Pages

HIKI NDICHO KILICHOTEKEA JANA KWENYE VURUGU ZA MACHINGA NA ASKARI WA JIJI LA MWANZA

Nov 16, 2012

Polisi wakiwa kwenye doria eneo la tukio.
 Mtu mmoja ameuawa na wengine wawili kujeruhiwa kufuatiaa vurugu zilizotokea leo majira ya saa tano asubuhi  katika eneo la barabara ya Pamba karibu na soko kuu la jijini Mwanza katika vurugu baina ya wafanyabiashara wadogo maarufu kama wamachinga na askari wa Halmashauri ya jiji la Mwanza.

Mtu huyo ambaye jina lake kamili halikupatikana badala yake ametambuliwa kwa jina moja tu la Greda.

Taarifa zaidi zinasema kuwa leo mnamo majira ya saa nne na nusu asubuhi askari wa halmashauri ya jiji la Mwanza wakiwa katika maeneo yao ya kazi eneo la barabara ya Pamba kwenye stendi ya zamani ya mabasi ya Tanganyika karibu na soko kuu la jiji hilo, wakiwa katika operesheni zao za kawaida za kusafisha jiji walikamata bidhaa zilizokuwa zimepangwa katika maeneo ambayo hayaruhusiwi kisheria wakiwa kwenye eneo hilo mtu mmoja ambaye anadaiwa kuwa ni mmachinga alimrukia mgambo wa jiji shingoni na kumtolea silaha ya jadi aina ya sime kwa nia ya kumdhuru.

Maganda  ya risasi zilizo tumika.
 Baada ya tukio hilo wamachinga waliokuwa eneo la tukio walianza kuwarushia mgambo hao wa jiji mawe ndipo wale mgambo wa jiji katika kujihami wakaanza kurusha risasi hewani kuwatawanya wamachinga hao  waliokuwa wakiongezeka kadri kuanza kwa seleka hilo, kwa bahati mbaya moja kati ya risasi hizo zikampiga mpiga debe mmoja upande wa kushoto na kufariki papo hapo.

 Machinga mwingine amejeruhiwa kwenye mkono wa kushoto katika kiwiko, naye dereva wa magari ya  biashara za kusafirisha mizigo wa gari aina ya Kenta, magari ambayo hupaki katika eneo hilo amejeruhiwa upande wa kushoto kichwani na kukimbizwa hospitali ya rufaa Bugando kwa matibabu. 



Mmoja wa viongozi wa akiwatuliza wamachinga wenzake kupata kumsikiliza mkuu wa polisi (OCD) wa wilaya ya Nyamagana Ally Kitumbu. .

Msikilize kwa kubofya play..
Mkuu wa polisi (OCD) wa wilaya ya Nyamagana Ally Kitumbu. akizungumza na wafanyabiashara hao wadogo (wamachinga) kuendelea na kazi kwa kufuata sheria wakati jeshi hilo likifanya uchunguzi wa tukio hilo.

Msikilize kwa kubofya play...
Maduka mengi hususani yaliyo karibu na eneo la tukio yamefungwa kufuatia seleka hilo.

Makutano ya barabara za Liberty na Nyerere ambalo muda wote huwa na pilikapilika za kibiashara likionekana tupu kutokana na vurugu hizo zilizo sababisha wafanyabiashara kukimbia na kufunga biashara zao kuhofia vurugu hizo.

Mmoja kati ya viongozi wa wamachinga akizungumza na wenzake kuwasihi kulinda utulivu ili haki yao isipotee.