Dada yake Michael Jackson, Janet Jackson amesilimu kuwa muislamu na atafunga ndoa ya kiislamu na mpenzi wake bilionea wa Qatar, Wissam Al Mana mwanzoni mwa mwaka ujao.
Sherehe ya kukata na shoka ambayo inatarajiwa kufanyika kwenye mji wa Doha, Qatar inatarajiwa kugharimu mamilioni ya dola ambapo bilionea huyo wa Qatar anataka kuifanya harusi yake iingie kwenye historia ya harusi bora kuliko zote duniani.
Sherehe ya kukata na shoka ambayo inatarajiwa kufanyika kwenye mji wa Doha, Qatar inatarajiwa kugharimu mamilioni ya dola ambapo bilionea huyo wa Qatar anataka kuifanya harusi yake iingie kwenye historia ya harusi bora kuliko zote duniani.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani zilizopatikana Janet na mchumba wake huyo wamepanga kutumia dola milioni 3 kwaajili ya kuwakodishia ndege za kuwaleta wageni wapatao 500 watakaohudhuria harusi hiyo.
Katika kuhakikisha kuwa wanaifanya harusi yao inakuwa ya kifahari zaidi, bilionea huyo wa Qatar amepanga kuwazawadia wageni wote watakaohudhuria sherehe hiyo saa ya kifahari aina ya Rolex yenye thamani zaidi Tsh, milioni 20. Kila mgeni atapata saa hiyo kama shukurani ya kutumia muda wake kuhudhuria harusi hiyo.
"Itakuwa ni harusi ya karne, Wissam amepanga kumwaga pesa kuifanya harusi yake na Janet iwe ya kipekee", alisema mtu mmoja wa karibu na wapenzi hao.
Janet mwenye umri wa miaka 46 alikutana na Wissam ambaye ni mdogo kwa miaka takribani 10 mnamo mwaka 2009 wakati Janet alipotembelea nchi za Mashariki ya kati na kufanya shoo maalumu kwenye nchi hizo.
Janet na Wissam walianza mapenzi yao mnamo mwaka 2010 na walivalishana pete za uchumba mwaka jana ambapo Wissam alimvalisha Janet pete ya uchumba ya almasi yenye carat 15.
"Mama yangu alitulea na kutufundisha tuamini kuwa umri ni namba tu", alisema Janet wakati alipoulizwa kuhusiana na umri wake mkubwa kulinganisha na Wissam.