KLABU ya Simba ya Dar es Salaam imemuongezea mkataba wa miaka miwili kocha wake Mserbia, Profesa Milovan Cirkovic baada ya kuridhishwa na kazi yake kwa kipindi cha nusu msimu alichokuwa na timu hiyo tangu arithi mikoba ya Mganda, Moses Basena >Mwandishi Bin Zubery wa bongostaz.blogspot.com ameandika kwamba Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amesema kwamba Milovan atakuwa kocha wa Simba kwa miaka miwili zaidi tangu sasa baada ya kuongezewa mkataba.Kipimo cha mafanikio ya kocha ni mataji na soka safi, kitu ambacho sisi kama viongozi tumekishuhudia Simba chini ya Profesa Milovan, sasa hatuoni kwa nini tusimuongeze mkataba,”alisema Kaburu Pamoja na kuipa ubingwa wa Ligi Kuu ya Bara kwa kishindo, Milovan aliiwezesha Simba kufika hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambako ilitolewa kwa penalti 9-8 na Al Ahly Shandy ya Sudan, baada ya sare ya jumla ya 3-3.
KOCHA MILOVAN WA SIMBA AONGEZEWA MKATABA, STORI KAMILI NDIO HII!
May 21, 2012