Pages

ZANTEL YA DHAMINI BONGO STAR SEARCH 2012, NA KUTOA ZAIDI YA MIL. 50 NA SASA KUITWA EPICBSS AU EBSS

May 22, 2012
Add caption
Afisa Mkuu wa Biashara wa Zantel Ahmed Mokhles (kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kampuni ya simu za mikononi Zantel kutangaza kuidhamini kipindi cha televisheni cha kitanzania Bongo Star Search 2012 kwenye awamu yake ya sita tokea ianzishwe, ambayo itajuliakana kama 'Epiq Bongo Star Search' (EBSS). Bw. Ahmed Mokhles aliongezea kuwa Zantel inatambua uwezo na nafasi ya vijana katika jamii na ndiyo maana kampuni hiyo imejikita katika kutoa huduma ambzo zinawalenga vijana moja kwa moja na sasa huduma imeandaliwa kwa vijana wa Epiq Nation inayounganiswa na Bongo Search katika kukuza na kuendeleza vipaji ambavyo vijana wa kitanzania wanavyo
Pia alisema kuwa katika kuboresha shindano hilo mwaka huu Zantel imejumlisha kipengele cha mitindo ambapo wabunifu wachanga watashiriki katika kuwavalisha wanamuziki ambao watatazamwa na wabunifu weledi. Pembeni ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benchmark, Bi. Ritha Poulsen.   

 Mtangazaji wa Clouds Fm Fetty ambaye alikuwa ni mshereheaji katika hafla fupi ya kutangaza na kuzindua Epiq Bongo Star Search 2012 iliofanyika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.