Pages

MJADALA KUHUSU LUGHA WAZUA TAFRANI BUNGENI NCHINI UKRAINE

May 26, 2012


Mjadala katika bunge la Ukraine kuhusu sheria ambayo ingeruhusu lugha ya Kirusi kutumiwa katika mahakama, hospitali na taasisi nyingine katika maeneo ya Urusi ambayo wakazi wake wanazungumza Kirusi umesababisha bunge hilo kugeuka kuwa jukwaa la masumbwi baada ya wanasiasa kurushiana ngumi. 


Wabunge wa chama cha rais Viktor Yanukovich wanataka lugha ya Kirusi ikubaliwe kama lugha rasmi ya pili nchini humo, lakini upinzani unaounga mkono sera za magharibi unapinga sheria hiyo.
Kufuatia tafrani huyo ya kupigana ilibidi mbunge mmoja wa upinzani apelekwe hospitali baada ya purukushani hiyo.