Pages

Breaking News: Mhashamu Askofu Alosius Balina afariki dunia

Nov 6, 2012
MHASHAMU Askofu mkuu wa Jimbo la Shinyanga Kanisa katoliki amefariki dunia akiwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando alikokuwa akitibiwa.
Historia yake:
Mhashamu Askofu Aloysius Balina alizaliwa Juni 21, 1945 katika kijiji cha Isoso Ntuzu wilayani Bariadi mkoani Shinyanga na aliwekwa wakfu na Papa Yohane Paulo II mwaka 1984 kuwa Askofu wa Geita na kusimikwa Machi 10, 1985.
Septemba 23, 1997 alihamishiwa Jimbo la Shinyanga na kuwa Akofu wa tatu wa Jimbo la Shinyanga hadi mauti yalipomkuta, huku watangulizi wake wakiwa Askofu Edward A. McGurkin, aliyetumikia cheo hicho toka mwaka 1956 hadi 1975, alifariki Agost 281983 huko Marekani, wa pili ni Askofu Castor Sekwa, aliyetumikiwa kuaznia mwaka 1975 hadi Juzi 6, 1996 alippofariki na askofu Balina kushika nafasi yake.

Taarifa kamili zitatolewa bwana alitoa na bwana ametwaa jina la bwana lihadudiwe mungu ailaze mahali pema pepon amenn..