Pichani mtoto Neema George aliyegundulika kuwa na matundu matatu kwenye moyo.
Mtoto Neema George (16) amewaomba wasamaria wema wajitokeze kumchangia fedha ili akapate matibabu ya moyo nchini India. |
Hali ya Neema George inazidi kuzorota siku baada ya siku, miguu ikiwa imevimba, akitaabika katika suala la kula, kuongea na akipata maumivu makali ya tumbo hasa nyakati za usiku
Baba mzazi wa Neema, George Mugunga (kushoto);anasema kuwa mnamo mwaka 2010 mara baada ya hali ya mtoto wake kuzorota alimfikisha katika hospitali ya Rufaa Bugando kwaajili ya matibabu, lakini mara baada ya vipimo kufanyika vikaonyesha kuwa moyo wa mtoto wake una matundu matatu.
Baadhi ya vithibitisho vya tiba
adaktari kupitia kliniki aliyokuwa akipata huduma (Bugando) wamesema kuwa tatizo la neema ni kubwa na haliwezi kupatiwa ufumbuzi hapa nchini bali linaweza kupata tiba Nchini India kwa makadirio ya gharama ya shilingi za kitanzania milioni 25.
Baba wa mtoto huyo aitwaye George Lenatus Mugunga amewaomba wasamaria wema, makampuni, wanasiasa, viongozi wa dini, wafanyabiashara na watu binafsi walioguswa na tatizo la mtoto Neema, kuwasiliana naye kupitia namba za simu ya kiganjani 0755424086 au kufika Ofisi za mkuu wa mkoa wa Mwanza ili kupata utaratibu wa kufikisha msaada huo haraka iwezekanavyo
habari hii chanzo ni michuzi blog na gsengo blog