Pages

PICHA MOJA ZAIDI MALIMI KATIKA POZI

Jul 26, 2012
Read more ...

BUGURUNI WAONJA JOTO LA JIWE KWA WIZI WA UMEME

Jul 25, 2012
Mtuhumiwa wa wizi wa umeme Jeilan Mohamed, akiongozwa na jeshi la polisi kupanda gari baada ya kutuhumiwakuliibia umeme shirika hilo kwa njia ya kuunganisha kabla haujafika kwenye mita (kubaipass) maeneo ya Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam. 




WATU watano wakazi wa Buguruni jijini Dar es Salaam wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za wizi wa umeme kufuatia operesheni kaliinayoendeshwa na shirika la umemem Tanzania kupitia kanda zake za Ilala, Kinondoni na Temeke.
Kwenye zoezi hilo ambalo juzi lilifanyika kwenye maeneo ya buguruni watu watu watano walikutwa wakiiba umeme kwa njia ya kuchezea mita kwa kuchukua umeme kabla haujafika kwenye mita ambayo kitaalamu hujulikana kama (bypass).
  
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye eneo la tukio Meneja wa Shirika hilo kanda ya Ilala Athanasius Nangali amesema kuna kila sababu ya zoezi hilo kuwa endelevu kutokana na watu wengi kuiba umeme.
Nangali amesema tatizolililopo kwa sasa sio la wateja wapya wanaounganishiwa sasa bali ni la wateja wazamani wanachezea mita ili waibe jambo ambalo halikubaliki hata kidogo.
“Akitoa mfano wa kwenye nyumba ambayo inamilikiwa na mmoja wa watuhumiwa hao ambaye ni Jeilan Mohamed, huyu ni mteja wetu wa siku nyingi lakini umeme aliokuwa akiiba ni asilimia 75 na kulitia hasara shirika hilo.
Aidha katika hatua nyingine ya kuongeza nguvu kwenye zoezi hilo Meneja huyo ametoa ofa kwa yeyote atakaetoa siri na kusaidia kukamatwa mwizi wa umeme atapata zawadi ya Tsh.50,000 kwa kila nyumba itakayokutwa inaiba umeme.
Akijibu maswali ya waandishi waliotaka kujua ufanisi wa zoezi hilo Nangali alisema linamafanikio makubwa kwani hadi sasa wamefanikiwa kukusanya zaidi ya Tsh 80millioni.
Aidha nangali pia ametoa ofa kwa wezi watakaojisalimisha wenyewe wataepuka kufikishwa mahakamani lakini badalayake watalazimika kufanyiwa hesabu ya umeme walioiba na kuulipia katika kipindi chote cha wizi.
Zoezi hilo linaendelea tena maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
 
CHANZO
Read more ...

UMEPITIA MISHE MISHE KAMA HII?

Jul 25, 2012
Read more ...

AJALI MBAYA YATOKEA MBEZI

Jul 25, 2012














Ajali hii imetokea maeneo ya Mbezi Afrikana jijini Dar es Salaam leo ambapo Lori hili lenye nambari za usajili T 545 BPU lililokuwa likimwaga mchanga na kujikuta likipiga mweleka na kuangukia Gari ndogo aina ya Toyota Rav4 yenye nambari za Usajili T839 BSL iliyokuwa imepaki katika eneo hilo. Hakuna mtu aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa katika ajali hiyo.
Read more ...

STORY KUHUSU KUPOTEA KWA MAMA YAKE MICHAEL JACKSON

Jul 24, 2012
Katherine JacksonHivi juzi kati  mpwa wake michael jackson alieleza kuwa Bi katherine mwenye miaka 82  ambaye ni mama yake mzazi michael jackson alipotea usiku wa jumamosi ,laikini katika interview iliyofanywa kati ya Los Angeles Sheriff's Department na kituo kimoja cha habari huko marekani kimeeleza kuwa Bi katherine yuko poa na hana matatizo yoyote na wengeweza kuonesha ni wapi alipo
Read more ...

