Pages

Zena Mondi anyakua taji la Redd's Miss Singida

Jun 2, 2012

Redd's Miss Singida 2012,Zena Mondi (katikati) akiwa na mshindi wa pili Rehema Marwa (kushoto) na wa tatu Eliza Diamond mara baada ya kumalizika kwa shindano lao na kutangazwa mshindi.shindano hili limefanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Aqua mjini Singida



                     warembo waliongia tano bora

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akikabidhi zawadi kwa Zena Mode, baada kuibuka mshindi, shindano la Redd's Miss Singida, lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Aqua mjini Singida. Mshindi wa kwanza amepata sh. 400,000, wapili sh. 300,000 na wa tatu sh. 200,000. Akifungua shindano hilo, Nape ameahidi kwamba CCM itatoa ajira kwa Miss Singida kama atafanikiwa kuingia katika tatu bora katika shindano la Miss Tanzania na kwamba CCM inayatambua mashindano ya urembo hapa nchini.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimtuza Khadija Kopa wakati akitoa burudani katika shindano hilo

Muimbaji wa muziki wa Taarab nchini,mkongwe Khadija Kopa akitumbuiza mashabiki wakati wa shindano hilo mjini Singida.Picha na Bashir Nkoromo