Rais Barack Obama, anatarajiwa kushauriana na viongozi wa bunge
la Congress, kwa mara ya kwanza hii leo, tangu alipochaguliwa kwa awamu
nyingine, kujaribu kuzuia kutokea kwa mzozo wa bajeti.
Ikiwa rais Obama na viongozi hao hawataafikiana lolote kabla ya mwisho wa
mwaka huu, viwango vya ushuru vitaongezeka na serikali italazimika kupunguza
matumizi yake, kwa mujibu wa sheria mpya itakayoanza kutekelezwa mwezi januari
mwakani.Rais Obama, tayari amesisitiza kuwa raia wa nchi hiyo wenye mapato ya juu, washurutishwe kulipa ushuru zaidi lakini chama cha republican, ambacho kina idadi kubwa ya wabunge katika bunge hilo,kimepinga vikali pendekezo hilo la raisObama.