Pages

MISUKULE YAZUA TAFRANI IRINGA POLISI YATAWANYA WATU KWA MABOM

Nov 22, 2012

Wananchi wakiwa wamekusanyika eneo la Mwangata mjini Iringa baada ya uvumi kuwa kuna msukule kaonekana eneo hilo.
Polisi wakidumisha amani na kuwasaka walioeneza uvumi huo.
Shughuli zikiwa zimesimama baada ya taarifa hizo za kuwepo msukule.

ZIMEZUKA  habari  zenye utata ambazo hazijathibitishwa mkoani Iringa  kuwa mtoto mmoja anayedaiwa kufa na kuzikwa  kuonekana leo akidaiwa kuwekwa Msukule.
Tukio  hilo  limetokea eneo la Mwangata mjini Iringa  na kupelekea  polisi  kufika  kuwatawanya  wananchi waliokusanyika eneo hilo na kuwasaka  wale wanadaiwa kueneza uvumi huo.
Hata  hivyo hakuna mwananchi hata mmoja kati ya  waliokuwepo eneo hilo ambaye amethibitisha  kuona msukule  huyo zaidi ya kila mmoja kusema amesikia.
Wananchi hao wameizunguka moja kati ya nyumba eneo hilo wakitaka  kuichoma moto kwa madai kuwa ndani kuna msukule  huyo.

Habari / Picha kwa hisani ya : FRANCIS GODWIN BLOG