengi kwenye paji la uso, hivyo nakwenda dukani kumnunulia vibanio vya kubana ili asipate tabu kuona,” alisema Wema.

Hivi karibuni, Wema alidai kuwa Fiona wake huyo ataolewa na mbwa wa Irene Uwoya aitwaye Dallas, akasema maandalizi ya shughuli ya ndoa yanaendelea.