BAADA YA KWAYA YA BUGANDO KUZINDUA ALBUM YAO SASA AIC PASIASI WAZINDUA YAKWAO

Jul 24, 2012

KWAYA YA UINJILISTI AIC (T) PASIANSI MWANZA WAZINDUA ALBUM 'TUHURUMIE'

Kwaya ya AIC Unjilisti Pasiansi.


Shughuli imefanyika katika viwanja vya nje ya kanisa la AIC Makongoro jijini Mwanza.

Mgeni rasmi bwana Eng. Robert Lupoja pamoja na mkewe Mrs Lupoja na Mr. Benjamin Kijika wakiangalia jinsi waimbaji wanavyomtukuza Mungu kwa uimbaji wao mzuri.
Ilifana vya kutosha.


Radio Presenter wa Kwaneema Fm Maria Philbert naye alikuwa shuhuda wa kile kizuri ambacho kilitendeka jana kwenye uzinduzi.


Eagt Uinjilisti Kwaya nao wakipata flsh huku wakiwa wamekaa wakiwatch shughuli nzima.


Aic Vijana Kwaya Bwiru.


Mgeni rasmi bwana Eng. Robert Lupoja pamoja na mkewe Mrs Lupoja akinunua nakala ya kwanza ya kwaya hiyo kuashiria uzinduzi.


Aic Mwananchi kwaya.

Aic Uinjilisti Pasiansi Kwaya wakiimba wakti wakizindua albam yao ya Tuhurumie.

Hapa wakiimba wimbo wa albam Tuhurumie.

Kwaya ya AIC Uinjilist Pasiansi leo jumapili wameweza kuzindua albam yao ya video kwa kishindo huku wakiwa wamepata takribani 5..9 milioni wakiwa na malengo wa kutafuta milioni 50 kwa ajili ya ununuzi wa coaster, uwanja wa kujenga hosteli ya wageni pamoja na vyombo vya muziki. Mungu ibariki kazi yao AMEN.  


Chanzo www.gsengo.blogspot.com 
Read more ...

AJALI MBAYA YA BASI YATOKEA IRINGA USIKU WA KUAMKIA LEO

Jul 23, 2012

 Hili ndilo basi la Tony Sley ambalo limepata ajali jana usiku na kuua watu watatu na kujeruhi 38





Majeruhi wakisubiri matibabu Hospitali ya mkoa wa Iringa.


Majeruhi wa basi la Tony Sley Bi Agnesy Lukasi akiwa na mtoto wake Dina Lukasi (4) wakisubiri kupewa matibabu katika Hospital ya mkoa wa Iringa baada ya kufikishwa hapo usiku huu wakitokea eneo la ajali mlima wa Kitonga






Majeruhi wakipatiwa huduma Hospitali ya mkoa wa Iringa

Ajali ya basi ya Tony Sley yenye namba za usajili T 218 ACH lililokuwa likitokea Tunduma mkoani Mbeya kwenda jijini D’Salaam imeua watu watatu wakiwemo wawili raia ya Zambia na mmoja mtanzania na kujeruhi wengine 38.

Ajali hiyo imetokea katika eneo la kona za mlima wa kitonga kwenye barabara kuu ya Iringa –D’Salaam jana majira yasaa 12 za jioni baada ya dereva wa basi hilo kushindwa kulipita lori lilolokuwa mbele yake.

Wakizungumza katika eneo hilo na Hospitali ya mkoa wa Iringa majeruhi wa ajali hiyo waliolazwa katika hospitali yawilaya ya Kilolo Ilula walisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wao alisema Agnes Lukasi (30).

Agnesy alisema kuwa kwa upande wake alikuwa amekaa siti ya mbele na wakati dereva huyo akifanya uzembe huyowalikuwa wakimshuhudia hata kujaribu kumuonya bila mafanikio.

