Pages

GEORGE ENTWISTLE AJIUZULU UKURUGENZI BBC.

Nov 16, 2012

Mkurugenzi aliyejiuzulu, George Entwistle.Mkurugenzi aliyejiuzulu, George Entwistle. BBC
Mkurugenzi Mkuu wa British Broadcasting Corporation au BBC, George Entwistle amejiuzulu wadhifa huo baada ya kushutumiwa kushindwa kushughulikia vyema taarifa iliyorushwa katika kipindi cha TV cha NewsNight.
Taarifa hiyo kwa makosa ilimshutumu aliyekuwa Waziri wa Fedha wakati wa serikali ya Conservative , Lord McAlpine, kwamba alihusika katika kashfa ya kudhalilisha watoto
BBC tayari wameshaomba radhi kutokana na kurusha taarifa hiyo na kama kuonyesha kusikitishwa kwake na kitendo hicho, George Entwistle amejiuzulu. Katika speech yake aliyoisoma wakati akitangaza kujiuzulu kwake, George alisema:
“Nilipopewa kazi hii, ambapo nilikuwa na uzoefu wa miaka 23 kama mtayarishaji na kiongozi wa BBC, nilikuwa na imani kwamba uongozi wa BBC ulimchagua mtu sahihi kufanya kazi hii. Hata hivyo,matukio tofauti ambayo yamekuwa yakitokea week hizi chache yamenifanya nifikie kuona kwamba BBC inahitaji kuchagua kiongozi mpya.”
Tim Davie,mkurugenzi wa BBC Audio & Music ambaye ndio aliyekuwa anasemekana kuchaguliwa kuwa CEO wa BBC Worldwide, atashika wadhifa wa Mkurugenzi Mkuu kwa muda wakati yule wa kudumu akitafutwa. Entwistle amefanya kazi hiyo kwa muda wa miezi miwili tu.