Wanaharakati nchini China wanasema kuwa vijana watatu watawa wa
Tibet pamoja na mama mmoja walijiteketeza mkesha wa kongamano la chama cha
tawala cha kikomunisti nchini China.
Shrika la Free Tibet linasema kuwa mmoja wa watawa hao alifariki katika kile inachosema ni idadi kubwa ya watu kujiteketeza kama njia ya kuonyesha kukerwa na utawala wa china.
Matukio ya hivi karibuni ya watu kujiteketeza moto katika maeneo ya china yaliyo na watu wa Tibet yamefikisha idadi ya watu hao wanaojiteketeza kuwa zaidi ya watu sitini tangu mwaka jana.
Wengi wao wamefariki. Na huenda kuna umuhimu katika wakati ambapo visa hivi vimetokea.
Kuimarishwa kwa usalama kote China kwa kongamano la chama tawala cha kikomyunisti nchini, hakujazuia malalamiko ya raia wa Tibet dhidi ya utawala wa China. Badala yake yameongezeka.
Wanaharakati wanasema idadi ya watu kujiteketeza kwa muda wa siku moja, hii leo, haikutarajiwa.