Pages

ALICHOSEMA MWAKILISHI WA ZIMBABWE BBA KUHUSU KANUMBA

May 16, 2012
Japokua ni zaidi ya siku 30 zimepita toka Steven Kanumba kufariki dunia, Mwakilishi wa Zimbabwe kwenye jumba la big brother mwaka huu, Tecla alietolewa weekend iliyopita, ambae pia ni mwimbaji na mwigizaji staa kwenye nchi yake, ameithibitishia AMPLIFAYA leo kwamba hakua na taarifa za kifo cha mwigizaji huyo mpaka alipokutana na Mtanzania Hilda kwenye jumba la Big Brother
Anasema alivutiwa na uigizaji wa Marehemu Steven Kanumba na kuwa shabiki wake na ndio alikua mwigizaji pekee aliemfahamu kutoka Tanzania ambapo kwa mara ya kwanza alimfahamu Kanumba kupitia Tv ya Africa Magic mwaka jana wakati alipoanza kutumia muda wake mwingi kutazama Tv.