Alisema kuwa katika basi hilo alikuwa na mtoto wake Dina Lukas (4) ambaye pia amejeruhiwa katika paji lake la uso.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamhanda ambaye alifika eneo la tukio pamoja na mkuu wa kikosi chausalama barabarani mkoa wa Iringa aliuthibitishia mtandao huu kuwa jumla ya abiria 38 ndio waliojeruhiwa katika ajalihiyo.

Aliwataja baadhi ya majeruhi ambao majina yao yamepatikana na kulazwa katika hospital teuli ya mkoa wa Iringa kuwa ni pamoja na Boyd Simwings(43) , Violet Chambale(35),Zilombo Wake(38),Warmen Mambwe (33),Eugen Maluge(39), Mwamba Andrew (27) , Bright Mwalukanga (33) na John Lemba( 30) wote raia wa Zambia.

Wengine ni Martine Shombe( 29) mkazi wa Tunduma, Zainabu Amuri (32) mkazi wa D’Salaam , Efrain Mwampashi (31) mkazi wa Tunduma, Sebastian Mhaya(25) mkazi wa Tunduma, Vedastus Benjamin (11) mkazi wa Tunduma, Mrashi Handu (38) mkazi wa Igulusi, Juma Ramadhan (40) mkazi wa Tunduma, Twaribu Juhim (39) mkazi wa Arusha, Muka Muka (26) mkazi wa Tunduma, Edina Ramadhan (3) mkazi wa Tunduma na Benjamin Enock (33) mkazi wa Mbeya.

Wengine ni Agness Lukas (30) mkazi wa Tunduma , Dina Lukas (4) mkazi wa Tunduma Beatrice Msakanti( 42) mkazi wa Zambia, Besa Shadrack (32) mkazi wa Zambia na Mary Mumba (48) mkazi wa Zambia pia.

Alisema majina ya majeruhi zaidi yatapatikana hivi karibuni baada ya majeruhi waliopo Hospital ya wilaya ya Kilolo Ilula kufika mjini Iringa.

Mbali ya majeruhi hao pia aliwataja waliopoteza maisha katika ajali hiyo kuwa ni Cla Pily (32) na Dany Kawina (43) wotewafanyabiashara raia wa Zambia pamoja na Abel Nelson (32) ambaye ni mtanzania.

Kamanda Kamhanda mbali ya kueleza masikitiko yake juu ya ajali hiyo bado aliwaonya madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuendesha kwa uangalifu wa hali ya juu na kuwa jeshi lake mkoani Iringa halitalala kuwabana madereva wazembe. Chanzo: 
Read more ...

ENGINEER WA VODACOM APATA PIGO KALI, AFIWA NA MKEWE

Jul 23, 2012


Marehemu Belinda J. Mwapinga enzi za uhai wake.
Marehemu Belinda J. Mwapinga alifariki tarehe 20/07/2012 katika Hospitali ya Muhimbili na mazishi yake kufanyika tarehe 23/07/2012 katika makaburi ya Kinondoni.

Baba Padre akitoa heshima yake ya mwisho kwa mwili wa Belinda. J. Mwapinga jana katika Kanisa la Katoliki Extenal Dar es salaam
Joseph Mwapinga mwenye suti nyeusi akiwa na watoto wake alio achiwa na mke wake kipenzi Belinda.
Wafanyakazi wa VODACOM Tanzania wakiwa wamebeba mwili wa Marehemu Belinda wakiufikisha katika makaburi ya Kinondoni.
Mhandisi Joseph Mwapinga akiweka shada la mauwa kwenye kaburi la Mke wake.
Hawa ni baadhi ya waombolezaji waliohudhuria kwenye safari ya mwisho ya Belinda.
Read more ...

DEMU ALIYEONEKANA KATIKA VIDEO YA DIAMOND(MOYO WANGU )AHAMIA KWENYE TASNIA YA USAGAJI

Jul 23, 2012

Yule dem aliyecheza video ya moyo wangu 
Read more ...