Pages

MAJANGA HAYA; ANGALIA PICHA NAMNA : KIJANA WA ROMBO AFYEKA NYETI ZAKE, KISA NI MADEMU

Nov 16, 2012
Kijana Priva Elian wa Rombo mkoani Kilimanjaro, amefyeka sehemu zake za siri na kuziondoa, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kugombaniwa na wanawake wawili.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo, walidai kijana huyo alifikia uamuzi huo baada ya wanawake wawili kumgombea.
Walidai kuwa alifikia uamuzi , mwaka huu saa 1:30 asubuhi baada ya kupandwa na ghadhabu kutokana na usumbufu mwingi aliokuwa akiupata kutoka kwa wanawake hao.
 

Walieleza kuwa mara baada ya kuchukua uamuzi huo, alimwita mdogo wake ambaye hakutambulika jina na kumweleza kuwa achukue viungo hivyo na kuwapelekea wanawake hao ili wavigombee.
 

“Hatujui alitumia kifaa gani kujifyeka kwani kinaonesha ni kikali sana, kwani baada ya kukata sehemu hizo nyeti, alimpa mdogo wake ili awapelekee wanawake hao kwani ndicho kitu muhimu kwao na siyo yeye,” alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo la kusikitisha.