Pages

BETHDAY YA BEBY MADAHA NI POMBE TU.....

Nov 23, 2012
POMBE, vituko na ngono njenje vilitawala katika ‘bethidei’ ya staa wa filamu na muziki Bongo, Baby Joseph Madaha, Ijumaa lilihudhuria. 
 Matukio hayo yalijiri Novemba 19, mwaka huu katika Baa ya Uhuru Peak Kinondoni jijini Dar, wakati staa huyo alipofanyiwa pati ya kusherehekea kuzaliwa kwake akitimiza miaka 26.

 Waandishi wetu waliohudhuria pati hiyo walishuhudia marafiki wa msanii huyo wakipombeka na baadhi walipozidiwa 
walifanya mambo ya ngono hadharani.
Msanii wa filamu Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ alinaswa akiwa na mwanaume aitwaye Boniface wakidendeka hadharani huku wengine wakipiga makele na kucheza kihasara kiasi cha kuligeuza eneo hilo kuwa la pombe na ngono.