Pages

Sheria ya hatari yaondolewa Misri

Jun 1, 2012

Waandamanaji MisriHali ya hatari ambayo imekuwa ikitumika nchini Misri kwa miongo mitatu na kuyapa majeshi ya usalama ya Misri madaraka ya kupindukia kwa kuwakamata washukiwa na kuwafikisha katika mahakama maalum, imeondolewa.
Sheria ya hali ya hatari ilianzishwa mwaka 1981 na Rais Mubarak, kufuatia mauaji ya mtangulizi wake, Anwar al-Sadat.
Watawala wa kijeshi wa Misri ambao walitwaa madaraka baada ya Rais Hosni Mubarak kung'olewa madarakani mwaka jana walionyesha kuwa wasingeirejesha tena sheria hiyo baada ya kumalizika muda wake usiku wa kuamkia leo.
Kuondolewa kwa sheria hiyo, lilikuwa dai kubwa la waandamanaji wapenda demokrasia ambao walichochea uasi dhidi ya Bwana Mubarak.